Monday 30 March 2015

Swali la Wiki

Ni kitu gani ungethubutu kukifanya ikiwa kama umehakikishiwa mafanikio kupitia kukifanya hicho kitu?

What would you dare to try to do if you were guaranteed to succeed?

Mambo 3 ya Msingi Kuhusu Malengo

Unapoweka lengo lolote ni muhimu liwe limejengwa katika misingi ya mambo yafuatayo:



Jambo la kwanza:
Lengo liwe linahamasisha (inspiring)

Jambo la pili:
Lengo liwe linaaminika (believable)

Jambo la tatu:
Lengo liwe linalowezekana kufanyiwa kazi (can act on)


Sunday 29 March 2015

Mambo ya Kuzingatia Unaposhirikiana

Unapoamua kushirikiana na mtu mwingine ni vizuri muweke msingi katika masuala 3 yafuatayo ili kuepuka kukatishwa tamaa kwa kutokuwa na ulinganifu wa matarajio na matokeo

Jambo la kwanza:
Fahamu kila mshirika nini atamiliki (own)

Jambo la pili:
Fahamu kila mshirika nini atafanya/wajibu (do)

Jambo la tatu:
Fahamu kila mshirika nini atapata (get)

Remember when expectations exceed outcome, you will arrive at disappointments

Usifanye Kosa Hili Katika Biashara

Unapoamua kuchagua kuwa utashirikiana na mtu mwingine kufanya biashara ya ndoto yako, usitumie kigezo cha huyo mshirika kuwa ni mmoja wa wanafamilia wako au ni mmoja wa marafiki zako wa karibu sana, utakuwa umejiingiza katika matatizo makubwa sana.

Vigezo vya kukuongoza kuchagua inatakiwa viwe; maarifa(knowledge), ujuzi (skills) na uwezo (capabilities) ambao unahitajika kwa ajili ya kusaidia biashara kusonga mbele.

In short s/he must bring something valuable to the table.


Monday 23 March 2015

Fanya Haya ili Ukue

1. Usitamani mambo yangekuwa marahisi, tamani ungekuwa bora mno
Don't wish it were easier; wish you were better

2. Usitamani ungekutana au ungekuwa na matatizo machache,tamani ungekuwa na ujuzi zaidi
Don't wish for less problem; wish for more skills.

3. Usitamani ungekutana na changamoto chache, tamani uwe na hekima zaidi
Don't wish for less challenges; wish for more wisdom.

Tuesday 17 March 2015

Je, Unajua?

Ni bora kufanya kitu kisicho kamili kuliko kutokufanya chochote kisicho na dosari

Better to do something imperfectly than to do nothing flawlessly

Tazama Kushindwa kwa Jicho Hili

Kushindwa hakuamaanishi wewe ndiye uliyeshindwa bali kunamaanisha hujafanikiwa bado

Kushindwa hakumaanishi haukutimiza/haujafanikisha kitu bali kunamaanisha umejifunza kitu

Kushindwa hakumaanishi wewe ni mjinga bali kunamaanisha unayo imani ya kutosha

Kushindwa hakumaanishi umeabika bali kunamaanisha una nia ya kujaribu

Kushindwa hakumaanishi hauna mbinu za kufanya kitu bali kunamaanisha unahitaji kufanya kwa mbinu tofauti

Kushindwa hakumaanishi umepoteza maisha bali kunamaanisha unayo sababu ya kuanza tena

Kushindwa hakumaanishi ukate tamaa bali kunamaanisha kujaribu tena kwa jitihada zaidi

Kushindwa hakumaanishi hautakamilisha bali kunamaanisha jambo unalofanya litachikua muda mrefu

Kushindwa hakumaanishi Mungu amekuacha bali kunamaanisha Mungu ana mawazo mazuri zaidi kwa ajili yako

Hauhitaji kuhofia kushindwa unaweza kuwa mtu unayetaka kuwa

No need to fear failure you can always become a person you want to be

Monday 16 March 2015

Usipuuze Tatizo

Matatizo mengi kamwe hayatatuliwi au hayadhibiti kwa ufanisi kutokana na kutoyapa uzito wa kutosheleza. Hakuna tatizo ambalo halina umuhimu kiasi kuwa hatuhitaji kujali kuhusu hilo tatizo. Mfano kwa mwanafunzi inawezekena hapati A au B lakini anafaulu. Kwa mwanafunzi anaweza akalipuuzia kwa kigezo kuwa hajafeli.

