Wednesday 21 December 2016

Sababu Kumi (10) Zinazokuzuia Kuanza Biashara

Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala mbalimbali zinazowekwa katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio.

Napenda kukupongeza kwa hatua uliyochukua ya kuamua kutembelea mtandao huu kwa ajili ya kuchota maarifa ambayo yatakusaidia katika maisha yako na pia kukushukuru kwa ajili ya kuwashirikisha marafiki wengine waungane nasi kwa ajili ya kuendelea kuboresha maisha yetu.

Katika makala yetu ya leo napenda kukushirikisha sababu kumi (10) ambazo zinatumika kama pazia la kujifichia au kisingizio cha kusababisha watu wasianze kutengeneza biashara zitakazohudumia watu na hatimaye kuwaingizia kipato.

1. Kukosa fedha (mtaji) kwa ajili ya kuanza biashara.

2. Kuwa na idadi kubwa ya ndugu au jamaa wanaokutegemea kwa ajili ya kuwasaidia kwa huduma mbalimbali kama mahitaji muhimu, elimu na kadhalika.

3. Kukosa mawasiliano na watu ambao wataweza kukuunga mkono katika biashara yako.

4. Kukosa uwezo wa kutosheleza wa kuanza , kuendesha na kusimamia biashara yako.

5. Kukosa muda wa kuendesha na kusimamia biashara kutokana na kutingwa na shughuli nyingine.

Soma Makala Hii Inayohusiana : Mambo Matano (05) Yanayosababisha Kushindwa

6. Kukosa mtu sahihi ambaye anaweza kukuongoza hatua kwa hatua katika biashara mpaka uweze kusimama mwenyewe.

7. Umri wako umeshakwenda sana.

8. Uhitaji wa muda mwingi kutoka kuanza biashara mpaka kukua na kuendelea.

9. Kuchukia kushughulika na wafanyakazi ambao unatakiwa kuwasimamia.

10. Hofu ya kuwa na biashara ni hatari (risky).

Rafiki hizi ni baadhi tu ya sababu zinazotumiwa, je ni sababu ipi umeitumia kujitetea kama hoja ya msingi ambayo inakuzuia mpaka sasa kuanza kutengeneza biashara?

Tafadhali nishirikishe maoni yako kwa kutaja sababu ipi ambayo unaona ndiyo kikwazo kikubwa au kunitajia sababu nyingine unazozifahamu, ili tuweze kuzijadili katika makala zijazo.

Rafiki napenda kukuarifu kuwa ikiwa una maswali au mada ambayo ungependa niiandikie makala , unaweza tuma katika anuani yangu luckmoshi@gmail.com

Goodluck Moshi
Mwandishi
StadizaMafanikio

Monday 5 December 2016

Jinsi ya Kuinstall Kapersky KIS 2017 Katika Microsoft Windows 7

Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio!

Ili kulinda programu na data zilizopo katika kompyuta muhimu kuweka programu ambazo zitazuia programu hatarishi kuathiri ufanyaji kazi wa kompyuta. Programu hatarishi hufahamika kwa jina la virusi (virus).
Na programu ambayo inazuia kompyuta kuathiriwa na virusi huitwa antivirus.

Kuna watengenezaji wengi ambao wanaandaa na kuuza hizi programu za antivirus. Baadhi ya antivirus ni Kapersky, McAfee, Avira, Escan, AVG na kadhalika.

Soma Makala Hii Inayohusiana Jinsi ya Kutatua Tatizo la Barua Pepe Kutoingia Katika Inbox

Katika makala hii napenda kukushirikisha namna ya kutatua changamoto ambayo unaweza kukutana nayo wakati unainstall Kapersky Internet Security 2017 (KIS 2017).

Changamoto moja kubwa ambayo nimekutana nayo wakati nafanya installation ya KIS 2017 katika Operating System ya Windows 7 Professional ni kuwa programu hizi mbili kutokuendana (compatible).

KIS 2017 inahitaji Windows 7 Professional Service Pack 1 ili ikubali kuwa installed. Ikiwa una Windows 7 Professional isiyo Service Pack 1 unahitaji kupakua (download) Service Pack 1 kwa kusearch katika Google na kisha kufanya installation.

Baada ya kufanya installation ya Service Pack 1 kwa mafanikio ndipo uendelee na kuinstall KIS 2017.

Tatizo hili la kuhitaji Service Pack 1 utalipata ikiwa Windows 7 ndiyo inatumika. Lakini hautakutana na tatizo hili ikiwa unatumia Windows 8 au Windows 10.

Rafiki unaweza kuwashirikisha wengine kuhusu blogu hii kwa ajili ya kupata maarifa mbalimbali na pia unaweza kubofya hapa ili kuweza kupata makala kila inapowekwa kupitia barua pepe yako.

Goodluck Moshi
Author
StadizaMafanikio

Tuesday 29 November 2016

Shule Mbili (02) Bora Unazopaswa Kuhudhuria Katika Maisha

Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio!

Rafiki suala la kujifunza ni endelevu halina ukomo. Pale unapopata ukomo wa kujifunza maana yake unajiandaa na kushindwa. Mara baada ya kumaliza elimu ya darasani kamwe usikubali kufanya hitimisho la kusoma.

Masomo mengi ambayo tunahitaji kujifunza inatakiwa kuwa na sehemu ambapo mtaala umeandaliwa utakaokuongeza hatua kwa hatua mpaka uweze kufuzu katika masomo hayo. Tofauti na elimu rasmi ya darasani ambapo unakuwa na mtaala maalum.

Huku katika maisha ya kila siku hakuna mtaala maalum bali unajifunza kutegemeana na mahitaji ya ujuzi husika. Hapa chini nakushirikisha shule mbili ambazo unaweza kuhudhuria masomo na kujifunza mambo mengi.

Soma Makala Hii Inayohusiana : Namna ya Kutambua Dalili Za Kushindwa

Shule ya kwanza unayoweza kuhudhuria ni uzoefu ulionao. Angalia historia yako mambo ambayo umekuwa ukiyafanya yamekujengea uwezo ambao una makosa uliyoyafanya unayoyaweza kuyakwepa kwa kutoyarudia lakini pia mambo uliyofanikiwa ambayo yanaweza kukusaidia kujikita zaidi na kuendelea kuyaboresha kuyatumia ili kukupatia mafanikio zaidi.

Shule ya pili unayoweza kuhudhuria ni kujifunza kwa wale walioshindwa na kufanikiwa katika lile eneo ambalo unalifanyia kazi. Angalia katika wale walioshindwa mambo yaliyowapelekea kushindwa na uyaepuke wakati huo huo ungalie pia wale waliofanikiwa uzingatie yale yaliyowasababisha wafanikiwe ili yakusaidie pia.

Rafiki unaweza kuwashirikisha wengine kuhusu blogu hii kwa ajili ya kupata maarifa mbalimbali na pia unaweza kubofya hapa ili kuweza kupata makala kila inapowekwa kupitia barua pepe yako.

Goodluck Moshi
Author
StadizaMafanikio

Monday 28 November 2016

Jinsi Ya Kutambua Uwezo wa Kompyuta Yako

Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio!

Rafiki kompyuta ni kifaa ambacho kinachukua nafasi kubwa katika matumizi ya kazi mbalimbali katika zama hizi za habari. Kompyuta zina sifa mbalimbali kutegemeana na mahitaji ya kazi zinazokwenda kufanya. Hivyo ni muhimu kujua namna ya kuthibitisha sifa zilizobebwa na kompyuta husika kabla hujanunua.

Katika makala ya leo napenda kukushirikisha njia ya kuangalia sifa tatu muhimu za kompyuta ambazo ni muhimu kuzikagua.

(a) Bofya kitufe cha kulia cha mouse katika neno Computer mara baada ya kuwasha kompyuta yako. Kisha chagua sehemu iliyoandikwa Properties , bofya. Hapa utapata taarifa kuhusu aina ya processor iliyowekwa katika kompyuta na memory iliyowekwa katika kompyuta pia. Processor hupimwa kwa kipimo cha GHz.

Soma Makala Hii Inayohusiana : Jinsi ya Kutumia Kompyuta Yako Kuwa Chanzo cha Intaneti

Katika kipengele cha System kwenye kurasa ya properties iliyofunguka taarifa za processor utazikuta katika sehemu iliyoandikwa Processor.
Na taarifa za memory utazikuta katika sehemu iliyoandikwa Installed memory (RAM). RAM hupimwa kwa kipimo cha GB.

(b) Bofya kitufe cha kulia cha mouse katika neno Computer mara baada ya kuwasha kompyuta yako. Kisha chagua sehemu iliyoandikwa Manage, bofya.
Chagua tena sehemu iliyoandikwa Disk Management, kisha angalia sehemu iliyoandikwa Disk 0 ndiyo sehemu utakayopata ukubwa wa hard disk iliyowekwa katika kompyuta. Hard disk hupimwa kwa kipimo cha GB kama ilivyo kwa RAM.

Rafiki unaweza kuwashirikisha wengine kuhusu blogu hii kwa ajili ya kupata maarifa mbalimbali na pia unaweza kubofya hapa ili kuweza kupata makala kila inapowekwa kupitia barua pepe yako.

Goodluck Moshi
Author
StadizaMafanikio

Sunday 27 November 2016

Namna Ya Kudelete File Katika Kompyuta

Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio!

Rafiki moja ya operation ambayo inafanyika mara kwa mara katika matumizi ya kompyuta ni delete. Delete hufanya kazi ya kufuta file lililopo katika sehemu au location katika kompyuta.

Kuna namna mbili ambazo unazoweza kutumia kufuta file katika kompyuta:

(a) Katika namna hii ya kwanza unachagua file unalotaka kulifuta kisha unabofya kitufe katika keyboard kilichoandikwa delete au unabofya kitufe cha kulia cha mouse na kuchagua delete.

Soma Makala Hii Inayohusiana : Jinsi ya Kutengeneza Bootable USB Drive

Mara baada ya kubofya, file litondolewa kutoka sehemu iliyopo kwenda katika recycle bin. Unaweza kulirudisha file ikiwa umelifuta kwa makosa kwa kubofya na kuchagua restore. Ikiwa pia unataka ulifute katika recycle bin basi rudia hatua za kawaida za kufuta file kama nilivyoelekeza hapo juu.

(b) Katika namna hii ya pili unachagua file unalotaka kulifuta kisha unabofya kwa pamoja (simultaneously) vitufe katika keyboard shift na delete.

Mara baada ya kubofya, file litaondolewa kutoka sehemu iliyokuwa lakini halitapelekwa katika recycle bin. Hapa unakuwa hauwezi kulirudisha file lilipokuwa. Hii hufahamika kama kudelete permanently

Rafiki unaweza kuwashirikisha wengine kuhusu blogu hii kwa ajili ya kupata maarifa mbalimbali na pia unaweza kubofya hapa ili kuweza kupata makala kila inapowekwa kupitia barua pepe yako.

Goodluck Moshi
Author
StadizaMafanikio

Saturday 26 November 2016

Uchambuzi Kitabu cha " THE COMPOUND EFFECT"

Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio!

Darren Hardy ni mwandishi wa kitabu cha THE COMPOUND EFFECT. Katika kitabu hiki mwandishi anatueleza siri kubwa iliyopo katika kufanya mambo hatua kwa hatua kidogo kidogo ili kufikia mafanikio. Hapa tunajifunza kuwa mafanikio ni mchakato na sio kitu ambacho kitatokea mara moja. Hapa chini ninakushirikisha yale mambo ambayo nimejifunza.

