Saturday 16 April 2016

Mambo 17 niliyojifunza katika kitabu cha SPEED WEALTH


Mambo niliyojifunza kutoka katika kitabu cha SPEED WEALTH kilichoandikwa na T Harv Eker




1. Ili uweze kufanikiwa na kuchomoza katika mafanikio unahitaji kumiliki biashara, ukitumia njia ya ajira ya kuwa umesoma ,umepata kazi nzuri, na ufanye kazi kwa jitihada haisaiidii sana wewe kuwa huru kifedha kwa kuwa mfumo huu haufanyi kazi katika mazingira ya sasa

2. Unaweza kuwa unahifadhi fedha ili ziweze kupitia katika riba na ziweze kukua, kiwango cha riba katika mazingira ya sasa pia ni kidogo hivo utakuta unachukua muda mwingi pia kufikia uhuru wa kifedha

3. Ukiona mtu anafanikiwa zaidi yako unahitaji kufahamu kuwa kuna  maarifa ya ziada anayo ambayo wewe bado hujaweza kuwa nayo au huyafahamu, hivyo unahitaji kufanya maamuzi ya kukusudia kuwekeza muda zaidi kujifunza

4. Siri kubwa ya wengi waliofanikiwa ni kujifunza kuwa na kipato kikubwa na matumizi madogo, biashara zote zilizochomoza wamejizatiti zaidi katika kutengeneza mapato zaidi kwa kutumia matumizi kidogo

5. Kutokana na mabadiliko yanayotokea kwa kasi katika kila nyanja kuanzia teknolojia na maeneo mengine ,pia kasi ya kupata uhuru wa kifedha nayo inaongezeka, ili kuweza kuendana na haya mabadiliko kwa kasi unahitaji pia kubadilika na kuyapokea mabadiliko kwa kasi pia ili kuichangamkia fursa kwa kasi

6. Mafanikio ni kitu ambacho unaweza kujifunza kabisa, na siri ni kuwa ukitaka kuwa mtaalamu katika kada husika ni lazima ujifunze na pia uweke katika matendo yale uliyojifunza

7.  Unahitaji kuwa na nia ya kujifunza na shauku ya kufanikiwa kwa haraka ili uweze kujenga kujitoa, kuwa na msimamo na kuweka jitihada katika kile unachotaka kufanya

8. Malipo unayoyapata inategemea na kiwango cha thamani unachokipeleka katika soko , ikiwa kiwango cha thamani ni kidogo na pia hakipo katika ujazo wa kujitosheleza au kumridhisha basi malipo nayo sambamba huwa kidogo.

9. Nguzo kuu nne zinazojenga thamani inayotolewa na bidhaa au huduma:
a) Hitaji : Kiwango ch a uhitaji wa thamani inayobebwa na bidhaa yako katika soko inaamua fedha utakayokuwa unalipwa

b) Upatikanaji : Thamani ya kitu huongezeka kutokana na Upatikanaji kuwa adimu katika soko. Unahitaji kutoa thamani ambayo wengine hawatoi au hawana au kufanya vitu tofauti na wengine wanavyofanya

c) Ubora: kiwango cha ubora katika thamani iliyopo katika bidhaa huamua kiwango cha malipo unayoweza kupata. Ni vema ukawa na msimamo kuwa unafanya kwa ubora au haufanyi kabisa

d) Kiasi (Uwingi): idadi ya bidhaa ulizonazo unazoweza kuziweka katika soko inaamua kiwango cha utajiri unaoweza kuipata

10. Ni vizuri kujua muda gani wa kuingia na kutoka sokoni, muda mzuri ni ule hitaji ni kubwa kuliko Upatikanaji, na kuna njia nyingi ni kushirikiana na mtu anayetoa huduma ambayo huwezi kutoa, au kukopi huduma fulani kutoka eneo lingine na kuleta katika eneo husika

11. Unahitaji kuwa na mfumo ambao unaweka shughuli zako katika utaratibu unaokusudia, hii itakusaidia sana kuongeza rasilimali ya muda n.k. Kuwepo kwa mfumo kunasaidia biashara kufanya kwa ufanisi bila wewe mhusika kuwepo eneo la biashara. Na mambo yanayohitajika kuwekewa mfumo ni masoko, uzalishaji na uendeshaji

12. Ni muhimu kujua namna ambavyo unaweza kutengeza kipato zaidi huku ukiwa wewe umelala au ukiwa umetumia fedha, muda na rasilimali kidogo

13. Maisha ni mafupi kitu chochote unachotaka kukifanya kifanye leo na vile unataka kuwa kuwa leo usingoje wakati mwingine