Kamwe usilipuuze tatizo wala usipuuze uwezo wako wa kukabiliana na tatizo. Tambua kuwa tatizo unalokutana nalo kuna mamilioni ya watu duniani wameshapitia tatizo kama hilo. Ukiwa na mtazamo chanya kuhusu tatizo utabadili tatizo na litakupatia uzoefu.

People who approach problems with a positive mental attitude, turn problems into creative experience

Sumu ya Mafanikio

Unapokosa lengo kubwa katika maisha yako kwa kutokujua nini hasa unahitaji na unakipataje, mara nyingi hupelekea kutegemea maoni au ushauri wa watu wengine zaidi katika kuamua kitu cha kufanya kwa ajili ya maisha yako badala ya kujenga msingi katika kutafuta taarifa za kweli zilizo sahihi.

Kwa kutokuwa na taarifa za kweli zilizo sahihi itakupelekea kuahirisha jambo kwa kusema unasubiri mambo yawe mazuri ndiyo uanze kufanya kitu kwa ajili ya maisha yako.

Chukua hatua sasa na anza hapo ulipo kwa kutumia taarifa hizo hizo chache za kweli zilizo sahihi na rasilimali ulizonazo ufanye jambo kwa ajili ya maisha yako na baadae kadiri unavyoendelea utapata njia bora iliyo na ufanisi wa kuleta matokeo mazuri zaidi.

Mbinu za Kustahimili Matatizo

Siri moja kubwa ambayo imewafanya watu waliofanikiwa kuendelea vizuri ni mtazamo juu ya matatizo wanayokutana nayo. Ukizielewa kanuni hizi 6 kuhusu matatizo na kuzifanyia kazi ipasavyo wewe pia utakuwa mshindi.

1. Kila mtu anayo matatizo
(Every living human being has problems)
Usifikiri ukishafanikiwa utakuwa ndio umeyaaga matatizo, kadiri unavyofanikiwa ndivyo matatizo unayatengeneza mapya.
Inawezekana unafikiri ukipata kazi fulani ndo utakuwa umefanikiwa Sana, lakini kumbe unaweza kupata hiyo kazi lakini bosi wako akawa ni mkorofi. Sawa suluhisho unaweza kufikiri ni kujiajiri hapo pia utakutana na matatizo ya kushughulika na wafanyakazi wako ili wazalishe zaidi.
Kubaliana na uhalisia kuwa Hakuna mtu ambaye yuko huru hana matatizo


2. Kila tatizo lina ukomo wake
(Every problem has a limited life span)
Hakuna tatizo ambalo ni la kudumu yaani litakuwepo milele. Muda wa uhai wa tatizo ukiisha litakufa kwa kuisha/kutokuwepo kabisa.


3. Kila tatizo lina fursa
(Every problem holds positive possibilities)
Tatizo linaweza kuwa tatizo kwa mtu mmoja ila kwa mtu mwingine linaweza kuwa fursa. Hospitali zipo kwa sababu watu wanaumwa au wanasheria wapo kwa sababu kuna matatizo ya kisheria


4. Kila tatizo litakubadilisha
(Every problem will change you)
Hakuna tatizo ambalo litakuja katika maisha yetu na kutuacha kama lilivyotukuta. Tatizo litakufanya uamke au uchangamke na usonge mbele


5. Unao uwezo wa kuchagua tatizo likuathiri vipi/kwa kiwango gani
(You can choose what your problem will do to you)
Namna ambavyo unavyorespond tatizo linavyokutokea inaamua pia athari ya tatizo husika kwako.Inawezekana usiwe na uwezo wa kuchagua tatizo linalokutokea lakini unao uwezo wa kuchagua namna unavyorespond