1. Fanya maamuzi ya kudhibiti/kuyaongoza maisha yako kwa kutafuta kujifunza kutoka kwa watu waliofanikiwa na kuyaweka katika katika miaka yako ambayo una nguvu/mapema kabla umri haujaongezeka sana

2. Kama unahitaji mafanikio makubwa wasaidie wengine wafanikiwe zaidi

3. Amua kufanya maisha yako kuwa maabara yako binafsi kwa ajili ya kujaribu kanuni mbalimbali za mafanikio kufanyiwa mafunzo na utafiti

4. Maamuzi yako yanatengeneza hatma yako

5. Maamuzi yako unayoifanya kila siku yanaamua kukuwezesha kufikia maisha unayotaka au kufikia maafa ya maisha unayotaka

6. Kama hujui kitu fulani weka jitihada na unadhifu katika kujifunza mpaka uweze kukivuka kikwazo

7. Si jambo/hatua nzuri ya mafanikio katika maisha kwenda pamoja na kundi (kimazoea) kuwa mtu ambaye anafanya mambo ya tofauti na makubwa

8. Unahitaji ari na uwajibikaji ili kuweza kuyafikia mafanikio unayoyahitaji

9. Tengeneza fedha na mali za kutosheleza kutunza familia yako maisha yao yote hata kipindi ambacho huna uwezo wa kufanya kazi au haupo kabisa

10. Hatua ndogo unazochukua na kuzifanya kwa muda kwa msimamo bila kusitisha au kuruka huleta mabadiliko kwa kiasi kikubwa

11. Machaguo nadhifu madogo + Msimamo + Muda = Tofauti kwa kiasi kikubwa

12. Siri ya mafanikio ambayo wazazi wetu wametumia katika maisha yao ni jitihada, bidii, nidhamu na tabia njema

13. Unashindwa pale unapoanza kuacha kufanya vile ambavyo vilikufanya ufanikiwe

14. Maisha yetu huishia kuwa ni matokeo ya machaguo tunayofanya

15. Ukiamua kukaa na kutokufanya uchaguzi maanake umeamua kupokea machaguo yoyote yanayokuja kwako

16. Bila kujali maamuzi unayofanya ni madogo kiasi gani, pale yanapofanywa kwa kulimbikizwa kwa muda mrefu huleta athari/faida

Soma Makala Hii Inayohusiana : Uchambuzi wa Kitabu " TOUGH TIMES NEVER LAST BUT TOUGH PEOPLE DO"

17. Unapofanya uchaguzi hakikisha unafikiria kwanza

18. Pale unapoamua kuwajibika 100% kitu kifanikiwe ndipo utapata mafanikio katika kitu hicho

19. Unawajibika kwa kila unachokifanya, usichokifanya na vile ambavyo utaitikia vile ulivyofanyiwa

20. Fursa inapokutana na maandalizi mazuri hutengeneza bahati

21. Kanuni ya bahati
     Maandalizi + Mtazamo + Fursa + Matendo = Bahati

22. Hatua ya kwanza kuelekea mabadiliko ni kufahamu/kutambua (awareness)

23. Huwezi kuboresha kitu bila kukifatilia na kukipima

24. Kitu chochote hakiwezi kuwa tabia mpaka ukifanyie kazi kwa wiki 3

25. Fanya machaguo sahihi kila siku kila wiki na mapema utaanza kuona utoshelevu kifedha katika maisha yako

26. Kila siku fanya uchaguzi wa kusonga mbele

27. Marekebisho kidogo katika mambo yale yale ya kila siku hubadilisha kwa kasi matokeo katika maisha yako

28. Fanya kitu cha tofauti ili upate matokeo tofauti na bora zaidi

29. Watu waliofanikiwa wanajua malengo yao kwa ufasaha ,wanajua wao ni nani na wanataka kuwa nani

30. Watu wasiofanikiwa wanajua malengo yao katika vichwa vyao hawayaandiki sehemu ambayo watajikumbusha mara kwa mara

31. Unatakiwa kuwa na malengo katika kila sehemu ya maisha yako
sio malengo ya upande mmoja mfano fedha peke yake

32. Unatakiwa uwe na ulinganifu katika kila eneo la maisha yako: biashara, fedha, afya, kiroho, kifamilia na mahusiano

33. Mafanikio ni kitu ambacho unakivuta kwa kuwa mtu anayevutia

Rafiki unaweza kuwashirikisha wengine kuhusu blogu hii kwa ajili ya kupata maarifa mbalimbali na pia unaweza kubofya hapa ili kuweza kupata makala kila inapowekwa kupitia barua pepe yako.

Goodluck Moshi
Author
StadizaMafanikio

Read, Apply and Share!

Friday 25 November 2016

Njia Bora Ya Kukabili Changamoto Yoyote

Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio!

Rafiki maisha tunayoishi yana changamoto za aina mbalimbali. Changamoto hizi ni njia pekee ambayo kama utaiitumia vizuri itakusaidia kukusogeza hatua ya ziada.

Katika makala ya leo napenda kukushirikisha namna bora ambayo itakusaidia namna ya kukabili au kuzitatua changamoto.

Jambo la kwanza rafiki usifanye kosa la kuhangaika na dalili za tatizo. Hakikisha unafahamu kile kilicho nyuma ya dalili ambazo unaziona, yaani sababu zilizopelekea changamoto kutokea.

Jambo la pili ni kuwa na kipaumbele wakati unatatua matatizo. Changamoto haziji katika mpangilio bali huja nyingi kwa wakati mmoja. Siri ya pekee itakayokusaidia ni kuwa na mpangilio unaokuelekeza kutatua changamoto moja baada ya nyingine hatua kwa hatua.

Jambo la tatu hakikisha unakuwa na ufasaha kuhusu changamoto unayoipitia. Njia ya pekee ya kukusaidia kupata ufasaha ni kujiuliza changamoto ni nini hasa , hii inakusaidia kufocus.

Jambo la nne hakikisha unatafuta watu ambao watakusaidia wakati unapitia hatua ya kutatua changamoto. Hawa watakusaidia kutambua au kuona mambo ambayo huwezi kuyaona kama ungekuwa peke yako.

Soma Makala Hii Inayohusiana : Uchambuzi wa Kitabu " TOUGH TIMES NEVER LAST BUT TOUGH PEOPLE DO"

Jambo la tano hakikisha unakusanya mambo yote ambayo yaliyosababisha changamoto unayoipitia.

Jambo la sita rafiki hakikisha unaorodhesha njia zote ambazo zinaweza kukusaidia kutatua tatizo husika. Kisha chagua njia ambayo ni bora kuliko njia zote ambazo umeziorodhesha

Jambo la saba hakikisha unafanyia kazi njia uliyoichagua na kisha unaifanyia tathmini ili iweze kukusaidia kujua kama umetatua changamoto unayoipitia au la.

Rafiki unaweza kuwashirikisha wengine kuhusu blogu hii kwa ajili ya kupata maarifa mbalimbali na pia unaweza kubofya hapa ili kuweza kupata makala kila inapowekwa kupitia barua pepe yako.

Goodluck Moshi
Author
StadizaMafanikio

Read, Apply and Share!

Wednesday 23 November 2016

Kwa Nini Unahitaji Kujifunza Jambo Jipya Kila Siku?

Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio!

Rafiki mabadiliko na ukuaji ni vitu viwili muhimu vyenye mchango mkubwa katika maisha tunayoishi kila siku. Maisha yanakua na ladha ambayo inatufanya kuendelea kuyafurahia kwa sababu ya mabadiliko na kukua.

Kujifunza ni jambo la muhimu zaidi ambalo tunahitaji kulipokea au kulikubali au kulifurahia kila wakati tunapopata fursa. Unaweza kujifunza mambo mengi mbalimbali kutegemeana na mapenzi na shauku ya maeneo ambayo unapenda kuwa na maarifa.

Soma Makala Hii Inayohusiana : Hii Ndiyo Njia Pekee ya Kutatua Matatizo Yako Yote

Unaweza kujifunza kutoka katika uzoefu alionao mtu au uzoefu ulionao, kutoka kwa mtu unayemfahamu, kutoka katika kitabu, kutoka katika semina,mkutano, kutoka kwa wazazi, kutoka kwa mtoto wako, mwenzi wako na kadhalika.

Kwa kadiri tunavyozidi kujifunza vile vile ndivyo tunavyozidi kukua na kuyapatia maisha yetu thamani zaidi. Rafiki unapojifunza usiende ukiwa na yale mambo unayoyafahamu tu na kuyang'ang'ania kuwa ndiyo sahihi na hutaki kupokea mambo mapya tofauti na unayofahamu , hapana rafiki unahitaji kuwa open ili uweze kuimarisha maarifa uliyonayo.

Rafiki unaweza kuwashirikisha wengine kuhusu blogu hii kwa ajili ya kupata maarifa mbalimbali na pia unaweza kubofya hapa ili kuweza kupata makala kila inapowekwa kupitia barua pepe yako.

Goodluck Moshi
Author
StadizaMafanikio

Read, Apply and Share!

Tuesday 22 November 2016

Uchambuzi Kitabu cha " MEGALIVING, 30 DAYS TO PERFECT LIFE"

Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio!

Robin Sharma ni mwandishi wa kitabu cha MEGALIVING, 30 DAYS TO PERFECT LIFE. Katika kibao hiki Robin anaeleza namna ambavyo unaweza kuyabadilisha maisha yako kwa kutumia uwezo wako na kuyafanya kuwa bora. Hapa nakushirikisha mambo ambayo nimejifunza katika kitabu hiki.

1. Hakuna shaka Unayo nguvu ya ajabu inayoweza kukuwezesha kufanikiwa katika lolote ulilolipanga/unalotazamia

2. Kuwa bora kwa kadiri inavyowezekana

3. Ukitaka kuweza kuingoza familia, kampuni ni lazima uanze kujiongoza / kujitawala wewe mwenyewe kwanza

4. Hakuna makosa katika maisha bali kuna masomo ya kujifunza kutoa fursa ya kukua na kupanda ngazi katika njia ya mafanikio

5. Usiwe mfungwa wa maisha yako yaliyopita bali uwe mbunifu/msanifu anayeunda maisha ya baadae

6. Mawazo yako ya leo yanatengeneza ndoto zako za kesho

7. Ni muhimu ukaanza kujiendeleza mwenyewe kwa kutengeneza uwezo wa akili na nidhamu kubwa mno katika maisha yako

8. Mafanikio ili yaonekane nje ni lazima yaanzie ndani kwako

9. Kitu chochote akili ya binadamu kinachoweza kukiwaza na kukiamini kinaweza kukipata

10. Yatambue mawazo uliyonayo yanayokuletea kikwazo na uyaondoe kabisa katika ufahamu na badala yake uweke mawazo yanayokupa nguvu, tumaini, hamasa pamoja na utimizaji wa ndoto zako

11. Ukiweza kutawala akili yako, unaweza kutawala maisha yako na ukiweza kutawala maisha yako utaweza kutawala hatima ya maisha yako (destiny)

12. Ukiendelea kufanya mambo yale yale kila siku utapata matokeo yale yale kila siku

13. Ushindi mdogo mdogo ndio hupelekea ushindi mkubwa

14. Kuwa na ari ya kuboresha kila siku maeneo ya msingi katika maisha yako na kuwa bora kadiri inavyowezekana

15. Hakuna kitu kinachoweza kumkwamisha mtu ambaye amekataa kukwamishwa

16. Watu waliofanikiwa daima wana kiu ya mawazo mapya na maarifa mapya

Soma Makala Hii Inayohusiana : Uchambuzi wa Kitabu " LUNCHTIME TRADER"

17. Mambo 3 muhimu kuhusu akili yako
a) Kujifunza namna ya kuiongoza/kuiendesha akili yako kama mshindi
b) Akili yako Ina uwezo wa kufanya mambo makubwa mazuri ya kushangaza Kama utairuhusu kufanya hivo
c) Vizuizi ni vile tu ambavyo unajiwekea we mwenyewe

18. Ngazi ya mafanikio yako inategemea kile unachofikiria kila sekunde, kila dakika kila siku

19. Ukitaka kubadili maisha yako unahitaji kubadili aina ya mawazo unayoweka akilini mwako

20. Unawajibika kwa kile unachofikiria Unao uwezo wa kuamua kuacha na kuondoa kufikiri hasi.

21. Taswira zetu binafsi zinazopita katika akili zetu ndo zinaamua sisi kuwaje

22. Unaweza kufanikiwa katika chochote ikiwa Una taarifa sahihi

23. Kila mtu mwenye mafanikio ni kwa sababu amekuwa na nidhamu ya kutosha

24. Kuwa na matarajio mazuri na siku zote uwaze mambo makubwa

25. Vikwazo vyote vinavyokuchelewesha kufikia mafanikio vinaweza  kubadilishwa kwa kuwa na mikakati sahihi

26. Inatakiwa kuwaza chanya ili kuweza kufanikisha kisichowezekana na kuweza kuwa vile unavyotakiwa kuwa

27. Hatua 7 za kufikia malengo yako:
a) Fahamu nini unachokitaka
b) Weka malengo sahihi na tarehe ya mwisho ya kuyafikia pamoja na mikakati
c) Kuhusu malengo yako yatawale mawazo yako
d) Weka msukumo kwa ajili ya faida yako
e) Tafuta network ya watu watakaokusapoti
f) Kumbuka kanuni ya 21
g) Furahia na ujipatie tuzo

