Tuesday 29 November 2016

Shule Mbili (02) Bora Unazopaswa Kuhudhuria Katika Maisha

Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio!

Rafiki suala la kujifunza ni endelevu halina ukomo. Pale unapopata ukomo wa kujifunza maana yake unajiandaa na kushindwa. Mara baada ya kumaliza elimu ya darasani kamwe usikubali kufanya hitimisho la kusoma.

Masomo mengi ambayo tunahitaji kujifunza inatakiwa kuwa na sehemu ambapo mtaala umeandaliwa utakaokuongeza hatua kwa hatua mpaka uweze kufuzu katika masomo hayo. Tofauti na elimu rasmi ya darasani ambapo unakuwa na mtaala maalum.

Huku katika maisha ya kila siku hakuna mtaala maalum bali unajifunza kutegemeana na mahitaji ya ujuzi husika. Hapa chini nakushirikisha shule mbili ambazo unaweza kuhudhuria masomo na kujifunza mambo mengi.

Soma Makala Hii Inayohusiana : Namna ya Kutambua Dalili Za Kushindwa

Shule ya kwanza unayoweza kuhudhuria ni uzoefu ulionao. Angalia historia yako mambo ambayo umekuwa ukiyafanya yamekujengea uwezo ambao una makosa uliyoyafanya unayoyaweza kuyakwepa kwa kutoyarudia lakini pia mambo uliyofanikiwa ambayo yanaweza kukusaidia kujikita zaidi na kuendelea kuyaboresha kuyatumia ili kukupatia mafanikio zaidi.

Shule ya pili unayoweza kuhudhuria ni kujifunza kwa wale walioshindwa na kufanikiwa katika lile eneo ambalo unalifanyia kazi. Angalia katika wale walioshindwa mambo yaliyowapelekea kushindwa na uyaepuke wakati huo huo ungalie pia wale waliofanikiwa uzingatie yale yaliyowasababisha wafanikiwe ili yakusaidie pia.

Rafiki unaweza kuwashirikisha wengine kuhusu blogu hii kwa ajili ya kupata maarifa mbalimbali na pia unaweza kubofya hapa ili kuweza kupata makala kila inapowekwa kupitia barua pepe yako.

Goodluck Moshi
Author
StadizaMafanikio

0 comments:

Post a Comment