6. Kuna namna chanya na hasi jinsi ya kurespond kwa kila tatizo
(There is a positive and negative reaction to every problem)
Mara zote chagua namna chanya ya kutatua tatizo kuliko namna hasi ya utatuzi wa tatizo. Jambo la msingi ni kuwa kama huwezi kutatua tatizo basi lisimamie kwa ubunifu


When you can't solve the problem, manage it creatively and constructively

Sunday 15 March 2015

Kanuni Inayoamua Wewe Kufanikiwa au Kushindwa

Katika mambo tunayofanya kuna matokeo mawili; aidha kufanikiwa sawasawa na malengo tuliyojiwekea kabla hatujanza kutekeleza jambo au kutokufanikiwa ambapo tunaweza kukuita kushindwa kutokana na kutofikia vigezo tulivyoviweka kuashiria kuwa jambo tumelifanikisha.

Kushindwa (failure) ni makosa madogo madogo katika maamuzi tunayorudia kuyafanya kila siku kuhusiana na jambo husika
(few error in judgment repeated everyday)

Wakati kufanikiwa (success) ni nidhamu au taaluma chache ambazo tunaziweka katika matendo kila siku kuhusiana na jambo husika
(few disciplines practiced everyday)

Kwa hivyo ulimbikizaji wa haya mambo madogo madogo kwa muda mrefu ndiyo hutupelekea kushindwa au kufanikiwa. Usidharau jambo dogo unalolifanya lichunguze kama hilo jambo unalolifanya ukilifanya kwa staili hiyo hiyo kwa muda mrefu litakuweka upande gani wa kushindwa au kufanikiwa? Kisha chukua hatua.

Je, Umepoteza Ujasiri (Confidence)?

Katika jambo lolote unalofanya unahitaji kuwa na ujasiri ili uweze kuwa na nguvu au stamina ya kuweza kulileta katika uhasilia(kulikamilisha) bila kujali vikwazo utakavyokutana navyo njiani.

Zifuatazo ni njia au namna ambavyo unaweza kuujenga ujasiri:

1. Shauku (passion) uliyonayo kulitekeleza jambo husika

2. Fahamu mambo ambayo una uwezo wa kufanya vizuri (strength zone) na uyafanye hayo kwa sababu tu ndiyo mambo ambayo utayafanya vizuri na Acha kufanya mambo usiyo na uwezo wa kuyafanya vizuri (weakness zone) kwa sababu hutayafanya vizuri na hauturuhusu mifumo iliyopo ikusaidie katika hayo maeneo usiyoyaweza

3. Fahamu lengo la wewe kuishi au kusudi ambalo Mungu anataka ulitimize (purpose of life) kwa wewe kuwepo hapa ulimwenguni

4. Unahitaji kuwa na utii (obedience)  kutimiza lile kusudi ambalo Mungu anataka ulitimize kwa wewe kuwepo hapa ulimwenguni

Kwa kifupi ujasiri unazalishwa hivi:

Shauku + Ushupavu + Kusudi + Utii = Ujasiri

au

Passion + Strength + Purpose + Obedience = Confidence

Saturday 14 March 2015

Fahamu Haya Kama Kiongozi

Kwa kila unayemuongoza unahusiana naye kwa kulingana na mojawapo kati ya ngazi hizi tano. Ngazi ya chini kabisa ni ngazi ya kwanza na ngazi ya juu kabisa ni ngazi ya tano:

1. Ngazi ya kwanza ambayo tunaanza nayo katika safari ya uongozi ni kupewa nafasi ya kuongoza (leadership position).
Katika nafasi hii watu walio chini yako wanakufuata kwa sababu ya nafasi yako hawaendi zaidi ya uwezo walionao na muda walio nao.