28. Tumia muda wako vizuri

29. Unaweza kujifunza kitu kutoka kwa kila mtu

30. Hekima inayopatikana kwa kujifunza huwa haisahauliki

31. Unahitaji kulala si zaidi ya masaa 6, jifunze kuamka mapema kwa siku 21 mfululizo na utakuwa umeshajenga tabia hiyo

32. Tenga lisaa limoja kila siku asubuhi kwa ajili ya maendeleo binafsi (personal development)

33. Ubongo wa binadamu ukishatanuka kwa kupata wazo jipya hauwezi kurudi katika size yake ya swali

34. Tumia kila jumapili jioni kupangilia namna ambavyo unataka wiki yako iende mfano vitabu unavyotaka kusoma, kazi utakazozifanya

35. Kile unachokiwekea mkazo (focus) ndicho utalachokipata

36. Bakia katika lengo na sio matokeo

37. Kuwa mtu mwenye nidhamu ya hali ya juu ya kutunza muda

38. Njia ya kujisomea ni njia yenye nguvu ya kujizolea miaka mingi ya uzoefu ndani ya muda mchache wa kujifunza

39. Jipatie tuzo hata kwa mafanikio madogo

40. Kuwa mkweli na mvumilivu

41. Usikatishwe tamaa pale majibu yanapochelewa kujitokeza

42. Tumia shajara (diary) kupima maendeleo yako na kunakili mawazo unayopata kila wakati

43. Jaribu kufunga (fasting) siku moja kila baada ya wiki 2. Na ule matunda na juice ya matunda tuu.

44. Samehe hata kama mazingira ni magumu

45. Tazama kila fursa Kama nafasi ya kujifunza

46. Kunywa kikombe cha maji ya moto kabla hujaanza kuhutubia ili kupata stamina nzuri ya kuhutubu

47. Kuwa na ujasiri, wahamasishe wengine kupitia matendo yako na pia uwe unawafikiria wengine

48. Usiulize ulimwengu utakufanyia nini bali jiulize utaufanyia nini ulimwengu, kuwa na lengo la kutoa huduma ulimwenguni

49. Nenda katika semina mbalimbali kwa ajili ya kupata uzoefu wa watu mbalimbali katika Yale unayotaka kufanya ambayo wengine wametumia muda mwingi kujifunza au kuyajua

50. Tembea kwa muda wa nusu saa kila unapomaliza kula chakula cha usiku

51. Uwe na kiasi kwa kila unachokifanya usipitilize

52. Katika vitabu vya maendeleo binafsi, chukua kile unachokihitaji na ambacho kinaweza kufanyika kwako na kile ambacho hakiendani nawe kiache

53. Siku iliyotumiwa vizuri huleta usingizi mzuri

54. Tafuta mshauri ambaye atakuongoza katika maendeleo yako

55. Orodhesha madhaifu yako yote na tafuta mbinu za kuboresha

56. Usilalamike

57. Kuwa na huruma, mwenye kufikiria wengine na mwenye adabu

58. Watu waliofanikiwa hufikiri mara tatu kabla ya kutamka neno

59. Zungumza mambo mazuri tuu kuhusu watu

60. Fanya mambo yawe mepesi kwa watu

61. Jifunze namna ya kupangilia muda wako

62. Mambo ambayo tusiyoyapenda huwa yanaendelea kuja na yale tunayoyapenda hayaji tunapotaka kuyakumbuka

63. Andaa mpango wa kina wa kifedha wa miaka kadhaa ambao utaufata

64. Furahi kwa kile ulichonacho

65. Jenga tabia ya kutoa zaidi kuliko kupokea

66. Usiongee wakati unasikiliza

67. Watu waliofanikiwa wana kiu na shauku kubwa ya maarifa

68. Weka mkazo katika malengo yako na soma yale mambo ambayo ni ya manufaa tu kwako

69. Kile ambacho unakitafuta utakipata

70. Tumia dakika 10 kila siku kabla hujalala kujitathmini

71. Fikiria mambo mazuri ambayo umeweza kuyafanya na yale mabaya ili ujifunze kwa ajili ya kukua na kusonga mbele

72. Kabla hujatoka kitandani hakikisha unasema maneno chanya au  unafanya maombi kwa ajili ya kuifanya siku yako ya mafanikio

73. Kuwa mbunifu ambae unampa maoni yako 10 kila wiki msimamizi wako wa kazi kwa ajili ya kuboresha kazi mnayofanya

74. Kila siku fanya mambo mawili ambayo hupendi kuyafanya hata Kama ni madogo we fanya tuu

75. Lala kidogo, tumia fedha kidogo ,fanya kazi zaidi

Goodluck Moshi
Author
StadizaMafanikio

Read, Apply and Share!

Monday 21 November 2016

Tofauti Ya Matumizi Ya Copy na Cut

Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio!

Katika matumizi ya kompyuta kila siku kuna operations ambazo hufanywa mara kwa mara ili kukuwezesha kukamilisha kazi (task) uliyokuwa unaifanya. Kwa bahati nzuri teknologia hii imeenea sana mpaka kugusa pia simu za mkononi.

Rafiki moja ya operations ambazo hufanyika mara kwa mara katika kompyuta ni cut na copy. Katika makala hii napenda kukuelezea kwa kina tofauti ya hizi operations.

(a) Cut
Operation hii imebeba lengo la kuondoa bila kuacha kitu kutoka katika eneo la awali ambapo kitu kinatolewa (source) na  kwenda eneo lingine ambalo limekusudiwa (destination).

Ikiwa cut itatumika katika maneno , sharti kwanza maneno yawekewe kivuli (highlight), alafu ndipo operation ya cut ifuate. Baada ya kufanya operation hii maneno yaliyotiwa kivuli yataondolewa kabisa (permanently ) kutoka katika source na yataweza kuwekwa katika destination kwa kufanya operation ya paste.

Cut pia inaweza kutumika kwa folder, folder ni kundi lililokusanya vitu aidha vinavyofanana ama mbalimbali katika sehemu moja kwa lengo la kusaidia upatikanaji wakati vinatafutwa.

(b) Copy
Operation hii imebeba lengo la kunakili kitu kutoka katika source na kupeleka katika destination. Kwa hiyo operation hii husababisha vitu vilivyomo katika source kufanana na vile vilivyopo katika destination.

Soma Makala Hii Inayohusiana : Jinsi ya Kuzuia Kupoteza Makala Katika Blogu Yako (Backup)

Kama ilivyokuwa kwa upande wa cut , vile vile ukihitaji kucopy maneno utahitaji kwanza kuyaweka kivuli ,kisha utayacopy. Hali kadhalika katika folder.

(c) Matumizi
Tumia cut ikiwa unataka kuhamisha au kuondoa kabisa file, document au folder kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine.

Tumia copy ikiwa unataka kuweka nakala sehemu zaidi ya moja kwa ajili ya kuchukua tahadhari na upotevu wa kazi (backup).

(d) Mipaka (Limitations)
Katika cut ikiwa source na destination ni ile ile (yaani si sehemu tofauti) , unapofanya hii operation hautaona mabadiliko itabaki kama ilivyokuwa kabla ya kufanya cut

Katika copy ikiwa source na destination ni ile ile (yaani si sehemu tofauti), unapofanya hii operation itatengenezwa nakala nyingine yenye jina linalofanana na lile la awali likiwa limeongezewa mabano na namba 1 yaani (1). Namba hii inaonesha ni mara ya ngapi umefanya hii operation, ukifanya tena kwa mara ya pili basi itaandika jina kama la awali na kuongeza (2).

Rafiki unaweza kuwashirikisha wengine kuhusu blogu hii kwa ajili ya kupata maarifa mbalimbali na pia unaweza kubofya hapa ili kuweza kupata makala kila inapowekwa kupitia barua pepe yako.

Goodluck Moshi
Author
StadizaMafanikio

Sunday 20 November 2016

Uchambuzi wa Kitabu " LUNCHTIME TRADER"

Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio!

Marcus de Maria ni mwandishi wa kitabu cha THE LUNCH TIME TRADER. Katika kitabu hiki mwandishi ametueleza namna ambavyo unaweza kutumia muda ambao unautumia kwa ajili ya chakula cha mchana kukusaidia kupata mafanikio ambayo umekuwa ukiyahitaji.

1. Maamuzi katika matendo mbalimbali ambayo tunayafanya ndio yanaamua matokeo tunayoyapata na kusababisha kutofautisha mtu  mmoja na mwingine

2. Hali ya kifedha tuliyonayo inatanuliwa kwa sehemu kubwa na mawazo, imani na mtazamo tuliyonayo

3. Hatua saba muhimu zinazoweza kukisaidia kuanza kufanya mabadiliko katika hali yako ya sasa
a) Fahamu hali yako ya sasa
b) Fahamu hali yako ambayo unataka uwe nayo
c) Tambua mbinu au njia inayoweza kukufikisha katika (b)
d) Tengeneza imani kuhusu mbinu unayotumia kuwa itakufikisha
e) Anza mara moja
f) Jiboreshe katika hiyo njia au mbinu
g) Ongeza kasi

4. Ishu sio kiasi gani cha fedha unatengeneza bali ni kiasi gani cha fedha ungeweza kukiweka na kukikuza

5. Kitu chochote ambacho umekitilia mkazo kwa kuweka muda na jitihada baada ya muda huwa kinakua

6. Usifanye kosa la kumpa mtu mwingine awekeze fedha badala yako mwenyewe

Soma Makala Hii Inayohusiana : Uchambuzi wa Kitabu cha "ACT LIKE A SUCCESS THINK LIKE A SUCCESS"

7. Ni vizuri kuwa na mikakati ya siku, wiki, mwezi na mwaka pia

8. Kwa siku nzima unaweza kufanya kazi kwa bidii ili kuingia fedha lakini tenga dakika 20 tu za kufanya fedha yako ifanye kazi kwa jitihada kwa ajili yako

9. Tumia muda wa wiki sita sita kuamua kama kuendelea kubaki na hisa au kuziuza

10. Mikakati unayotumia katika uwekezaji ni lazima iwe na ukomo ili uweze kuboresha mikakati na kutafuta mingine kutokana na mazingira katika eneo la uwekezaji linavobadilika

11. Ni muhimu kuwa na ufuatiliaji wa mwenendo wa mtiririko wa hisa jinsi unavyoperform

12. Katika biashara yoyote usipoteze fedha nyingi sana

13. Katika uwekezaji huhitaji kumtegemea sana broker kwa sababu unashindwa kujua mikakati na mbinu za namna ya kufanya uwekezaji

14. Kanuni ya kwanza ya ulimbikizaji inasema uanze na kiwango kikubwa kadiri inavyovezekana

15. Kanuni ya pili ya ulimbikizaji inasema uendelee kuwekeza kiwango kikubwa kadiri inavyowekeza kila mwezi

16. Faida inayopatikana ni vema ikawekezwa

17. Mjue mtu mmoja ambae unataka uwe kama yeye alafu iga  kufanya yale anayoyafanya yeye pia

18. Ni vizuri broker akaulizwa ana hisa ngapi katika hiyo kampuni anayokushauri uwekeze.

Rafiki unaweza kuwashirikisha wengine kuhusu blogu hii kwa ajili ya kupata maarifa mbalimbali na pia unaweza kubofya hapa ili kuweza kupata makala kila inapowekwa kupitia barua pepe yako.

Goodluck Moshi
Author
StadizaMafanikio

Saturday 19 November 2016

Tofauti Kati Ya Save Na Save As Katika Programu Za Kompyuta

Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio!

Katika programu zinazotumika katika kompyuta , njia ya pekee ya kukulinda usipoteze kazi uliyofanya ni kusave. Katika kila programu maneno haya Save na Save As utayakuta katika menu ya File.

