Friday, 25 November 2016

Njia Bora Ya Kukabili Changamoto Yoyote

Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio!

Rafiki maisha tunayoishi yana changamoto za aina mbalimbali. Changamoto hizi ni njia pekee ambayo kama utaiitumia vizuri itakusaidia kukusogeza hatua ya ziada.

Katika makala ya leo napenda kukushirikisha namna bora ambayo itakusaidia namna ya kukabili au kuzitatua changamoto.

Jambo la kwanza rafiki usifanye kosa la kuhangaika na dalili za tatizo. Hakikisha unafahamu kile kilicho nyuma ya dalili ambazo unaziona, yaani sababu zilizopelekea changamoto kutokea.

Jambo la pili ni kuwa na kipaumbele wakati unatatua matatizo. Changamoto haziji katika mpangilio bali huja nyingi kwa wakati mmoja. Siri ya pekee itakayokusaidia ni kuwa na mpangilio unaokuelekeza kutatua changamoto moja baada ya nyingine hatua kwa hatua.

Jambo la tatu hakikisha unakuwa na ufasaha kuhusu changamoto unayoipitia. Njia ya pekee ya kukusaidia kupata ufasaha ni kujiuliza changamoto ni nini hasa , hii inakusaidia kufocus.

Jambo la nne hakikisha unatafuta watu ambao watakusaidia wakati unapitia hatua ya kutatua changamoto. Hawa watakusaidia kutambua au kuona mambo ambayo huwezi kuyaona kama ungekuwa peke yako.

Soma Makala Hii Inayohusiana : Uchambuzi wa Kitabu " TOUGH TIMES NEVER LAST BUT TOUGH PEOPLE DO"

Jambo la tano hakikisha unakusanya mambo yote ambayo yaliyosababisha changamoto unayoipitia.

Jambo la sita rafiki hakikisha unaorodhesha njia zote ambazo zinaweza kukusaidia kutatua tatizo husika. Kisha chagua njia ambayo ni bora kuliko njia zote ambazo umeziorodhesha

Jambo la saba hakikisha unafanyia kazi njia uliyoichagua na kisha unaifanyia tathmini ili iweze kukusaidia kujua kama umetatua changamoto unayoipitia au la.

Rafiki unaweza kuwashirikisha wengine kuhusu blogu hii kwa ajili ya kupata maarifa mbalimbali na pia unaweza kubofya hapa ili kuweza kupata makala kila inapowekwa kupitia barua pepe yako.

Goodluck Moshi
Author
StadizaMafanikio

Read, Apply and Share!

Related Posts:

  • Kwa Nini Unahitaji Kujifunza Jambo Jipya Kila Siku?Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio! Rafiki mabadiliko na ukuaji ni vitu viwili muhimu vyenye mchango mkubwa katika maisha tunayoishi kila siku. Maisha yanakua na ladha a… Read More
  • Njia Bora Ya Kukabili Changamoto YoyoteHabari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio! Rafiki maisha tunayoishi yana changamoto za aina mbalimbali. Changamoto hizi ni njia pekee ambayo kama utaiitumia vizuri itakusaidia … Read More
  • Jinsi Ya Kutambua Uwezo wa Kompyuta YakoHabari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio! Rafiki kompyuta ni kifaa ambacho kinachukua nafasi kubwa katika matumizi ya kazi mbalimbali katika zama hizi za habari. Kompyuta zina… Read More
  • Namna Ya Kudelete File Katika KompyutaHabari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio! Rafiki moja ya operation ambayo inafanyika mara kwa mara katika matumizi ya kompyuta ni delete. Delete hufanya kazi ya kufuta file li… Read More
  • Uchambuzi Kitabu cha " THE COMPOUND EFFECT"Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio! Darren Hardy ni mwandishi wa kitabu cha THE COMPOUND EFFECT. Katika kitabu hiki mwandishi anatueleza siri kubwa iliyopo katika kufany… Read More

0 comments:

Post a Comment