2. Ngazi ya pili inajengwa katika misingi ya mahusiano (relationship) na wale unaowaongoza. Watu unaowaongoza wanakufuata sio kwa sababu ya nafasi yako ya uongozi kama ngazi ya kwanza bali kwa sababu wanapenda namna unavyohusiana nao katika kuwaongoza. Hapa unakuwa umewapa nafasi ya kukusikiliza, kuona unachofanya na kujifunza.

3. Ngazi ya tatu inajengwa katika misingi ya uzalishaji/ufanisi.
Unaowaongoza watu kwa kuwa mfano katika uzalishaji na ufanisi katika mambo unayoyafanya. Hii itawasaidia kufanya kile wanachokiona na hivyo utakuwa umewavutia kuzalisha na kuweka mkazo katika ufanisi. Hapa ndipo matatizo mengi katika sehemu unayoongoza yanaweza kushughulikiwa.

4. Ngazi ya nne inajengwa katika misingi ya kuwaendeleza wale unaowaongoza ili kuongeza uwezo wao wa ufanisi/uzalishaji (developing people). Na hii itachangiwa kwa kuchagua watu sahihi na kuwaweka sehemu sahihi ambazo zinaendena na uwezo wao

5. Ngazi ya tano inajengwa katika misingi ya heshima. Umefanya mengi yanayowagusa wale unaowaongoza na hivyo kusababisha wakufuate. Wanakufuata kwa sababu ya mambo mengi uliyoyafanya kwa ubora kwa muda mrefu. Hii ni ngazi ya juu kabisa katika uongozi

Unahitaji Wastani wa Maswali 12 Kufanikiwa

Unapofanya maamuzi ya kutaka kufanikiwa unahitaji kufanya mabadiliko ya msingi (fundamental change).Ili kufanya mabadiliko unahitaji namna nzuri ya kuelewa sehemu ambayo unatakiwa kuanzia.

Sehemu iliyo bora kabisa ya kuanza ni kwa kujiuliza maswali. Kwa nini ujiulize maswali? Kwa sababu karibia matatizo ya aina yoyote yanaweza kupatiwa ufumbuzi kwa kuuliza maswali sahihi ya kutosha.

a) Ninahitaji nini?
b) Nini machaguo yangu?
c) Mawazo gani ninayo?
d) Nini wajibu wangu?
e) Nawezaje kuwaza tofauti kuhusu jambo husika?
f) Watu wengine wanafikirije, wanahisije na wanahitaji nini?
g) Kitu gani napoteza au nakikwepa?
h) Nini naweza kujifunza kutoka kwa huyu mtu/hali iliyotokea/kosa nililofanya/mafanikio niliyoyapata?
i) Ni hatua zipi za kutiliwa maanani/kupewa kipaumbele?
j) Maswali gani nijiulize mwenyewe/niwaulize wengine?
k) Nawezaje kubadili jambo husika kuweza kupata ushindi pande zote mbili?
l) Kipi kinawezekana?

Kuuliza maswali hayo yanasaidia kuliangalia tatizo/jambo kwa undani na kwa kadiri unavyoweza kuliangalia tatizo/jambo kwa undani zaidi ndivyo unavyoweza kutumia ujuzi/maarifa uliyonayo na mikakati iliyo bora kufanya mabadiliko unayoyahitaji

Jenga Mtazamo Huu Unapouliza Maswali

Tukio lolote linapotutokea bila kujali ni zuri au baya katika akili kuna mambo matatu huwa yanaendelea:

a) Fikra (thoughts)
b) Hisia (feelings)
c) Hali (circumstances)

Bila kujali hali ya tukio mambo hayo 3 ndiyo yanayotuongoza kwa sehemu kubwa namna tutakavyochagua jinsi tutaitikia (kurespond) katika tukio husika.

Mara nyingi husahaulika kuwa hatua ya utekelezaji katika matendo hufuata baada ya hatua ya kuuliza maswali.