Kwa kukuangalia maneno yake yanaonekana kuwa yanafanana sana lakini maneno haya yana tofauti hasa kwa kuzingatia kazi zinazofanywa. Katika makala hii ninapenda kukushirikisha tofauti iliyopo kati ya Save na Save As.

Soma Makala Hii Inayohusiana : Jinsi ya Kubadili Settings za Kusave Katika Microsoft Word

(a) Katika Document Mpya (New Document)
Unapokuwa umefungua document mpya ambayo ndiyo umeanza kuifanyia kazi, Save na Save As hazina tofauti katika utendaji wake kwa mara ya kwanza. Zote zitakuwezesha kuhifadhi kazi yako isipotee.

(b) Katika Document Za Zamani (Existing Document)
Katika document za aina hii unapobofya Save huiuisha document ya mwanzo na kufanya ifanane na inavyoonekana katika screen.Kwa hiyo inaiupdate.

Wakati ukibofya Save As utapata machaguo ya kubadili jina la document au tolea la document au kubadili extension (mfano .docx kuwa doc).

(c) Katika Intaneti
Unapokuwa unatumia mtandao wa intaneti, ukibofya kitufe cha kulia cha mouse (right click) katika link utapata pia chaguo la Save As ambayo itakusaidia kupakua document.

Rafiki unaweza kuwashirikisha wengine kuhusu blogu hii kwa ajili ya kupata maarifa mbalimbali na pia unaweza kubofya hapa ili kuweza kupata makala kila inapowekwa kupitia barua pepe yako.

Goodluck Moshi
Author
StadizaMafanikio

Friday 18 November 2016

Uchambuzi wa Kitabu cha "ACT LIKE A SUCCESS THINK LIKE A SUCCESS"

Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio!

Steve Harvey ni mchekeshaji maarufu sana ambaye ameanza fani hii kati ya miaka ya 1980. Pamoja na fani hii ya uchekeshaji Steve ameandika vitabu mbalimbali kama Act Like A Lady, Think Like A Man and Straight Talk , No Chaser na Act Like A Success Think Like A Success.

Katika makala hii ya leo natumia kitabu cha Act Like A Success, Think Like A Success kukushirikisha mambo ambayo Steve anasema yakizingatiwa yatakusaidia jinsi ya kutumia kipaji ulicho nacho kwa ufanisi kukupatia mafanikio katika maisha.

1. Tunapotumia vipawa/vipaji vyetu ipasavyo, ulimwengu hutushukuru kwa kutupatia wingi wa utajiri, kwa kuanzia na wingi wa fursa ,wingi wa afya bora na wingi wa utajiri wa kifedha

2. Kipindi unapoamua kupambana na hofu, utagundua kuwa hofu sio kubwa kama ulivokuwa unawaza. Kitu kinachofanya hofu kuwa kubwa ni kama usipogeuka na kukubali kuanza kuzikabili. Na jinsi unavyochukua muda mrefu kukwepa hofu ndivyo zinavyozidi kuongezeka ukubwa katika akili.

3. Kushindwa ni sehemu ya mchakato unapokuwa katika njia ya mafanikio. Kushindwa huibuka kutokana na ukosefu wa mpango wa kifedha, ukosefu wa rasilimali, ukosefu wa watu sahihi katika timu yako.

4. Usiruhusu kushindwa kukusimamishe eneo moja na kuacha kutafuta/kukamilisha ndoto zako.

5. Kila siku unapoamka ni kwa sababu Mungu ana mipango mikubwa kwa ajili yako na bado haijamalizwa/haijatekelezwa

6. Fursa zipo katika maamuzi yako unayofanya

7. Maswali muhimu ya kujiuliza kwa ajili ya kuchagua chombo sahihi cha kukusafirisha kwenda katika mafanikio ya ndoto yako:
a) Wapi ni mwisho wako wa safari?
b) Kituo chako kinachofata ni kipi?
c) Je unajua namna ya kukiendesha chombo chako kwa kiasi ambacho hakitaweza kukupatia ajali(yaani kukuzuia kukua)?

8. Heshimu muda wako na muda wa wengine pia

9. Usiogope kupokea msaada unaohitaji ili kuweza kuishi maisha unayostahili kuishi

10. Mpangilio muhimu unaopaswa kuufata kwa ajili ya mafanikio:
a) Kwanza ni Mungu
b) Pili ni Familia
c) Tatu ni Elimu/Maarifa katika kile unachofanya
d) Nne ni biashara

11. Mungu ameshawapanga katika foleni watu wote unaowahitaji katika njia yako ya kutimiza ndoto zako na maono yako; unachotakiwa kufanya ni kuwaondoa watu wasio sahihi (wasio sawasawa na maono/ndoto zako

12. Kitu ambacho huhitaji kujua ni jinsi gani hautafanikiwa katika kitu fulani unachofanya; unachohitaji kujua ni jinsi gani utafanikiwa katika kitu fulani unachofanya

Soma Makala Hii Inayohusiana : Uchambuzi wa Kitabu cha " EAT THAT FROG"

13. Kuweka mambo katika matendo ndiyo dawa ya kusonga mbele

14. Kumbuka sio kila mtu unayeanza naye safari yako anaweza kwenda mpaka mwisho wa safari unayoelekea

15. Kanuni 6 za kukuwezesha kupata NDIO unapoomba kitu unachohitaji:
a) Jua thamani yako
b) Tambua unachostahili
c) Kuwa maalum (specific) na kile unachokihitaji
d) Kamwe usidhani kuwa wanajua unachohitaji
e) Waeleshe maadili yako kwa vitendo
f) Tambua HAPANA haimaanishi umekataliwa

16. Kuwa na ujasiri wa kuingiza ujuzi wako katika fursa ambazo zitakupatia ukuaji au kupanda ngazi katika eneo lako

17. Chagua kuwa makini na kushiriki katika mabadiliko yanayotokea maishani mwako

18. Kwa kadiri unavyoyakubali mabadiliko na kuwa sehemu ya mabadiliko, ndivyo utakavyofanikiwa zaidi

19. Usiruhusu asili yako ikuwekee mipaka

20. Chagua kila siku kutoruhusu wanaowaza hasi kukusimamisha kutumia karama/kipawa alichokupa Mungu

21. Mlinganyo sahihi kwa ajili ya mafanikio:
a) Nyumbani (home)
b) Afya (health)
c) Fedha (finances)

22. Mafanikio si kitu asipokuwepo yule umpendaye ili kuweza kumshirikisha mafanikio uliyoyapata

23. Usiruhusu mtu kuja nyumbani na kuvuruga amani na utulivu ulioutengeneza kwa ajili yako na familia yako

24. Mungu anakubariki ili uwe mtoa baraka

Rafiki unaweza kuwashirikisha wengine kuhusu blogu hii kwa ajili ya kupata maarifa mbalimbali na pia unaweza kubofya hapa ili kuweza kupata makala kila inapowekwa kupitia barua pepe yako.

Goodluck Moshi
Author
StadizaMafanikio

Thursday 17 November 2016

Uchambuzi wa Kitabu cha " EAT THAT FROG"

Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio!

Brian Tracy ni mwandishi wa kitabu cha "EAT THAT FROG". Brian ni mwalimu mwenye uzoefu sana katika eneo la mafanikio. Mambo mengi ambayo Brian anatushirikisha ni yale ambayo amekuwa akijifunza, kisha anayafanyia kazi yeye binafsi na ndipo anatushirikisha kupitia vitabu vyake. Katika kitabu hiki ametushirikisha namna ya kupambana na hali ya kuahirisha mambo uliyopanga kuyafanya.

1. Kuwa na nidhamu ya kutekeleza jambo lolote mara tu unapolipata na uendeleee kulifanyia kazi mpaka likamilike kabla hujaenda kutekeleza jambo lingine

2. Ni muhimu kuamua nini unataka kufanya katika kila eneo linalohusu maisha yako

4. Fahamu kwa ufasaha ni kitu gani kinatarajiwa kutoka kwako na katika mpangilio upi wa kipaumbele

5. Orodhesha mambo ambayo unayajua ni ya lazima uyafanye ili ufikie malengo

6. Endelea kupitia malengo yako na uyaboreshe siku hadi siku

7. Kupangilia ni kuleta baadae sasa ili uweze kufanya kitu kwa ajili ya baadae

8. Kuamua kufanya vitu bila kufikiria ndiyo chanzo kikubwa cha matatizo

9. Ni vizuri kuwa na orodha mbalimbali kwa madhumuni mbali mbali
a) Orodha kuu
b) Orodha ya mwezi
c) Orodha ya wiki
d) Orodha ya siku

Soma Makala Hii Inayohusiana : Uchambuzi wa Kitabu cha " SECRETS OF SELF MADE MILLIONAIRE"

10. Orodhesha malengo yako yote unayotaka kuyatimiza alafu uchague lengo moja ambapo ukilifanya hilo liyasababisha mengine yote kuyafanikisha

11. Weka malengo yako kwa kipaumbele kujua lipi ni muhimu kwanza na pia iwe katika mtirirko kujua lipi linaanza, lipi linafuata na lipi linamalizia

12. Muda utakaoutumia kufanya kazi isiyo na umuhimu ni sawa na muda ambao utautumia kufanya kazi iliyo na umuhimu

13. Amua leo kufanya yale mambo ambayo yataleta mabadiliko katika maisha yako

14. Hakuna muda wa kutosha kufanya kila kitu ila kuna muda wa kutosha kufanya jambo lililo na umuhimu

15. Neno lenye nguvu kati ya maneno yote yanayohusiana na muda ni neno Hapana

16. Ili kufanya jambo jipya unahitaji kumaliza au kuacha kabisa kufanya mambo ya zamani

17. Fanya vile vitu ambavyo vinaboresha maisha yako

18. Jenga nidhamu ya kutofanya jambo lingine lolote isipokuwa lile moja tuu uliloanza mpaka likamilike

19. Kamwe usiache kujiboresha

20. Maeneo matatu ambayo wengi huweka malengo:
a) Kwanza ni fedha na kazi
b) Pili ni familia au mahusiano
c) Tatu ni afya

21. Uhuru wa kifedha unafikiwa kwa kuweka akiba kila mwezi mwaka hadi mwaka

22. Jisomee katika eneo unalotaka kuwa mtawala angalau kwa saa limoja kwa siku

23. Ni muhimu utambue kwa ufasaha mambo yanayokuzuia kutoka halo ulipo kufikia unapoelekea katika malengo yako

24. Katika wiki tenga siku moja kwa ajili ya kufanya mambo tofauti kama kufanya shughuli ambazo hazihusishi kutumia ubongo au akili yako

25. Lala saa limoja kabla kila siku

26. Yafanye matatizo yako yawe binafsi sababu asilimia 80 hawajali kuhusiana na hayo matatizo yako na asilimia 20 wanayo furaha matatizo yamekupata

27. Mambo manne ya kuzingatia
a) Tafuta kitu kizuri katika kila jambo bila kujali ni baya kiasi gani
b) Jiulize somo gani la thamani unajifunza kutokana na ugumu au kikwazo unachopitia
c) Tafuta utatuzi wa kila tatizo
d) Endelea kufikiria na kuongea kuhusu malengo yako

Rafiki unaweza kuwashirikisha wengine kuhusu blogu hii kwa ajili ya kupata maarifa mbalimbali na pia unaweza kubofya hapa ili kuweza kupata makala kila inapowekwa kupitia barua pepe yako.

Goodluck Moshi
Author
StadizaMafanikio

Wednesday 16 November 2016

Faida Tatu (03) za Biashara Inayoendeshwa Kwa Intaneti

Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio!
Rafiki katika zama za viwanda (industrial age) bidhaa nyingi zilizokuwa zinauzwa zipo physical kiasili. Bidhaa hizi mpaka uzinunue ulihitaji kuzishika au kuziona kwa kukutana na muuzaji ana kwa ana. Lakini leo hii tupo katika zama za habari (information age) ambapo mambo ni tofauti na kipindi cha nyuma.





