Habari na karibu ndugu
mpenzi msomaji wa blogu hii. Ni matumaini yetu umekuwa na
wiki ya mafanikio sana.
Leo tutaangalia sifa
unazotakiwa kuzitambua kwa mtu unayetaka awe kiongozi au unamtegemea awaongoze.
- Tabia
Mtu
mwenye tabia nzuri au njema anakuwa na uaminifu, utiifu, nidhamu, kutegemewa,
uvumilivu, kujitambua na pia anakuwa na bidii katika kazi.Wakati kwa upande
mwingine mtu asiye na tabia njema au nzuri anakuwa hana uwezo wa kuwajibika kwa
matendo yake, hawezi kukamilisha kazi kwa wakati, na pia hatimizi ahadi au
majukumu yake.
- Kuhamasisha
Mtu
ambaye anajua wapi anaelekea anakuwa na uwezo wa kuhamsisha wengine wafuatane
nae kutokana na ahadi au mambo mazuri yanayopatikana kule anakoelekea. Kwa hiyo
unahitaji kuangalia mtu Yule ambaye anafuatawa na watu wazuri na sio wale walio
wa kawaida kabisa pia angalia huyu mtu anamtazama nani kama mtu anayemhamasisha
bila shaka kwa Yule anayefaaa kuwa kiongozi utamkuta anamfatilia mtu ambae pia
ni kiongozi na ana sifa njema
- Mtazamo chanya
Tafuta
mtu Yule ambaye hana vizuizi katika akili yake kwa kuona jambo Fulani
haliwezekani bali awe ni Yule mwenye nia ya kujaribu pamoja na kuwaza chanya
kuwa atafanikiwa katika lile atendalo na anakuwa hazuiwi na vikwazo binafsi.
- Ufanisi mzuri
katika kuwasiliana
Viongozi
wazuri ni wale ambao wanaweza kuwasiliana vema, wanakuwa wanajihusisha vema na
wale wanaoongea nao kwa kuweza kumtazama ana kwa ana pamoja na kuwa na tabasamu
kwa Yule anayeongea naye. Kiongozi mzuri si Yule anayeweza kuwasilisha ujumbe
wake lakini pia anakuwa na uwezo mzuri wa kusikiliza pia wale anaowaongoza.
- Kujiamini
Bila
kujali hali gani katika wakati husika kiongozi pamoja na kundi wanapitia ,
kiongozi mzuri ni Yule anayekuwa anayejiamini na kuwa na ujasiri kuwa yeye
pamoja na timu anayoiongoza wanaweza kusogea hatua kutoka walipofika
- Nidhamu
Kiongozi
ni Yule mwenye nidhamu anayeweza kutawala hisia zake na pia ana uwezo wa
kusimamia au kutawala muda wake jinsi ya kuutumia ili kumsaidia kupata
mafanikio kwa ajili yake na timu anayoiongoza
- Rekodi nzuri ya
mafanikio
Ni
vizuri ukacheki historia yake ya nyuma ya utendaji wa mtu. Na kiongozi mzuri
utakuta ana rekodi nzuri ya utendaji