Kwa nini hatua ya kuuliza maswali itangulie kabla ya hatua ya utekelezaji katika matendo? Umuhimu wa kuuliza maswali upo katika:

a) Kukusanya taarifa za kina
b) Kujenga uelewa na kujifunza
c) Kujenga, kuboresha na kuendeleza mahusiano
d) Kufafanua na kuthibitisha ulichosikiliza/ulichokiona/ulichokipokea
e) Kuchochea ubunifu na uvumbuzi
f) Kujenga ushirikiano
g) Kuweka malengo na kutengeneza mpango kazi
h) Kuchunguza, kugundua na kutengeneza nafasi/fursa mpya

Hivyo maswali tunayojiuliza wenyewe hutupatia fursa kwa ajili ya kufikiri na kuwezekana kwa namna ya kipekee kwa jambo husika tofauti na vile kabla hatujajiuliza hayo maswali.
Na jinsi utakavyoweza kuuliza maswali kwa ufasaha/kina zaidi ndivyo utaweza pia kupata matokeo makubwa zaidi

Umakini Unaouhitaji Kabla Hujaanza Kufanya Lolote

Kutegemeana mtu na mtu kuna tofauti kati ya vitu vinavyoleta bugudha wakati unafanya jambo. Mfano kuna mtu hawezi kufanya kazi katika mazingira yenye kelele au wakati redio inazungumza wakati huo huo kuna mwingine anaweza kufanya katika mazingira ambayo redio inazungumza.

Katika ulimwengu huu wa sasa ambao umetawaliwa na maendeleo ya sayansi na teknolojia kuna aina nyingi za bugudha zimeongezeka pia, mfano kwa wale wanaoutumia kompyuta kuna bugudha kama vile michezo (games), mitandao ya kijamii, barua pepe, utafutaji wa kitu katika tovuti (web search) hata ujumbe katika simu (SMS- chatting)

Unaweza kufikiri kwamba kwa kuanza kuchukua hatua ya kulitekeleza basi ndio suluhisho la wewe kuelekea kukamilisha jambo husika. Unahitaji kuwa makini kwa kufanya maandilizi ya kutosha namna ambavyo utashughulikia bugudha, vizuizi na vikwazo katika harakati zako za kutimiza malengo yako.

Njia rahisi ni kuondoa kila bugudha unayoifahamu itaathiri utendaji wako mapema kabla hujaanza kufanya jambo, mfano kuiweka simu katika hali ya ukimya (silent mode) , kuondoka katika mitandao ya kijamii wakati unatekeleza jambo (facebook, twitter n.k) na vitu vingine vyote vinavyoweza kuondoa umakini wako katika kazi husika (magazeti, majarida n.k)

Lakini sio mara zote tunaweza kukisia bugudha, kikwazo au kizuizi tunachoweza kukutana nacho katika harakati za kufikia malengo, kwa zile zote ambazo tumeshindwa kuzikisia na kuziwekea mikakati mapema tunaweza kuzishughulikia kwa kujua kusudi kubwa la kile unachokitekeleza. Kusudi likiwa kubwa kuliko kikwazo, bugudha au kizuizi unapata nguvu na sababu ya kusonga mbele

Namna Bora ya Kugawa Mapato Yako

Wakati unapopokea mapato/mshahara wako ugawe katika makundi haya 5 :



a) Sadaka
Kundi hili la fedha utalitumia kwa kufuata imani yako. Mara nyingi huwa ni asilimia kumi ya mapato.

b) Matumizi
Kundi hili la fedha ni kwa ajili ya kukuhudumia mahitaji yako ya kila siku. Huu huweza kuhusisha chakula, nauli kwa ajili ya kwenda sehemu unapofanya biashara/kazi n.k

c) Msaada
Kundi hili la fedha ni kwa ajili ya kutuma fedha kwa wale ndugu wanaokutegemea ili waweze kupata mahitaji yao ya kila siku. Mfano wazazi ambao wanakuwa hawawezi tena kufanya kazi kutokana na umri au kuumwa.

d) Dharura
Kundi hili la fedha ni kwa ajili ya kushughulika na misiba, ugonjwa na majanga ambayo yanaweza kukupata au kupata wanaokutegemea. Haya ni mambo yanayotokea kwa ghafla bila ya kuyatarajia

e) Kustaafu
Kundi hili la fedha ni kundi ambalo utalitumia kufanya uwekezaji, kuwekeza katika soko la hisa. Kundi hili halitakiwi kuguswa kabisa kwani ndilo linalotengeneza mfumo wa kukusaidia kipindi ambacho utakuwa huwezi kuzalisha/kufanya kazi