Hapa ninakushirikisha faida utakazozipata kwa kuwa na biashara inayoendeshwa kwa kutumia teknologia ya intaneti.
Soma Makala Hii Inayohusiana : Mambo Matano (05) Yanayosababisha Kushindwa
(a) Uwepo Wako Katika Eneo la Biashara
Katika zama za viwanda biashara inakuhitaji kuwepo katika eneo la biashara muda wote ili kuiendesha (full time). Lakini biashara inayoendeshwa kwa teknologia ya intaneti unahitaji idadi ya masaa mawili au matatu kuiendesha hauhitaji kuwepo eneo la biashara muda wote (part time). Mfano wa biashara hii ni blogu ambapo muda utakaoutumia ni ule ambao unatengeneza makala.
(b)  Masoko
Katika zama za viwanda biashara inaendeshwa katika maeneo yale ambayo bidhaa yako inafika ,hivyo siku lako sio pana. Lakini katika zama za taarifa biashara inaendeshwa katika eneo pana zaidi,kwa sababu soko lako ni mtandaoni, hivyo kila mtu anayeweza kuingia mtandaoni anakuwa ni mmoja kati ya wale waliopo katika soko lako.
(c) Muda wa Kutoa Huduma
Katika zama za viwanda masaa ya kufanya kazi au biashara ni muda ule ambao watu wanakuwa eneo la biashara , huu muda unaitwa muda wa kazi (office hours). Lakini katika zama za taarifa masaa ya kufanya kazi ni masaa 24 kutokana na huduma kupatikana katika mtandao muda wote.
Rafiki unaweza kuwashirikisha wengine kuhusu blogu hii kwa ajili ya kupata maarifa mbalimbali na pia unaweza kubofya hapa ili kuweza kupata makala kila inapowekwa kupitia barua pepe yako.
Goodluck Moshi
Author
StadizaMafanikio

Tuesday 15 November 2016

Mambo Matano (05) Yanayosababisha Kushindwa

Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio!

Rafiki si wote wanajifunza kutokana na makosa wanayoyafanya au kutambua mapema makosa waliyoyafanya ili wasiyarudie. Kuwa na mwongozo kutasaidia sana kujua namna ya kuenenda katika mambo haya.

Katika maisha ya kila siku kuna mambo matano yanayosababisha kushindwa. Ukiyafahamu na kujua jinsi ya kuyakabili utakuwa umesaidia kuondoa vizuizi katika njia yako ya kuelekea mafanikio.

Jambo la kwanza ni kulaumu wengine kuwa ndiyo wamesababisha kutokea kushindwa. Hii hali hujitokeza kipindi ambapo kosa limetokea badala ya kubeba wajibu wa kuuliza mambo gani yamechangia kuwafikisha katika kushindwa badala yake unamtafuta mtu wa kumlaumu kama yeye ndiye chanzo kikuu cha kushindwa.

Jambo la pili lipo kinyume na hilo la kwanza , hapa unakuta unajilaumu binafsi kuwa wewe ni chanzo cha kusababisha kushindwa. Hapa badala ya kupambana na tatizo lililosababisha kushindwa, kupambana ili kulitatua na kuzuia lisijirudie , badala yake unajilaumu. Suala kubwa si kushindwa je umeridhika na kushindwa huko, ukiridhika na kushindwa maana yake umekubaliana na hali na hujipatii nafasi ya kukua kupitia kujiendeleza binafsi.

Soma Makala Hii Inayohusiana : Namna ya Kutambua Dalili Za Kushindwa

Jambo la tatu ni kutokuwa na malengo. Kukosa malengo ni sawa na kutokuwa na uelekeo wa safari yako yaani unasafiri lakini hufahamu kituo cha mwisho cha safari yako. Kutokuwa na malengo kunasababisha kutokuwa na umakini wa kuzingatia wapi uweze kuelekeza nguvu na vipaji ambavyo umepewa na muumba wako.

Jambo la nne ni kutokuwa na malengo sahihi. Watu wengi wanafanya kosa la kutokupanga malengo yao wao wenyewe badala yake wanawaachia watu wengine kama wanafamilia au marafiki au mazingira kuwasaidia kupanga. Wanapofika mwisho wa safari ya kutimiza lengo husika wanakosa furaha kutokana na kukosa uhusiano wa lengo kutokuwa yeye ndiye mwanzilishi au umiliki wa lengo.

Jambo la tano ni kupenda kutumia short cut. Matumizi ya shortcut huonekana ni njia ya haraka ya kupata matokeo. Changamoto ya njia hii ni kuwa matokeo unayoyapata hayadumu yanakuwa ya muda mfupi , kwa sababu ili kupata matokeo ya kudumu ni lazima kazi ifanyike ambayo huhesabika kuwa ni gharama ya kufikia matokeo husika.

Rafiki unaweza kuwashirikisha wengine kuhusu blogu hii kwa ajili ya kupata maarifa mbalimbali na pia unaweza kubofya hapa ili kuweza kupata makala kila inapowekwa kupitia barua pepe yako.

Goodluck Moshi
Author
StadizaMafanikio

Monday 14 November 2016

Uchambuzi wa Kitabu " HOW SUCCESSFUL PEOPLE THINK"

Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio!
John C. Maxwell ni mmoja wa waandishi maarufu ambao amedumu akitushirikisha mambo mbalimbali ambayo amejifunza katika maisha yake. John ni mwanafalsafa mzuri sana katika eneo la Uongozi. Hapa chini ninakushirikisha maarifa machache kwa muhtasari ambayo nimejifunza kutoka katika kitabu chake cha "HOW SUCCESSFUL PEOPLE THINK".



1. Ikiwa utabadili namna unavyofikiri, utabadili maisha yako
2. Kufikiri vema huleta faida tatu:
a) Kutengeneza mapato
b) Kupata ufumbuzi wa matatizo
c) Kutengeneza fursa
3. Tunahitaji kuwa na sehemu maalum tuliyoitenga kwa ajili ya kufikiri, sehemu hii ni ile ambayo itakufanya uweze kucapture mawazo yote mazuri na mema kutoka kichwani mwako na kuyahamisha katika karatasi kwa ajili ya hatua zaidi bila ya kuwa na usumbufu wowote
4. Ili kuweza kufikiri vizuri unahitaji kuwa makini na inputs unazozipata kupitia vitu unavyovisoma, unavyovisikiliza au unavyovitazama. Kupitia hizi inputs unaweza kunote vile vitu ambavyo unaona ni mawazo yanayoweza kukusogeza hatua moja mbele
5. Unapofikiri wazo vema linahitaji hatua moja zaidi ya kuliboresha kwa kujaribu kulifanyia uchunguzi wa kina kuweza kuona namna ambavyo linaweza kwenda katika uhalisia wa kutekelezeka
6. Unapokuwa na wazo sahihi, unatakiwa uwashirikishe watu sahihi kwa ajili ya wazo husika, wazo pia lazima lishirikishwe katika mazingira sahihi, muda pia unatakiwa uwe sahihi kwa ajili ya wazo hilo, na sababu ni lazima iwe sahihi, hakuna namna ambavyo hilo wazo halitakuwa kubwa zaidi na kutoa matokeo sahihi
7. Ili kuweza kujifunza na kukua kwa mafanikio inatakiwa kujua maswali ambayo utawauliza watu wanaojua vitu vingi kuliko wewe unavyovifahamu na pia namna ya kuweka katika matendo yale majibu wanayokupatia katika maisha yako
8. Ni vizuri kuwa na agenda kabla ya maongezi na mtu yoyote itakusaidia kuyaongoza maongezi katika kujifunza kwa kina
9. Namna nzuri ya kuamua vipaumbele:
a) Kuelekeza nguvu zako katika vitu ambavyo vitatumia kwa ubora zaidi strengths zako na vipaji alivyokuzawadia Mungu
b) Kufanya vitu ambavyo vinakupatia matokeo makubwa na tuzo/malipo makubwa
c) Wekeza asilimia 80 ya juhudi zako katika asilimia 20 ya kazi zenye umuhimu zaidi
d) Kuelekeza umakini katika fursa za kipekee zenye matokeo makubwa mno
10. Unapofikiri kwa umakini (focused thinking) inakusaidia pia kutambua ndoto yako katika maisha ikiwa hujaweza kuitambua
11. Jitahidi kuwa na ubora sana katika vitu vichache kuliko kuwa na utendaji bora katika vitu vingi
(Strive for excellence in a few things rather than a good performance in many)
12. Namna ya kujizuia na vitu vinavyoweza kuondoa umakini katika shughuli unayoitenda:
a) Dumisha nidhamu ya kuzingatia vipaumbele vyako
b) Jizuie na vitu vinavyokuletea usumbufu
13. Kuna thamani kubwa sana katika kuunganisha wazo moja na wazo jingine haswa pale ambapo mawazo yanayounganishwa hayahusiani
14. Ubunifu ni uwezo wa kuona kila kitu ambacho kila mmoja amekiona, kufikiri tofauti ambavyo hakuna aliyefikiri hivyo na kutenda tofauti na ambavyo hakuna aliyetenda hivyo
15. Tumaini sio mkakati
16. Ukiwa na tumaini pekee inamaanisha kufanikiwa kwako kuko nje ya uwezo wako
17. Mabadiliko pekee hayawezi kuleta ukuaji, ila pia ukuaji hauwezi kutokea bila mabadiliko
18. Ukweli utakuweka huru, ingawa kwanza utakufanya ukasirike
19. Unahitaji kuitazama kiuhalisia ndoto yako ili kujua vitu vinavyohitajika ili kuweza kuikamilisha/kuifanikisha
20. Maswali muhimu ya kujiuliza unapounda mpango mkakati:
a) Kitu kinachofuata kufanywa na kwa nini?
b) Nani anawajibika kwa ajili ya kitu gani? Na nani anawajibika lwa nani?
c) Nini makisio yetu ya mapato na matumizi?
d) Je tupo katika lengo?
e) He tunafanikiwa kupata ubora tunaotazamia na mahitaji yetu?
f) Je tunawezaje kuwa na utendaji bora zaidi na ufanisi zaidi katika kuelekea kulifanikisha jambo kiuhalisia?
21. Ni vizuri kuoanisha/kulinganisha kati ya mkakati na tatizo husika linalotafutiwa ufumbuzi
22. Mwongozo unaohitaji katika kutengeneza na kutekeleza mipango ya kukuwezesha kufikia malengo yako:
a) Vunjavunja suala husika katika vipengele vidogo vinavyoweza kusimamiwa. Kuvunjwavunjwa kwa suala kunaweza kufanyika kwa kutegemea ratiba, kusudi, kazi (function), wajibu au kwa mbinu/njia nyingine
b) Jiulize kwa nini kabla ya kujiuliza jinsi/namna gani. Inasaidia kukupatia sababu kwa ajili ya maamuzi yako. Itafungua akili yako kwa ajili ya uwezekano na fursa. Ukubwa wa fursa unaamua kiwango cha rasilimali na jitihada unayohitaji kuwekeza.
c) Kusanya taarifa za kutosheleza zinazofafanua suala husika katika uhalisia wake.
d) Fanya mahesabu kuhusu rasilimali ulizonazo. Una muda kiasi gani? Una fedha kiasi gani? Una vifaa gani? Una mali gani nyingine?
Madeni au wajibu gani utakaojitokeza? Watu gani wanaohitajika kuunda timu ili kuweza kukamilisha lengo?
e) Unapoanza kutengeneza mpango anza na masuala yaliyo dhahiri/wazi
f) Kuwa na watu sahihi katika sehemu/mahali sahihi
23. Jifunze kutafakari kwa ajili ya kujifunza kutoka katika mafanikio na kushindwa kwako kulikotangulia, gundua kipi unatakiwa kujaribu kurudia, na amua kipi unatakiwa kubadilisha
24. Adui mkubwa wa mafanikio yako ya kesho ni mafanikio yako ya leo
25. Watu wengi sana wameridhishwa na matatizo ya zamani kuliko nia ya kutafuta ufumbuzi mpya
26. Awamu tatu za maisha:
a) Moja ya tatu ya kwanza inakwenda katika elimu  (Education)
b) Moja ya tatu ya pili katika kutengeneza ujuzi na maisha (Building Career and Making Living)
c) Moja ya tatu ya mwisho ni kwa kujitolea kwa shukrani (Returning something in gratitude)
27. Maswali mawili ya kutathmini nia yako:
a) Unapoamka asubuhi jiulize ni kitu gani chema/kizuri unaenda kufanya leo?
b) Unapoenda kulala jiulize ni kitu gani chema/kizuri umekifanya leo?
Rafiki unaweza kuwashirikisha wengine kuhusu blogu hii kwa ajili ya kupata maarifa mbalimbali na pia unaweza kubofya hapa ili kuweza kupata makala kila inapowekwa kupitia barua pepe yako.
Goodluck Moshi
Author
StadizaMafanikio

Sunday 13 November 2016

Namna ya Kutambua Dalili Za Kushindwa

Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio!
Rafiki gari linapopelekwa kwa fundi kwa ajili ya kutatua tatizo lililo nalo, litaweza kutatuliwa ikiwa tuu kisababishi cha tatizo husika kimefahamika . Ila pia ukienda kwa daktari wa binadamu ukiwa dhaifu , ataweza kukupatia matibabu sahihi baada ya kugundua dalili za tatizo husika. 



