Thursday, 2 July 2015

Sifa Unazotakiwa Kuzitambua Kwa Kiongozi Anayeweza Kuleta Mabadiliko

Habari na karibu ndugu mpenzi msomaji wa blogu hii. Ni matumaini yetu umekuwa na wiki ya mafanikio sana.
Leo tutaangalia sifa unazotakiwa kuzitambua kwa mtu unayetaka awe kiongozi au unamtegemea awaongoze.

  1. Tabia
Mtu mwenye tabia nzuri au njema anakuwa na uaminifu, utiifu, nidhamu, kutegemewa, uvumilivu, kujitambua na pia anakuwa na bidii katika kazi.Wakati kwa upande mwingine mtu asiye na tabia njema au nzuri anakuwa hana uwezo wa kuwajibika kwa matendo yake, hawezi kukamilisha kazi kwa wakati, na pia hatimizi ahadi au majukumu yake.

  1. Kuhamasisha
Mtu ambaye anajua wapi anaelekea anakuwa na uwezo wa kuhamsisha wengine wafuatane nae kutokana na ahadi au mambo mazuri yanayopatikana kule anakoelekea. Kwa hiyo unahitaji kuangalia mtu Yule ambaye anafuatawa na watu wazuri na sio wale walio wa kawaida kabisa pia angalia huyu mtu anamtazama nani kama mtu anayemhamasisha bila shaka kwa Yule anayefaaa kuwa kiongozi utamkuta anamfatilia mtu ambae pia ni kiongozi na ana sifa njema

  1. Mtazamo chanya
Tafuta mtu Yule ambaye hana vizuizi katika akili yake kwa kuona jambo Fulani haliwezekani bali awe ni Yule mwenye nia ya kujaribu pamoja na kuwaza chanya kuwa atafanikiwa katika lile atendalo na anakuwa hazuiwi na vikwazo binafsi.

  1. Ufanisi mzuri katika kuwasiliana
Viongozi wazuri ni wale ambao wanaweza kuwasiliana vema, wanakuwa wanajihusisha vema na wale wanaoongea nao kwa kuweza kumtazama ana kwa ana pamoja na kuwa na tabasamu kwa Yule anayeongea naye. Kiongozi mzuri si Yule anayeweza kuwasilisha ujumbe wake lakini pia anakuwa na uwezo mzuri wa kusikiliza pia wale anaowaongoza.

  1. Kujiamini
Bila kujali hali gani katika wakati husika kiongozi pamoja na kundi wanapitia , kiongozi mzuri ni Yule anayekuwa anayejiamini na kuwa na ujasiri kuwa yeye pamoja na timu anayoiongoza wanaweza kusogea hatua kutoka walipofika

  1. Nidhamu
Kiongozi ni Yule mwenye nidhamu anayeweza kutawala hisia zake na pia ana uwezo wa kusimamia au kutawala muda wake jinsi ya kuutumia ili kumsaidia kupata mafanikio kwa ajili yake na timu anayoiongoza

  1. Rekodi nzuri ya mafanikio

Ni vizuri ukacheki historia yake ya nyuma ya utendaji wa mtu. Na kiongozi mzuri utakuta ana rekodi nzuri ya utendaji 

Related Posts:

  • Utaratibu Sahihi wa Uandishi wa Saa Habari rafiki! Kumekuwa na changamoto katika kujua namna sahihi ya uandishi wa muda kutoka katika saa.Saa ni kifaa ambacho kinatumika kusoma muda ambao huwa katika mpangilio wa kuanza na saa, kisha kufuata dakika na kuishia… Read More
  • Uchambuzi wa Kitabu cha ONE MINUTE MANAGER Habari rafiki yangu ambaye unaendelea kufuatilia makala katika blogu hii, wiki hii nilifanikiwa kusoma kitabu kinachoitwa One Minute Manager, hapa chini nimekushirikisha mambo ambayo nilijifunza na kuyanote ili kuweza kutusa… Read More
  • Uandishi Sahihi wa Siku na Mwezi Katika Mwaka Habari rafiki mfuatiliaji wa makala mbalimbali katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio! Muda unaweza kuoneshwa kwa vipimo mbalimbali. Kipimo kidogo  cha muda ni sekunde. Sekunde zikikusanyika na kufika idadi ya siti… Read More
  • Jinsi ya Kutumia Kompyuta Yako Kuwa Chanzo cha Intaneti Habari rafiki! Katika makala ya leo ninapenda kukushirikisha namna ya "kushare" intaneti kutoka kwenye kompyuta na kwenda kwenye vifaa vingine vyenye uwezo wa kupokea intaneti. Kompyuta yoyote ambayo ina kifaa kinachoitwa "… Read More
  • Maana za Vibao Vya Namba Za Magari (Plate Number) Habari rafiki! Katika kila gari kuna sehemu mbili ambapo huwekwa vibao vyenye namba kwa ajili ya kulitambulisha gari husika. Vibao hivi huwekwa mbele na nyuma ya gari. Katika lugha ya kiingereza huitwa "plate number". Katik… Read More

0 comments:

Post a Comment