14. Ukihitaji kufanikiwa unatakiwa uweke jitihada katika kujifunza kujiendeleza binafsi na kuzisoma biashara

15. Kila unayemwona leo ni bora sana aliwahi kuwa wa kawaida sana wakati anaanza

16. Biashara ni ujuzi ambao unaweza kujifunza

17. Hakikisha kama unajifunza , basi unajifunza vile vitu ambavyo vinaleta tofauti na vina tija.

Wednesday 13 April 2016

Mbinu pekee inayoweza kukusogeza hatua moja mbele

Business is a learnable skill.
No one comes out of the womb a business expert. Everyone has to learn how to do it. Which means everyone who is great at something now was terrible when they started.

But if you are going to learn things, you have to make sure you are learning right things, the things that makes the difference

~ T Harv Eker

Biashara ni ujuzi ambao unaweza kujifunza. Hakuna ambaye amezaliwa na akawa ni mtaalamu uliyobobea katika biashara , kila mmoja alijifunza namna ya kufanya na hii ina maana kila ambaye anaweza kufanya kitu fulani vizuri basi alishawahi kuwa ovyo wakati anaanza. Na pia hakuna kitu kinakuwa rahisi kabla hakijawa kigumu

Jambo la kuzingatia ni kuwa unapoamua kujifunza basi ujifunze yale mambo ambayo yana maana na yanaleta tofauti chanya katika maisha yako

Tuesday 12 April 2016

Siri Kubwa ya Biashara ni Kuzalisha Thamani Toshelevu

DELIVER MASSIVE VALUE

Money is a convenient symbol that represents and measures the value of goods and services exchanged between people.

The keyword here is VALUE. It's value that determines your income.

The Law of Income states that , you will be paid in direct proportion to the value you deliver according to the market place.

The reason most people are broke is that they don't deliver a lot of VALUE in the eyes of current market place.
The important element here is DELIVER.

Many people have good ideas, good intentions, even produce good products and services, but either their values is not considered very valuable in the today's market place, or they just don't deliver enough of it. It's simple if you don't deliver a lot, you don't get paid a lot

~ T Harv Eker

Fedha ni alama inayotumika kuwasilisha na kupima thamani ya bidhaa na huduma ambazo watu hubadilishana.
Unalipwa kutokana na kiwango cha thamani thamani ambayo unayoleta katika soko husika.
Unaweza ukawa na mawazo mazuri, nia nzuri hata bidhaa au huduma nzuri pia lakini kiwango cha utoshelevu wa thamani unayoleta katika soko ndicho kinaamua malipo utakayoyapata.
Mambo makubwa mawili ndiyo husababisha kutofanikiwa katika biashara ni aidha thamani ya hicho unachotoa au kiwango cha thamani si toshelevu

Monday 11 April 2016

Kuwa Bango la Matumaini

Be a Billboard for Hope
To live victoriously in our everyday lives, one thing we definitely need is hope. Hope is the happy and confident anticipation of good. It is the belief that something good is about to happen at any moment! And it’s a great place to hang out in your everyday life! Resist the temptation to look at what you have lost or don’t have and choose to look at all that God has done, is doing, and will do. When you do, hope will come alive, joy will increase, faith will grow, and activity will increase. - Joyce Meyer

Katika maisha yetu ya kila siku kitu kimoja cha pekee kikubwa tunachokihitaji ni tumaini. Tumaini ni kitendo cha imani kinachoambatana na furaha pamoja na ujasiri wa kuwa mambo mema yatatokea kwako wakati wowote.
Mara nyingi tumaini hupotezwa kwa kuangalia ni vitu gani tumepoteza au hatuna badala ya kutathmini mambo ambayo Mungu ameyafanya , anayafanya na ataendelea kuyafanya kwa ajili ya maisha yetu ya kila siku.
Tumaini huwa hai, furaha huongezeka , imani hukua na hamasa ya utendaji huongezeka ikiwa tutashinda jaribu la kutazama yale tuliyopoteza au ambayo hatuna

Tuesday 5 April 2016

Mambo 13 ya kuzingatia katika kuelekea mafanikio




1. Watu wengi wanofanikiwa sio kwamba wana ujuzi au uwezo kuzidi ambao unao bali ni kiwango cha maarifa walochonacho ndicho kinatofautisha. Ni muhimu kuwa na hamu na kiu kubwa ya kupata maarifa yanayohusu eneo unalotaka kuwa bora zaidi