Kwa upande mwingine katika maisha yetu unaweza kuwa unashindwa katika kila kitu unachofanya na ukakosa mtu wa kukusaidia kuvuka hiyo hali kwa sababu tuu ya kutoa visingizio (excuse) au sababu zilizokusababishwa ushindwe.
Mambo haya yanaweza kuwa yanaumiza lakini ni bora na sahihi kufahamu ukweli ambao umekuwa hujui na namna ambavyo unaathiri fursa yako ya kufanikiwa.
Soma Makala Hii Inayohusiana : Jinsi Ya Kuishinda Hofu Uliyonayo
Kufanya jambo chini ya uwezo ulionao au kufanya tofauti na mpango uliokuwa umejiwekea ni moja ya dalili itakayokupelekea. kushindwa. Hali hii inachangiwa sawa na kujidanganya kwa kukubali maoni ya marafiki au mambo ambayo umeshafanikiwa kuyapata.
Ili kuweza kuepuka hali hii hakikisha unafanya jambo lolote kwa uwezo wako wote na kuzingatia mpango uliouweka katika kufanikisha jambo husika.
Kufanya jambo kana kwamba una muda wa miaka elfu ya kuishi ni dalili nyingine itakayokupelekea kushindwa. Na hapa utakuta kwa chochote unachofanya utakuta unafanya kama vile unayo masaa yakutosha au wakati mwingine unatumia muda wako muhimu katika mambo muhimu bila kujali kuwa muda upo na ukomo.
Ili kuweza kuepuka hali hii hakikisha unatumia muda wako vizuri kwa kuchagua kufanya yale mambo muhimu ambayo yatachangia katika kukusogeza hatua ya kutimiza malengo yako, na epuka kufanya mambo yasiyo ya msingi.
Kukubali kuchukua jambo ambalo unajua linazidi uwezo wako wa kulitenda ni dalili nyingine itakayokupelekea kushindwa. Sababu ujuzi na maarifa uliyonayo hayakidhi uwezo wa kulibeba jambo. Hivyo hata kama utalichukua ujue utafanya chini ya kiwango au utafanya bila mafanikio.
Ili kuweza kuepuka hali hii ikiwa umechukua jambo linalozidi uwezo wako hakikisha una mpango mkakati wa kukuwezesha kupandisha uwezo wako wa kimaarifa na kiujuzi utakaoweza kuhimili ukubwa wa jambo unapokwenda.
Rafiki unaweza kuwashirikisha wengine kuhusu blogu hii kwa ajili ya kupata maarifa mbalimbali na pia unaweza kubofya hapa ili kuweza kupata makala kila inapowekwa kupitia barua pepe yako.
Goodluck Moshi
Author
StadizaMafanikio

Saturday 12 November 2016

Uchambuzi wa Kitabu cha " GETTING RESULTS THE AGILE"

Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio!
J.D Meier ni mwandishi wa kitabu cha GETTING RESULTS THE AGILE WAY. Mwandishi katika kitabu hiki anatueleza mfumo wenye nguvu ya kukupatia matokeo katika kazi na maisha. Na mwandishi anazidi kusisitiza kuwa siri kubwa ya kupata matokeo imefichwa katika uwezo wa kuendana na mabadiliko. 





Rafiki hapa nakushirikisha mambo muhimu ambayo nimejifunza katika kitabu hiki:
1. Uwezo wetu wa kupokea mabadiliko inaamua kuhusu kiwango cha mafanikio
2. Ni muhimu kujenga uwezo wa kutawala mabadiliko na siyo mabadiliko yakutawale na kukuendesha
3. Unapokutana na changamoto ambazo zimekuzidi uwezo , ujuzi hata maarifa , njia ya pekee ya kushinda ni kujifunza mifumo ambayo wanatumia wengine katika kuleta matokeo kwao nawe unatumia njia hiyo
4. Ni vizuri kuwa na uwajibikaji kuhusiana na muda wako, weka mipaka kuhusiana na muda ambao unaweza kuuutumia kuhusiana na jambo fulani, weka vipaumbele na focus katika mambo kadhaa
5. Ni vizuri kuamua jinsi ya kudhibiti taarifa unazozipata kuna taarifa nyingine ni za kupokea na kuzitupilia mbali , si taarifa zote unahitaji kuzibeba na kuendelea nazo
6. Ni muhimu kujifunza namna ya kusimamia miradi itakuwezesha kulivunjavunja tatizo kubwa kuwa dogo dogo na kukusaidia kupata matokeo ndani ya muda husika
7. Mambo mengi tunajifunza shuleni na kazini , lakini ni mambo machache tunajifunza kwa muda mfupi ambayo yanabadilisha maisha yetu
8. Ni muhimu kujua thamani gani unaitoa katika kile unachofanya kuliko kufanya kwa lengo la kukamilisha tuu uonekane umemaliza shughuli husika
9. Ni vema kuwa na mipaka ya muda, nguvu ambayo unayoweza kuwekeza katika shughuli fulani na siyo kufanya tuu ili kuonekana umefanya maana unaweza kupoteza muda na nguvu nyingi katika shughuli bila kuwa na uangalizi. Kuwa na mipaka kunakusaidia kuwa na mlinganyo katika maisha
10. Kujua kipimio chako cha mafanikio kunakusaidia kuweka vipaumbele katika yale unayoyafanya
11. Ni muhimu njia unayotumia kufanikisha jambo lako iwe inaendana na misingi yako ila pia ni njia inayoaminika na inayoweza kutumiwa na yoyote na kutoa majibu yale yale, na pia ni njia ambayo inaweza kuboreshwa na pia ni njia ambayo inaongeza ufanisi wako na inapunguza udhaifu wako
12. Ili kuweza kujifunza zaidi unahitaji kufanya tathmini ya kila wiki kipi ambacho kinafanya kazi kwako, uimara wako, udhaifu wako, yale ambayo hayafanyi kazi kwako achana nayo tafuta namna mpya ambayo itakusaidia kupata matokeo bora zaidi
13. Ili kuweza kupata matokeo yanayohitajika ni muhimu kujua jinsi ya kudhibiti muda, nguvu na utumiaji wa mbinu bora za kuifanikisha. Nguvu huamuliwa na shauku uliyonayo katika kukamilisha jambo, na muda unaotumia katika jambo huamuliwa na nguvu uliyonayo ya kulitenda jambo husika
14. Kanuni ya 3
Hapa unaamua kuhakikisha unakamilisha mambo matatu tu katika mwaka, mwezi, wiki hata siku hii inakusaidia kuweka kipaumbele na mipaka ya vitu unavyotaka kuvipata ndani ya muda fulani
15. Kila wiki ni mwanzo mpya, hakikisha kila jumatatu unakuwa na maono ya Wiki, matokeo ya kila siku na kufanya tathmini kila ijumaa kuhusiana na matokeo matatu ambayo unayalenga kuyapata
16. Katika yale unayofanya ni muhimu kuwa na mwendelezo katika kutoa thamani sawasawa na jinsi unavyokua au unavyoongezeka kutokana na shughuli zako
Rafiki unaweza kuwashirikisha wengine kuhusu blogu hii kwa ajili ya kupata maarifa mbalimbali na pia unaweza kubofya hapa ili kuweza kupata makala kila inapowekwa kupitia barua pepe yako.
Goodluck Moshi
Author
StadizaMafanikio

Friday 11 November 2016

Jinsi Ya Kuishinda Hofu Uliyonayo

Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio!
Rafiki katika maisha watu wamekuwa wakitawaliwa na hofu, wameipa hofu nafasi kubwa ya kutawala maisha yao. Hofu huzaa malalamiko kunakosababishwa na hali ya kutoridhika na hatua au hali uliyonayo. Lakini ukifanya ulinganisho kati ya vile ulivyonavyo na walivyonavyo wengine,utagundua unahitaji kuwa na moyo wa shukrani.



Utafiti unaonesha asilimia tisini ya mambo au vitu katika maisha yetu ni sahihi au sawa (right), wakati asilimia kumi ya mambo au vitu katika maisha ndiyo haviko sahihi (wrong). Ikiwa unataka kuwa na furaha hakikisha unaegemea zaidi katika upande wa mambo yaliyo sahihi (asilimia tisini) kuliko yasiyo sahihi (asilimia kumi). Na ikiwa unataka kuishi maisha ya masikitiko au huzuni hakikisha unachagua kuegemea zaidi katika upande wa mambo yasiyo sahihi (asilimia kumi) kuliko yaliyo sahihi (asilimia tisini).
Ni mara chache sana tunatumia wakati kufikiri yale ambayo tunayo, badala yake utakuta  tunawaza kuhusu yale ambayo hatuna. Usilalamike kama vile upo wewe peke yako ndiye mwenye matatizo au ambaye hana. Ukichunguza utagundua una mambo mengi sana ya kukufanya uwe na shukrani kutokana na kuwa na upekee hasa ukilinganisha na wengine ambao hawana vitu ulivyonavyo. Hapa rafiki ninapenda kukusisitiza kuamua kwa kukusudia kuangalia upande wa uzuri kuliko upande wa ubaya wa kila tukio linalokuja katika maisha yako.
Rafiki napenda kusisitiza usihesabu idadi ya matatizo uliyonayo anza kuhesabu mambo mazuri uliyonayo, hii itakusaidia kuondoa hofu ya kuishi.
Rafiki unaweza kuwashirikisha wengine kuhusu blogu hii kwa ajili ya kupata maarifa mbalimbali na pia unaweza kubofya hapa ili kuweza kupata makala kila inapowekwa kupitia barua pepe yako.
Goodluck Moshi
Author
StadizaMafanikio

Thursday 10 November 2016

Mambo Matano (05) Yaliyojificha Katika Mafanikio Yako

Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio!
Rafiki watu wengi wamekuwa wakipima mafanikio kwa kiwango cha vitu vinavyomilikiwa na mhusika. Kutokana na hili kunakuwa na maana mbalimbali kwa kila mtu kuhusu mafanikio. Leo ninapenda kukushirikisha mambo ambayo utayakuta katika kila mafanikio.



