Sunday, 25 September 2016

Uchambuzi wa Kitabu cha ONE MINUTE MANAGER

Habari rafiki yangu ambaye unaendelea kufuatilia makala katika blogu hii, wiki hii nilifanikiwa kusoma kitabu kinachoitwa One Minute Manager, hapa chini nimekushirikisha mambo ambayo nilijifunza na kuyanote ili kuweza kutusaidia kupata maarifa ambayo yatatusaidia katika maisha yetu ya kila siku. Karibu tujifunze



Utangulizi
Mambo ambayo tunajishughulisha nayo katika ratiba zetu za kila siku ikiwa kama ni ya kazi au hata biashara kwa namna moja au nyingine inahusisha kushirikiana na watu wenye weledi au ujuzi mbalimbali ili kutekeleza.

Kitabu hichi kinaelezea kwanza juu ya thamani ya hawa watu ambao ni rasilimali muhimu katika muhimili wako wa kuweza kukufanikisha kwa shughuli unayofanya, lakini pia waandishi wanajikita zaidi katika kujenga mazingira bora ya mahusiano kati yao na wewe kiongozi kuweza kusaidia kufanikisha malengo yenu.


Mambo  sita niliyojifunza:
1. Ukichunguza mameneja wengi utakuta ama wamejikita zaidi katika kusimamia watendaji wao wa chini kwa kuwatawala au kusimamia katika kuhakikisha matokeo yanapatikana, lakini sifa za meneja mzuri ni yule ambaye anaweza kujisimamia kwanza yeye binafsi, pili anawasimamia wale anaowaongoza na tatu ni yule ambaye anasimamia upatikanaji wa matokeo katika yale yanayotekelezwa. Huitwa mameneja wenye ufanisi


2. Ni muhimu kuzingatia kwa watu ambao unawategemea wafanye uzalishaji katika shughuli yako waweze kuwa vizuri na hali ya kuridhika na unavyofanya nao, kuridhika kwao na matokeo unayoyapata ni vitu vinavyohitaji kwenda sambamba.


3. Uzalishaji wowote usipimwe kwa kigezo cha idadi tu bali kigezo cha ubora pia, katika uzalishaji ubora na idadi ni mambo ambayo yanahitaji kwenda sambamba


4. Ili kuweza kuwasaidia watu unaowaongoza kuwa na utaratibu wa kufanya vikao ambavyo utaweza kuwasikiliza kuhusu mambo ambayo wamefanikiwa kuyakamilisha na yale ambayo bado wanaendelea kuyafanyia kazi kuyakamilisha, na kikubwa unahitaji kuwapatia nafasi ya wao kufanya maamuzi na siyo kila maamuzi uyafanye wewe tuu


5. Meneja mzuri ni yule ambaye anakupa majukumu yako na nini kinachotarajiwa kutoka kwako kabla hujaanza kazi husika, na mnakuwa mmekubaliana vigezo vya utendaji kazi ambavyo unaweza kujipima kati ya kile unachokifanya na unachotarajia kutoa matokeo


6. Kazi inapofanyika vizuri watu wanatakiwa kupongezwa au kusifiwa kwa kile ambacho wamekifanya na upongezaji ni muhimu uwe unaamuliwa na takwimu za kile anachozalisha


Tuendelee kuyaweka katika matendo ili tuweze kuyabadilisha maisha yetu

Related Posts:

  • Usipobadilika, utamezwa na mabadilikoYanapotokea mabadiliko jifunze kukabiliana nayo (kuadapt) kwa haraka vinginevyo utakavochelewa zaidi kwa kutafakari nini cha kufanya na kulialia na hali halisi utatumia gharama kubwa kuyapokea na muda utakuwa umekwenda pia. … Read More
  • Njia Rahisi Kuzuia Utendaji MbovuKama hali yetu ya hamasa ya kufanya jambo fulani haifanani/haiendani na jambo tunalohitajika kulifanya, moja kwa moja inapelekea kukosa hamasa ya kulitekeleza hilo jambo. Kukosekana kwa hamasa kutapelekea kulihairisha hilo j… Read More
  • Uwekaji Mipango UsioaminikaNi asili yetu kuwa na matumaini mema juu ya jambo fulani ambayo yamepitiliza uhalisia. Mfano tunadhani kuwa tutafanya mambo mengi kwa muda mchache kuliko inavyotakiwa kiuhalisia au kudhani jambo unalolifanya litachukua muda m… Read More
  • Maliza Robo ya Kwanza 2015 Hivi Hatua 3 muhimu unazohitaji kuzichukua ili kuweza kutumia muda wako kwa ufanisi na kupata matokeo ya ndoto yako kwa haraka: 1. Have a Plan Kuwa na mpango wa kina unaoanisha nini unachotaka kufanya na mpango huu ni lazima uw… Read More
  • Umakini Unaouhitaji Kabla Hujaanza Kufanya LoloteKutegemeana mtu na mtu kuna tofauti kati ya vitu vinavyoleta bugudha wakati unafanya jambo. Mfano kuna mtu hawezi kufanya kazi katika mazingira yenye kelele au wakati redio inazungumza wakati huo huo kuna mwingine anaweza kuf… Read More

0 comments:

Post a Comment