2. Ukiwa kiongozi unapoletewa tatizo na mteja usipende sana kujua historia ambayo haitakusaidia katika utatuzi wa tatizo ,  jitahidi kulichambua tatizo kwa lengo la kukusaidia kupata maarifa zaidi ya jinsi ya kulitatua, halafu uwajibike kulibeba tatizo na kisha ufanye maamuzi sahihi kwa kupata ufumbuzi wa tatizo husika

3. Mara nyingi huwa tunavutiwa sana na hatua fulani mtu mwingine anayofikia ya mafanikio, kikubwa ni kufahamu matokeo ya kiwango cha juu wanayoyafikia kunakuwa kuna gharama wanayolipia ya kuwa na nidhamu, kujitoa hasa kutimiza ilo jambo na Kujituma kwa jali ya juu

4. Mara nyingi huwa tunapenda kuona mtu fulani ni mbaya kutokana labda ameshindwa kutekeleza jambo fulani, ni vema ukiwa kiongozi kuyatazama mambo katika jicho la kuelewa nini kinaendelea na pia kupenda kuweka mkazo kutazama upande wa uzuri wa mtu

5. Kunahitajika kuwa na mkazo katika yale mambo ambayo ni muhimu na yanafaida kwako, na kuyaondoa yale ambayo hayana faida au hayaongezi thamani kwako, ni vizuri kila siku unaandika mambo yale ambayo yana umuhimu , na ambayo unahitaji kuyafanyia kazi kuelekea ndoto yako, na pia ni vema ukaweka jitihada kufanya yaliyobora kwa maisha yako ili uvune yaliyobora pia, na ni muhimu kufurahia pia maisha kadiri unavyoelekea kutimiza ndoto yako

6. Vile unavyofikiri ndivyo unavyokuwa , mara nyingi watu hutazama jambo katika lenzi ya kutowezekana, uwoga, vikwazo na mambo ya kufikiria kutokana na vile anavyoamini au unafahamu, ni vizuri ukajiwekea viwango ambavyo unaviamini na unaweza kuvunja rekodi kwa kuvitimiza, siku zote tazama mambo katika lenzi ya kuwekezekana bila kujali nani alifanya nini

7. Watu wa familia yako ndio ambao watakuwa na wewe muda wote katika hali yoyote hawawezi kuacha peke yako , ni vizuri hata katika shida na mafanikio yako ukaambatana nao, ni vema kujizoesha kuwapigia simu wazazi wako, kumbusu mwenza wako na kuwakumbatia watoto wako hii huongeza upendo na ukaribu

8. Mambo mengi ambayo tunayafanya hutanguliwa kwanza na fikra ambayo tunawaza juu ya jambo husika hivyo ni muhimu sana kuwaza chanya na kuwezekana kwa jambo ili kusaidia kukupa msukumo na nguvu ya kulifanya liweze kutokea

9. Njia nzuri ya kupata kile unachokitaka ni kwa kuomba, na siku zote watu wapo tayari kukupatia kike kitu ambacho tu kitaleta maana kwako au kinaongeza thamani kwako na kuweza kuwasaidia watu wengine

10. Inashauriwa kuamka mapema na kufanya mazoezi kutokana unakuwa upo na nguvu na hamasa ya kufanya jambo , akili inakuwa na uwezo mkubwa kutokana na mifumo kufanya kazi ipasavyo, na unakuwa na muda wa kutosha kutekeleza ndoto yako

11. Vipindi vya maisha ambavyo vina changamoto au vigumu ndivyo vipindi ambavyo ni vizuri kwa sababu hutusaidia kujua ujasiri wetu, kujifahamu zaidi na kuwa na shauku zaidi ya kufanikiwa katika jambo husika

12. Unapoanguka hakikisha unaamka tena unapukuta vumbi unaendelea kusonga mbele usikubali kubaki pale ulipo kuwa bora zaidi ya kabla hujaanguka

13. Unahitaji kutoulisha udhaifu wako , tunaweza kuwa bora sana kwa kufanya yale mambo yanayotufanya tuwe bora sana , tunakuwa waoga kwa kuendelea kuyatazama yale mambo yanayotuogopesha


Hayo ni baadhi kati ya mengi yaliyo katika kitabu cha Stunning Success kilichoandikwa na mwandishi Robin Sharma

Mambo 10 yatakayokusaidia kuboresha Mawasiliano yako

Utangulizi:
Kuna wakati mada ambayo unahitaji kuzungumza na hadhira hupelekea kuleta ugumu katika uwasilishaji kwa kujadiliana. Na hii hupelekea kuleta hata hofu kuona kama mahusiano yako na hadhira unayowasilisha majadiliano kuweza kubadilika. Changamoto hii huonekana hasa katika mada ambazo labda hazijazoeleka katika tamaduni za jamii husika au kuona zinagusa hisia moja kwa moja ya hadhira au kuona kama utaonekana ni mtu asiyejali. Majadiliano yenye ugumu namna hii huenda yakatokea katika mazungumzo yanayohusu binafsi, biashara , dini, siasa n.k.
Waandishi wa kitabu hiki wameweka mbinu ambazo zitasaidia kuweza kuwasilisha ujumbe hata kama unaonekana mgumu lakini pia kuendelea kulinda na kuyaboresha mahusiano ya pande zote mbili na kuacha pande zote zikiwa na furaha.