(a) Lengo
Kutokuwa na lengo ni adui mbaya sana wa mafanikio. Chochote unachofanya kinakuongoza kuelekea katika kutimiza lengo fulani. Ni muhimu kuwepo kwa lengo sababu litasababisha uwe kwanza  na nguvu ya kukusukuma na pili uwe na fikra za ubunifu ambazo zinakupeleka hatua fulani ya kufikia lengo. Lakini pia kunakuwa na hali ya kuridhika wakati upo katika mchakato wa kufikia lengo.
(b) Safari ya mafanikio ina kupanda na kushuka.Siku zote au vipindi vyote haviwezi kufanana. Kuna vipindi vitafika utakuwa unakutana na hali ya kushindwa ,hii isiwe sababu ya wewe kuamua kuchoka na kukata tamaa bali ni ushahidi kuwa mafanikio yanahitaji juhudi au bidii , na mafanikio siyo rahisi kama unavyofikiri. Na mtu yoyote ambaye hataki kupokea vipindi vya kushindwa katika safari yake hayuko tayari kupambana ili kuweza kuonja ladha ya mafanikio.
Ukiweza kushinda hali hii, utakuwa umeishinda hali ya kufanya mambo kwa kawaida (mediocre) , utajenga ujasiri, na utaongeza uwezo wako wa kupokea (absorb) kushindwa.
(c) Gharama
Hakuna mafanikio ambayo utayapata bure. Furaha ya mafanikio imo ndani ya jitihada iliyowekwa kufikia mafanikio.Gharama na mafanikio ni vitu ambavyo vinakwenda pamoja au sambamba hauwezi kuvitenganisha.
(d) Kuridhika
Mafanikio ni muhimu yakufanye upate furaha ya ndani (inner joy au satisfaction). Mtazamo imewekwa sana kupima mafanikio kwa kiwango cha vitu vinavyomilikiwa. Ikiwa hata mafanikio yamefikiwa kwa machozi ni muhimu yavishwe yako la furaha inayotoka ndani yaani kuridhishwa na hatua uliyofikia, na hii inasaidia kutambua kiwango cha jitihada kilichokufikisha katika ngazi ya mafanikio husika.
(e) Imani
Kwa wewe kuwepo hapa duniani kuna kusudi maalum ambalo aliyekuumba anataka ulitimize hapa duniani. Ni muhimu ufahamu mafanikio unayoyapata pia yanaletwa na kusababishwa na uwepo wa aliyekuumba katika kuyapata mafanikio. Kwa kutegemeana na imani yako ni muhimu kutambua uhusiano huo uliopo kati ya maisha yako au malengo makubwa ya maisha yako (greater purpose) na mwandishi wa hayo malengo (author of greater purpose au maker).
Kama ambavyo alama za vidole (finger prints) zilivyo pekee kwa kila mtu haziwezi kufanana na mtu mwingine yoyote, basi mafanikio pia kwa kila mtu yako pekee. Tunachohitaji ni ujasiri wa kufanikiwa na kuwa vile ambavyo tumekusudiwa na aliyetuumba kuyafikia mafanikio.
Rafiki unaweza kuwashirikisha wengine kuhusu blogu hii kwa ajili ya kupata maarifa mbalimbali na pia unaweza kubofya hapa ili kuweza kupata makala kila inapowekwa kupitia barua pepe yako.
Goodluck Moshi
Author
StadizaMafanikio

Wednesday 9 November 2016

Hatua Zitakazokusaidia Kukabili Changamoto Zinazokuzuia Kupata Mafanikio

Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio!

Rafiki unahitaji kufahamu haitatokea kuwepo kwa mtu ambaye ataishi au atapata mafanikio kwa ajili yako au kwa niaba yako. Mambo yote ambayo unayohitaji iwe ni mafanikio au vitu, unahitaji kuwajibika kuvitafuta kwa ajili yako binafsi.



Utakuwa unafanya makosa makubwa sana ikiwa utaamua kuridhika na hali uliyo nayo na kukubali kuwa dunia ndiyo itaweka jitihada kwa ajili ya kuboresha hali yako.Unahitaji kuweka jitihada binafsi ili kubadili hali uliyonayo au unayoipitia kwa sasa.


Soma Makala Hii Inayohusiana: Jambo Moja la Kuzingatia Ili Kuwa Tajiri


Tumaini kubwa ambalo unahitaji kulijua bila kujali umeathiriwa kwa kiwango gani na changamoto, bado unayo nafasi ya kuamua kujifunza jinsi ya kuinuka kutoka katika hizo changamoto, kusimama tena na kusonga mbele.

Kitendo cha kuinuka na kusonga mbele kinabeba kwanza ujumbe wa kujitegemea (self reliance au independence). Na hii ni moja ya kiungo muhimu sana ambacho kitakusaidia kutoka zaidi ya maeneo yako uliyoyazoea (comfort zone). Lakini pia  hii itachangia kujua ukomo wa uwezo wako na kupata watu wengine ambao wataungana na wewe kukusaidia (dependence) kutokea pale ulipoishia kulikosababishwa na uwezo wa juhudi zako.

Utapata hamasa ya kutafuta majibu ya maswali mengi sana ambayo utakutana nayo, lakini rafiki suala la kutafuta majibu ni sawa na kufanya hitimisho (conclusion), badala yake unashauriwa uulize maswali zaidi, kitendo cha kuuliza maswali kinasaidia kukusanya taarifa zaidi (facts) , ambazo pia zitakusaidia kupata sababu ya majibu au hitimisho kuwa vile lilivyo.

Rafiki ili kuweza kupangilia vizuri maisha yako ya baadae ni muhimu kutazama maisha yako miaka ya nyuma yathamini,yakubali , shukuru kwa ajili ya mafunzo yaliyokupatia na kusonga mbele.

Rafiki unaweza kuwashirikisha wengine kuhusu blogu hii kwa ajili ya kupata maarifa mbalimbali na pia unaweza kubofya hapa ili kuweza kupata makala kila inapowekwa kupitia barua pepe yako.

Goodluck Moshi
Author
StadizaMafanikio

Tuesday 8 November 2016

Vigezo Vitatu (03) Vya Kuzingatia Kabla ya Kupublish Makala Katika Blogu

Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio!

Rafiki kwa kila msomaji ambaye amechagua kutembelea blogu yako hakika ni fursa ya kipekee mno kwako, kwa sababu kwanza kati ya masaa 24 aliyonayo katika siku ameamua kutenga sehemu ya muda  kupata maarifa kupitia blogu yako, lakini pili ni kuwa kati ya blogu nyingi ambazo angeweza kwenda kutembelea ameamua kuchagua blogu yako kwa ajili ya kupata maarifa.



Katika makala ya leo ninapenda kukushirikisha vigezo vitatu ambavyo unapaswa kuhakikisha unazingatia kabla ya kuiweka hewani (publish) makala yoyote unayoandika katika blogu yako.



(a) Utofauti au upekee (distinction)
Hii ni thamani au kigezo namba moja ambacho kila makala unayoandika hakikisha imebeba. Tengeneza mikakati na malengo maalum ya kuhakikisha kazi yako inakidhi kigezo hiki. Fanya homework ya kutosha kutembelea waandishi wengine na kujifunza mambo kama vile wanaandika nini, wanatumia staili gani ya uandishi na kadhalika.
Usishawishike na kukopi makala au aina ya uandishi wa mwandishi mwingine kwa kuwa tayari ana wasomaji wengi, bali angalia namna ambavyo unaleta kitu kipya ambacho wasomaji wamekuwa hawakipati (tafuta pengo au gap).
Upekee katika uandishi wako ndiyo silaha pekee ambayo itatofautisha makala zako na za waandishi wengine zinapowekwa pamoja.

(b) Ubora (Excellence)
Hii ni thamani au kigezo namba mbili ambacho kila makala unayoandika hakikisha imebeba. Hakikisha unaweka jitihada kubwa ya kutosheleza kutoa kilichobora mno ndani yako ,penda makala unazoandika na wasomaji wako kwa kuzifanya  kuwa bora kuliko makala zako zilizotangulia au makala za waandishi wengine.
Kiwango cha ubora kinatakiwa kupanda siku hadi siku, kamwe usiridhike kutokana na idadi ya mashabiki au wasomaji wako kupitia mrejesho wanaokupatia. Hii ni mbinu pekee itakayokusaidia kuendelea kubaki na wasomaji kutokana na kuwa na uboreshaji endelevu au usio na kikomo. Usibaki na kitu ndani yako (die empty).

(c) Huduma (World - Class Service)
Hii ni thamani au kigezo namba tatu ambacho kila makala unayoandika hakikisha imebeba pia. Makala unayoandika hakikisha inamuhudumia msomaji katika kiwango sawasawa na mahitaji yake au kupitiliza mahitaji yake lakini isiwe kiwango cha chini kuliko mahitaji yake. Kupitia maandishi unayoandika hakikisha yana mtiririko mzuri, hayana makosa ya uandishi (grammar), umetumia lugha rahisi inayoeleweka kwa msomaji ili kumwezesha kupata maarifa ambayo yatachangia kuboresha maisha yake. Akili na moyo ujikite (focus) katika kile unachoandika kama fursa ya kuhudumia wasomaji .Na hakikisha unatumia fursa vizuri kwa kufanya kilicho sahihi kwa msomaji.
Mambo haya matatu ni muhimu yaende kwa pamoja bila kuacha lolote.

Soma Makala Hii Inayohusiana: Kanuni Kumi (10) za Huduma Bora Kwa Mteja

Rafiki unaweza kuwashirikisha wengine kuhusu blogu hii kwa ajili ya kupata maarifa mbalimbali na pia unaweza kubofya hapa ili kuweza kupata makala kila inapowekwa kupitia barua pepe yako.

Goodluck Moshi
Author
StadizaMafanikio

Monday 7 November 2016

Dondoo Tatu (03) Zitakazokusaidia Kupata Mada za Kuandika Katika Blogu

Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio!



Rafiki kati ya maswali yanayoulizwa na waandishi wanaanza kuandika (beginners) ni mada gani waichague kuandika makala katika blogu. Lakini pia kwa wale ambao wameanza kuandika huwa wanajiuliza nijikite katika mada gani katika kuendelea kuandika makala katika blogu.
Katika makala hii napenda kukushirikisha maeneo matatu ambayo tunakutana nayo au tumeshakutana nayo (common) lakini tumekuwa hatuyapi kipaumbele au kuwa na mtazamo wa kupata mada za kuandika katika blogu zetu.

Soma Makala Hii Inayohusiana; Hatua Nne (04) Katika Uandishi wa Blogu

(a) Andika kuhusu mada unayopenda kujifunza.
Kwa mfano ukikuta unapenda kusoma au kununua vitabu vya masuala ya mafanikio, basi fahamu hilo ni eneo mojawapo ambalo unaweza kuandika. Pia ikiwa una mtu ambaye ni mtaalamu wa kada fulani unayependa kumuuliza maswali kwa ajili ya kujifunza , basi fahamu hilo ni eneo lingine pia unaweza kuandika.
Rafiki ukiyaandika haya ambayo unajifunza unakuwa umewasaidia wengine kupata maarifa ambayo umejifunza.
(b) Andika kuhusu mambo unayopenda kufanya
Ukitafakari miaka yako mitano iliyopita, utagundua kuna kitu au vitu fulani umekuwa unapenda kuvifanya. Katika vitu hivi utagundua kuna mambo umekuwa ukiyafanya yakisukumwa na shauku ya wewe kuyafanya.
Rafiki unaweza ukayaona haya mambo ni ya kawaida kwako, lakini kuna watu ambao wanashauku na wanapenda kufanya mambo sawasawa na wewe ulivyoyafanya lakini hawana watu wa kuwasaidia kuwaongoza, ukiyaandika utakuwa umewasaidia kuwa role model wao kupitia yale unayoyaandika.
(c) Andika kuhusu mambo uliyopitia katika maisha yako
Kutokana na sehemu ulizoishi au sehemu ulizofanya kazi kuna uzoefu ambao  umekuwa ukiujenga hatua kwa hatua, siku hadi siku. Uzoefu huu ni hazina kubwa ambao unaweza kuwasaidia wale ambao wanaanza katika maeneo hayo.
Rafiki mambo haya uliyoyapitia katika maisha unaweza kuandika ili kuwasaidia waweze kuepuka makosa ambayo wewe uliyafanya  lakini pia waweze kutumia muda mfupi zaidi kuliko ambao uliuutumia kutokana na kukosa kocha wa kukusaidia.
Rafiki unaweza kuwashirikisha wengine kuhusu blogu hii kwa ajili ya kupata maarifa mbalimbali na pia unaweza kubofya hapa ili kuweza kupata makala kila inapowekwa kupitia barua pepe yako.

Sunday 6 November 2016

Uchambuzi wa Kitabu cha " SUCCESS SECRETS OF THREE TIME OLYMPIAN"

Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio!




