Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio!
Darren Hardy ni mwandishi wa kitabu cha THE COMPOUND EFFECT. Katika kitabu hiki mwandishi anatueleza siri kubwa iliyopo katika kufanya mambo hatua kwa hatua kidogo kidogo ili kufikia mafanikio. Hapa tunajifunza kuwa mafanikio ni mchakato na sio kitu ambacho kitatokea mara moja. Hapa chini ninakushirikisha yale mambo ambayo nimejifunza.
1. Fanya maamuzi ya kudhibiti/kuyaongoza maisha yako kwa kutafuta kujifunza kutoka kwa watu waliofanikiwa na kuyaweka katika katika miaka yako ambayo una nguvu/mapema kabla umri haujaongezeka sana
2. Kama unahitaji mafanikio makubwa wasaidie wengine wafanikiwe zaidi
3. Amua kufanya maisha yako kuwa maabara yako binafsi kwa ajili ya kujaribu kanuni mbalimbali za mafanikio kufanyiwa mafunzo na utafiti
4. Maamuzi yako yanatengeneza hatma yako
5. Maamuzi yako unayoifanya kila siku yanaamua kukuwezesha kufikia maisha unayotaka au kufikia maafa ya maisha unayotaka
6. Kama hujui kitu fulani weka jitihada na unadhifu katika kujifunza mpaka uweze kukivuka kikwazo
7. Si jambo/hatua nzuri ya mafanikio katika maisha kwenda pamoja na kundi (kimazoea) kuwa mtu ambaye anafanya mambo ya tofauti na makubwa
8. Unahitaji ari na uwajibikaji ili kuweza kuyafikia mafanikio unayoyahitaji
9. Tengeneza fedha na mali za kutosheleza kutunza familia yako maisha yao yote hata kipindi ambacho huna uwezo wa kufanya kazi au haupo kabisa
10. Hatua ndogo unazochukua na kuzifanya kwa muda kwa msimamo bila kusitisha au kuruka huleta mabadiliko kwa kiasi kikubwa
11. Machaguo nadhifu madogo + Msimamo + Muda = Tofauti kwa kiasi kikubwa
12. Siri ya mafanikio ambayo wazazi wetu wametumia katika maisha yao ni jitihada, bidii, nidhamu na tabia njema
13. Unashindwa pale unapoanza kuacha kufanya vile ambavyo vilikufanya ufanikiwe
14. Maisha yetu huishia kuwa ni matokeo ya machaguo tunayofanya
15. Ukiamua kukaa na kutokufanya uchaguzi maanake umeamua kupokea machaguo yoyote yanayokuja kwako
16. Bila kujali maamuzi unayofanya ni madogo kiasi gani, pale yanapofanywa kwa kulimbikizwa kwa muda mrefu huleta athari/faida
Soma Makala Hii Inayohusiana : Uchambuzi wa Kitabu " TOUGH TIMES NEVER LAST BUT TOUGH PEOPLE DO"
17. Unapofanya uchaguzi hakikisha unafikiria kwanza
18. Pale unapoamua kuwajibika 100% kitu kifanikiwe ndipo utapata mafanikio katika kitu hicho
19. Unawajibika kwa kila unachokifanya, usichokifanya na vile ambavyo utaitikia vile ulivyofanyiwa
20. Fursa inapokutana na maandalizi mazuri hutengeneza bahati
21. Kanuni ya bahati
Maandalizi + Mtazamo + Fursa + Matendo = Bahati
22. Hatua ya kwanza kuelekea mabadiliko ni kufahamu/kutambua (awareness)
23. Huwezi kuboresha kitu bila kukifatilia na kukipima
24. Kitu chochote hakiwezi kuwa tabia mpaka ukifanyie kazi kwa wiki 3
25. Fanya machaguo sahihi kila siku kila wiki na mapema utaanza kuona utoshelevu kifedha katika maisha yako
26. Kila siku fanya uchaguzi wa kusonga mbele
27. Marekebisho kidogo katika mambo yale yale ya kila siku hubadilisha kwa kasi matokeo katika maisha yako
28. Fanya kitu cha tofauti ili upate matokeo tofauti na bora zaidi
29. Watu waliofanikiwa wanajua malengo yao kwa ufasaha ,wanajua wao ni nani na wanataka kuwa nani
30. Watu wasiofanikiwa wanajua malengo yao katika vichwa vyao hawayaandiki sehemu ambayo watajikumbusha mara kwa mara
31. Unatakiwa kuwa na malengo katika kila sehemu ya maisha yako
sio malengo ya upande mmoja mfano fedha peke yake
32. Unatakiwa uwe na ulinganifu katika kila eneo la maisha yako: biashara, fedha, afya, kiroho, kifamilia na mahusiano
33. Mafanikio ni kitu ambacho unakivuta kwa kuwa mtu anayevutia
Rafiki unaweza kuwashirikisha wengine kuhusu blogu hii kwa ajili ya kupata maarifa mbalimbali na pia unaweza kubofya hapa ili kuweza kupata makala kila inapowekwa kupitia barua pepe yako.
Goodluck Moshi
Author
StadizaMafanikio
Read, Apply and Share!
0 comments:
Post a Comment