Mambo ya kujifunza na kuyafanyia kazi:
1. Kunapokuwa kuna mazungumzo ambayo yana ugumu ndani yake mara nyingi kunakuwa na mambo ambayo yanafikiriwa na mambo ambayo hayasemwi pia, na hofu ya kusema inatokea kutokana na kuona kuwa utaharibu mazungumzo zaidi, kunakuwa hakuna kuridhika na maamuzi yanayotokana na mazungumzo ya namna hii, maamuzi mengi yanayotokana na mazungumzo haya hufanywa kwa kuwa kiongozi tuu amesema

2. Kuna aina tatu za mazungumzo yenye ugumu:

a) Kitendo: mazungumzo ya namna huleta fikra ya kujiuliza ni nini kimetokea, jambo gani halikufanywa ipasavyo
b) Hisia: mazungumzo haya huhusisha namna mtu atakavyojisikia mfano kudharauliwa, kuumizwa na kadhalika
c) Utambulisho: mazungumzo haya huhusisha haiba ya mtu, yaani mtu amekuonaje kwa nafasi yako

3. Mara nyingi kunakuwa na kulaumu kwa nini upande wa pili umefanya vile umefanya katika shughuli mliyokubaliana na kupelekea kulaumu badala ya kutaka kuelewa kuwa kila mmoja ana mtazamo wake, matatizo yake na hivyo mnahitaji kuheshimu kila wazo la mmoja linapowekwa mezani na linatakiwa lipewe nafasi

4. Kunahitajika kuelewa (dhamira) dhumuni lililonyuma ya kile kilichotekelzwa na sio kuyatazama mambo kibinafsi na kuona kama umedharauliwa na kutoheshimika kwa mawazo au maelekezo yako umeyatoa

5. Ni vizuri pia kuheshimu hisia kutokana na yale yalikubalika kufanyiwa kazi, usifanye kitu kikamuumiza mtu na kuona amegandamizwa badala ya kuona amepewa nafasi ya kutenda ka uhuru na kufanya afurahie yale anayoyafanya

6. Kunapokuwa kuna mazungumzo ambayo ni magumu ni muhimu kuelewa mtazamo wa kila pande na kuona inaleta maana ipi katika lile suala mnalojadili ili kuweza kufikia muafaka , kwa hiyo ni muhimu kila mmoja apewe hiyo nafasi na sio kujibizana tuu maana hii ndo hatua muhimu ya kwanza kuelekea mabadiliko au kukubali mtazamo wa pande ya upinzani

7. Kila mtu anakuwa ana uchaguzi wa taarifa anazozingiza katika akili yake kutegemeana na mvuto alionao na hizo taarifa, kuna uwezekano wote mnaongea mada inayofanana ila kwa jinsi kila mmoja anavovutiwa na kipengele husika utakuta atatoa mchango wa mawazo kutegemeana na maslahi aliyonayo katika eneo hilo

8. Wakati mnapokuwa na mazungumzo magumu ni vizuri kama ukiwa unakataa mawazo ya mtu ukayakataa kwa uwazi, na pia lengo si kuonesha nani ameshinda bali ni kuonesha namna gani kila pande imeeeleweka na mawazo ya kila pande yamrjumuishwa pamoja

9. Kunapokuwa na mada unahitaji kuwasilisha kwa muhusika na ukiwa unafahamu kuwa wewe ndio upo sahihi na yeye hayuko sahihi, njia nzuri ni kwanza kuelewa namna anavyolielewa au kuamini kuhusu lile jambo na pia kufahamu wajibu wako wa kumsaidia ni nini katika hilo suala

10. Kosa kubwa linalofanyika katika mazungumzo huwa ni kufikiri tumepewa nia ya mtu bila kujua kuwa tunakuwa tunaelewa nia ya mtu kupitia hisia tulizonazo kutegemeana na kwamba tunaathirika kwa kiwango gani, inatakiwa hisia hizi ziwekwe pembeni

Hayo ni baadhi kati ya mengi niliyojifunza katika kitabu cha Difficult Conversation - How to Discuss what matters most