Ruben Gonzalez ni mwandishi wa kitabu "SUCCESS SECRETS OF THREE TIME OLYMPIAN" . Katika kitabu hiki ameeleza mambo ambayo amekuwa akiyafuatilia na kujifunza kutoka kwa watu waliofanikiwa. Baada ya kujifunza alianzia  kuweka katika matendo yale ambayo alijifunza kutoka kwa watu waliofanikiwa, na hatimaye kanuni au mbinu zile zile zilimsaidia kufanikiwa pia. Hapa ni nakushirikisha mbinu au kanuni ambayo Ruben ameyaleeza.
1. Fanya maamuzi leo ya kuwa mwanamafanikio kwa kuwa tayari/nia ya kulipa gharama inayohitajika ili kuweza kufikia ndoto yako
2. Mafanikio hayapimwi na hatua uliyofikia leo bali hupimwa na vizuizi ambavyo umevivuka mpaka kufikia mafanikio
3. Watu waliofanikiwa hujiandaa na kujiweka katika nafasi sahihi kuweza kutumia fursa yoyote ambayo inaweza kujitokeza kuwasaidia katika safari ya mafanikio
4. Mtazamo wako juu ya jambo fulani unaamua kiwango chako cha kufanikiwa, kufikiri chanya kunakupa njia nyingi za kuweza kukusaidia kufanikiwa
5. Jipe nafasi ya kujifunza ujuzi, maarifa yanayoweza kukufikisha kupata ndoto zako
6. Iruhusu sheria ya wastani ifanye kazi katika maisha yako, kwa kadiri unavyoshindwa katika jambo fulani unapata mafunzo mengi ambayo yatakusaidia kufanikiwa kutokana na kujaribu njia nyingi za kufanikiwa
7. Unahitaji kujiamini wewe mwenyewe na kuamini kuwa utafikia ndoto yako.
8. Unapokuwa na mtazamo wa kuwa na utayari wa kufanya lolote linalokuhitaji bila kujali muda utakaoutumia ili kufikia mafanikio basi   kufanikiwa ni suala ambalo la kitambo kidogo
9. Vinaweza vikachakuliwa vitu vyote katika maisha yako ukabaki hauna kitu lakini kitu kimoja hubaki na wewe muda wote ni nguvu ya kuchagua, chagua leo namna unavyoitikia (react) katika hali yoyote inayokutokea
10. Daima weka malengo yako mbele yako
11. Fikiria mawazo ambayo yatakuhamasisha kufikia malengo kwa kuwa like unachokifikiria muda wote ndicho kitakachokutokea katika uhalisia
12. Kila kitu hutokea kwa sababu, changamoto tunazopata katika safari ya mafanikio ni kwa ajili ya kutupatia masomo makubwa ya kujifunza ili kuweza kuwa na uuanzaji sahihi katika jambo tunalofanya na pia kuweza kufikia mafanikio
13. Unahitaji kuwekeza nguvu zako katika lengo moja mpaka ufanikiwe ndio uelekeze nguvu zako katika lengo lingine mpaka malengo yako yote yaishe/yakamilike, usielekeze nguvu katika lengo zaidi ya moja kwa kuwa kiwango cha kufanikiwa kitapungua
14. Ujasiri hutokana na muda ambao umewekeza katika masaa, siku ili kujijengea maarifa na ujuzi wa kuwa bora katika fani unayoifanya
15. Changamoto kubwa kuliko zote kuelekea kufanikiwa ni kujitawala mwenyewe, utashawishika kufanya vitu ambavyo vitakuweka nje ya mstari wa Mafanikio, lakini siku zote katika Yale unayofanya jiulize swali moja kuwa je unachokifanya kinakusaidia kukusogeza Karibu na kufanikiwa
16. Jifunze masuala ya uongozi na uwasaidie wengine kwa kuwajenga kiujuzi ili waweze kuwa na ujasiri wa kuungana na timu yako ili kuweza kukusaidia kufikia mafanikio yako
17. Ujasiri katika kufanikiwa hutokana na utayari wa kuweka mambo katika matendo na kuvumilia.
18. Bila kujali shida unayoipata ni ya namna gani jifunze kuiongelesha na kuiambia kuwa wewe ni mkubwa mno kuliko hiyo shida na haitaweza kukushinda
19. Kila Mafanikio makubwa ni mjumuisho wa mafanikio madogo madogo
20. Jifunze kutokana na makosa yako, fanya marekebisho yanayohitajika alafu jiweke katika nafasi sahihi ya kutumia fursa inayokuja mbele yako
21. Shauku yako ya kufanikiwa itakupa nguvu ya kukusaidia usiachie njiani unachokihitaji na pia itakupa njia za kuweza kufanya ili ufanikiwe
22. Fanya zaidi ya kile kinachotarajiwa
23. Ukiamini kuwa unachokitaka kuwa kinawezekana na ukatenda mambo ambayo yanasaidia kukfanikisha unachotaka, ulimwengu nao utakusaidia kufanya ndoto, mipango na matarajio yako katika uhalisia
24. Tumaini hutuonyesha vile visivyoonekana na kutupatia vile visivyowezekana
25. Usiruhusu hofu ikutawale, hofu inatawaliwa kwa kutenda yale unayoyahofia
26. Usijudge siku kwa mavuno uliyoyapata bali judge kwa mbegu uliyootesha/uliyopanda
27. Ulimwengu daima humpatia mtu fursa ya kufanikiwa ikiwa maneno na matendo yake yanaonesha anajua anapoelekea
28. Kila siku kitu cha kwanza andika malengo yako
29. Amua kuwa mwanafunzi wa kudumu wa mafanikio
30. Vitabu unavyosoma na watu unaokutana nao vinaamua wapi utakuwa miaka mitano ijayo
31. Furaha ni zao la mambo matatu:
a) ubora wa mahusiano na watu wako muhimu
b) kiwango cha kudhibiti hisia zako
c) kutumia vipawa vyako kufikia malengo yako
32. Haijalishi unaanguka mara ngapi katika safari ya Mafanikio simama endelea na safari
33. Watu waliofanikiwa wanawekeza muda wao kutafuta njia za kufanikiwa zaidi
34. Fall in love with the process of making you succeed
35. Tafuta watu ambao wana ujuzi na rasilimali ambazo unahitaji ili kuweza kufikia mafanikio unayoyahitaji
36. Tafuta mshauri au kocha ambaye ataharakisha mafanikio yako
37. Leaders make decision all time. Followers make suggestions.
38. Kama unapitia mapambano katika maisha , unaandaliwa kwa ajili ya malengo makubwa na muhimu
39. Viongozi wapo tayari kufanya lolote linatakiwa kufanywa na wao ili kuboresha matokeo
40. Hauwezi kufanikiwa kupata kitu kikubwa katika maisha mpaka utakapoanza kuamini kuwa kuna kitu kikubwa ndani yako kuliko hali au mazingira unayoikabili
Rafiki unaweza kuwashirikisha wengine kuhusu blogu hii kwa ajili ya kupata maarifa mbalimbali na pia unaweza kubofya hapa ili kuweza kupata makala kila inapowekwa kupitia barua pepe yako.

Saturday 5 November 2016

Uchambuzi wa Kitabu The Top Ten Distinctions Between Winners and Whiners

Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio!



Keith Cameron Smith ni mwandishi wa kitabu "THE TOP TEN DISTINCTIONS BETWEEN WINNERS AND WHINERS ". Keith anatushirikisha mbinu ambazo washindi wamekuwa wakizitumia kila mara wanapokuwa wanafanya kazi yoyote ili kuwasaidia kuwapa ushindi. Keith anasisitiza kuwa adui mkubwa anayechangia katika kushindwa ni tabia ya ulalamikaji, hali ya kukataa kuwajibika.
Keith anaamini kwa kusoma kitabu hiki ni njia mojawapo ya kuweza kukushirikisha mambo chanya yatakayochangia katika kukufanya uwe mshindi. Hivyo katika makala napenda kukushirikisha mambo ambayo nimeyapata kutoka katika kitabu hiki.
1. Kuwa mshindi sio tukio linalotokea katika muda mfupi, ni safari ndefu ya maisha
2. Maisha hayakwendi sawa sawa na mipango inasemekana maisha ni vile yanavyokwenda wakati unaendelea kupanga mipango
3. Uwajibikaji ni kufanya kile kilicho bora kwa nafasi yako au uwezo wako ukiwa na imani kuwa utapata matokeo mazuri
4. Ushindi ni mchezo unaohitaji timu na umoja
5. Hofu ni imani ya kuwa kitu kibaya kabisa kitatokea
6. Hofu imejengwa katika mizizi kuwa hauna machaguo
7. Ili uweze kuwa mshindi unahitaji kuwajibika kwa kufanya uchaguzi wa imani chanya zidi ya hofu
8. Washindi hujua kuwa daima wana machaguo na wanawajibika na hayo machaguo
9. Machaguo yanaamua hali, hali haiamui machaguo
10. Ni sahihi kusikitika kuhusu mategemeo fulani lakini si sahihi kukata tamaa
11. Ushindi huanza na mawazo na kuwaibika kufanya machaguo yale yaliyo chanya tuu
12. Washindi wana mtazamo wa mawazo yao ndio mbegu, na akili yao ndio udongo wa kukuzia mbegu, mawazo unayoyaweka katika akili yako huota mizizi na kisha kukua kuwa mti unaozaa matunda, kwa hiyo ni muhimu sana kuchagua ni mawazo ya aina gani unayoyaruhusu kukaa akili mwako
13. Washindi huamini wanawajibika na matokeo wanayoyapata
14.  Kwa kudhibiti mawazo yako unabadilisha matokeo yako, washindi huwajibika kwa matokeo yao kwa kudhibiti mawazo yao
15. Washindi wako tayari kulipia gharama inayohitajika ili waweze kushinda
16. Washindi hujifunza kutoka kwa wale walio bora zaidi yao kufanya vile wanavotakiwa kuvifanya ili kufikia hatua kama za hao walio mbele yao
17. Inawezekana ukajifunza na kupata kile unachotamani kukipata
18. Gharama kubwa washindi wanayolipa ni kupata maarifa
19. Mipaka uliyonayo katika kufanikiwa ni kwa sababu ya kukosa maarifa, waliofanikiwa zaidi yako ni kwa kuwa wana maarifa ambayo hauna na pia wameamua kuweka katika matendo yale maarifa waliyoyapata
20. Gharama nyingine inayolipwa na washindi ni upinzani, washindi hawajali watu wengine wanawafikiriaje bali wanajali wao wenyewe washindi wanajifikiriaje binafsi
21. Washindi hawawasikilizi wapinzani bali wanasikiliza mioyo/nia yao inavowaelekeza
22. Watu hawana muda na maisha yako hata kukufikiria, hata pale mtu anapokuwa mpinzani wako dakika tano baadae hata hana mawazo kuhusu wewe
23. Washindi wako tayari kulipa gharama ya kuwahudumia wengine kwa moyo mmoja kwa sababu kwa kuwahudumia wengine kupata kile wanachokihitaji kunakusaidia kuweza kupata chochote unachohitaji
24. Ongeza maarifa juu ya kile unachokitaka katika maisha yako, wapuuzie wapinzani na wahudumie watu kwa moyo mkunjufu
25. Malipo ya gharama hayatupatii tunachokitaka bali yanatupa fursa ya kukipata ( The payments don't give you what you want they only give you the opportunity to get it)
26. Usiruhusu mtu akuambie nini huwezi kufanya, ukihitaji kitu nenda ulipe gharama unayohitaji ukipate
27. Washindi huamini kuna njia ya kutupeleka katika mafanikio kwa kila jambo
28. Washindi hutazama matokeo wanayoyataka kwa umakini, wakiona hawajapati kama wanavotarajia wanarekebisha matendo yao (actions) hadi waweze kupata matokeo wanayoyahitaji
29. Washindi hulisha imani yao na kuifisha hofu
30. Kwa kawaida maono hutuonesha mwisho wa safari
31. Baadhi ya masomo utakayojifunza wakati was kuelekea mafanikio yako ni kushindwa, kukataliwa na kupoteza vitu.
32. Washindi hawalalamiki bali huthamini maisha. Huthamini kwa kuongea vitu vizuri vilivyotokea awali, vinavyotokea sasa na vitakavyotokea baadaye
33. Changamoto ya mabadiliko katika maisha
Nenda kwa siku kumi mfululizo bila kulalamika, ikiwa utalalamika kabla ya siku kumi hazijaisha bila kujali upo siku ya ngapi utakuwa umefuta zile siku zote ambazo ulifanikiwa kupita bila kulalamika kwa hivyo unatakiwa uanze mpya
34. Unahitaji kuwa msikivu zaidi kuliko unavyoongea, sikiliza kwa lengo la kuelewa unachoambiwa na si kwa lengo la haraka ya kujibu ulichokuwa unaambiwa
35. Kama unapitia wakati mgumu sasa kuna uwezekano mkubwa kuna baraka zilizojificha
Rafiki unaweza kuwashirikisha wengine kuhusu blogu hii kwa ajili ya kupata maarifa mbalimbali na pia unaweza kubofya hapa ili kuweza kupata makala kila inapowekwa kupitia barua pepe yako.