Monday, 5 December 2016

Jinsi ya Kuinstall Kapersky KIS 2017 Katika Microsoft Windows 7

Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio!

Ili kulinda programu na data zilizopo katika kompyuta muhimu kuweka programu ambazo zitazuia programu hatarishi kuathiri ufanyaji kazi wa kompyuta. Programu hatarishi hufahamika kwa jina la virusi (virus).
Na programu ambayo inazuia kompyuta kuathiriwa na virusi huitwa antivirus.

Kuna watengenezaji wengi ambao wanaandaa na kuuza hizi programu za antivirus. Baadhi ya antivirus ni Kapersky, McAfee, Avira, Escan, AVG na kadhalika.

Soma Makala Hii Inayohusiana Jinsi ya Kutatua Tatizo la Barua Pepe Kutoingia Katika Inbox

Katika makala hii napenda kukushirikisha namna ya kutatua changamoto ambayo unaweza kukutana nayo wakati unainstall Kapersky Internet Security 2017 (KIS 2017).

Changamoto moja kubwa ambayo nimekutana nayo wakati nafanya installation ya KIS 2017 katika Operating System ya Windows 7 Professional ni kuwa programu hizi mbili kutokuendana (compatible).

KIS 2017 inahitaji Windows 7 Professional Service Pack 1 ili ikubali kuwa installed. Ikiwa una Windows 7 Professional isiyo Service Pack 1 unahitaji kupakua (download) Service Pack 1 kwa kusearch katika Google na kisha kufanya installation.

Baada ya kufanya installation ya Service Pack 1 kwa mafanikio ndipo uendelee na kuinstall KIS 2017.

Tatizo hili la kuhitaji Service Pack 1 utalipata ikiwa Windows 7 ndiyo inatumika. Lakini hautakutana na tatizo hili ikiwa unatumia Windows 8 au Windows 10.

Rafiki unaweza kuwashirikisha wengine kuhusu blogu hii kwa ajili ya kupata maarifa mbalimbali na pia unaweza kubofya hapa ili kuweza kupata makala kila inapowekwa kupitia barua pepe yako.

Goodluck Moshi
Author
StadizaMafanikio

Related Posts:

  • Uchambuzi wa Kitabu " TOUGH TIMES NEVER LAST BUT TOUGH PEOPLE DO" Robert H Schuller ni mwandishi wa kitabu cha "TOUGH TIMES NEVER LAST BUT TOUGH PEOPLE DO" . Katika kitabu hiki mwandishi anatupa mbinu za kutumia tunapokuwa tunapitia vipindi vigumu katika maisha yetu ya kila siku. Hapa nina… Read More
  • Mfumo Pekee Utakakokusaidia Kukidhi Mahitaji ya Mteja Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio! Suala la kukidhi mahitaji ya mteja unaowahudumia linakwenda sambamba na utoaji wa huduma bora kwa mteja. Kiwango cha kukidhi mahita… Read More
  • Matumizi Bora ya Siku za Wikiendi na Sikukuu Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio! Rafiki katika wiki tuna siku saba, kati ya siku hizi kuna baadhi ya watu kutegemea na ratiba ya majukumu pale anapofanya kazi anaku… Read More
  • Hatua Nne (04) Katika Uandishi wa Blogu Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio! Rafiki unapoanza kuandika makala katika blogu kuna changamoto mbalimbali ambazo utakutana nazo. Changamoto hizi zinatokana na kuwa … Read More
  • Jinsi ya Kutengeneza Bootable USB Drive Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio! Flash ni kifaa ambacho hutumika kwa ajili ya kuhifadhi data kutoka katika kompyuta. Flash inaweza kuchomekwa na kutolewa katika kom… Read More

0 comments:

Post a Comment