Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala mbalimbali zinazowekwa katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio.
Napenda kukupongeza kwa hatua uliyochukua ya kuamua kutembelea mtandao huu kwa ajili ya kuchota maarifa ambayo yatakusaidia katika maisha yako na pia kukushukuru kwa ajili ya kuwashirikisha marafiki wengine waungane nasi kwa ajili ya kuendelea kuboresha maisha yetu.
Katika makala yetu ya leo napenda kukushirikisha sababu kumi (10) ambazo zinatumika kama pazia la kujifichia au kisingizio cha kusababisha watu wasianze kutengeneza biashara zitakazohudumia watu na hatimaye kuwaingizia kipato.
1. Kukosa fedha (mtaji) kwa ajili ya kuanza biashara.
2. Kuwa na idadi kubwa ya ndugu au jamaa wanaokutegemea kwa ajili ya kuwasaidia kwa huduma mbalimbali kama mahitaji muhimu, elimu na kadhalika.
3. Kukosa mawasiliano na watu ambao wataweza kukuunga mkono katika biashara yako.
4. Kukosa uwezo wa kutosheleza wa kuanza , kuendesha na kusimamia biashara yako.
5. Kukosa muda wa kuendesha na kusimamia biashara kutokana na kutingwa na shughuli nyingine.
Soma Makala Hii Inayohusiana : Mambo Matano (05) Yanayosababisha Kushindwa
6. Kukosa mtu sahihi ambaye anaweza kukuongoza hatua kwa hatua katika biashara mpaka uweze kusimama mwenyewe.
7. Umri wako umeshakwenda sana.
8. Uhitaji wa muda mwingi kutoka kuanza biashara mpaka kukua na kuendelea.
9. Kuchukia kushughulika na wafanyakazi ambao unatakiwa kuwasimamia.
10. Hofu ya kuwa na biashara ni hatari (risky).
Rafiki hizi ni baadhi tu ya sababu zinazotumiwa, je ni sababu ipi umeitumia kujitetea kama hoja ya msingi ambayo inakuzuia mpaka sasa kuanza kutengeneza biashara?
Tafadhali nishirikishe maoni yako kwa kutaja sababu ipi ambayo unaona ndiyo kikwazo kikubwa au kunitajia sababu nyingine unazozifahamu, ili tuweze kuzijadili katika makala zijazo.
Rafiki napenda kukuarifu kuwa ikiwa una maswali au mada ambayo ungependa niiandikie makala , unaweza tuma katika anuani yangu luckmoshi@gmail.com
Goodluck Moshi
Mwandishi
StadizaMafanikio