Kumbuka kadiri fedha yako inavyokua (financial growth) unahitaji pia kukuza misuli yako namna ya kuweza kuhimili/kudhibiti kiwango kikubwa cha fedha kwa kupata elimu endelevu ya fedha (financial education)

Njia Rahisi Kuzuia Utendaji Mbovu

Kama hali yetu ya hamasa ya kufanya jambo fulani haifanani/haiendani na jambo tunalohitajika kulifanya, moja kwa moja inapelekea kukosa hamasa ya kulitekeleza hilo jambo.

Kukosekana kwa hamasa kutapelekea kulihairisha hilo jambo na kusema litatekelezwa baadae au kesho n.k. Matokeo yake tutakuja kuhamasishwa na msukumo wa muda (time pressure).

Hamasa inayotokana na kufikia muda wa kuliwasilisha jambo (deadline) hupelekea utendaji mbovu kwa ujumla. Usisubiri mpaka uhamasishwe na muda ,jijengee nidhamu ya kufanya kila jambo ulilolipanga kwa wakati hata kama haujisikii kulifanya

Uwekaji Mipango Usioaminika

Ni asili yetu kuwa na matumaini mema juu ya jambo fulani ambayo yamepitiliza uhalisia. Mfano tunadhani kuwa tutafanya mambo mengi kwa muda mchache kuliko inavyotakiwa kiuhalisia au kudhani jambo unalolifanya litachukua muda mchache kufanyika kuliko muda halisi ambao jambo husika linaweza kuchukua.

Kimsingi huwa tunasahau kufikiri katika uhalisia muda ambao jambo litachukua kwa kuzingatia uzoefu wetu wa awali. Tunaweka mkazo (focus) katika jambo hilo moja na kusahau kuzikusanya taarifa mbalimbali zilizosambaa ambazo zimetokana na uzoefu wetu katika utekelezaji wa jambo linalofanana au linaloendana nalo. Taarifa hizi zingetusaidia kuweka uhalisia na hivyo kutupatia uwekaji mipango bora iliyo halisi.Hii hutupatia matokeo ya uwekaji mpango hafifu au mbovu.

Friday 13 March 2015

Maliza Robo ya Kwanza 2015 Hivi

Hatua 3 muhimu unazohitaji kuzichukua ili kuweza kutumia muda wako kwa ufanisi na kupata matokeo ya ndoto yako kwa haraka:

1. Have a Plan
Kuwa na mpango wa kina unaoanisha nini unachotaka kufanya na mpango huu ni lazima uwe umeuandika sehemu

2. Finish Something
Maliza kufanya kitu kwa kukianza kukifanya kila siku na kuendelea kubakia unakifanya mpaka kitakapokamilika

3. Don't Wait
Usisubiri tena mpaka ufike muda fulani ndo uanze kufanya unachotaka kufanya, anza kufanya kile kinachowezekana leo kwa kupangilia vizuri rasilimali ulizonazo

Thursday 12 March 2015

Usipobadilika, utamezwa na mabadiliko

Yanapotokea mabadiliko jifunze kukabiliana nayo (kuadapt) kwa haraka vinginevyo utakavochelewa zaidi kwa kutafakari nini cha kufanya na kulialia na hali halisi utatumia gharama kubwa kuyapokea na muda utakuwa umekwenda pia.

Kuna mambo 7 muhimu unayopaswa kufahamu kuhusu mabadiliko (change) ili uweze kupiga hatua zaidi:
a) Mabadiliko hutokea
b) Tazamia/tarajia mabadiliko
c) Fuatilia/simamia mabadiliko
d) Kabiliana na mabadiliko kwa haraka
e) Badilika kutokana na mabadiliko
f) Furahia mabadiliko
g) Kuwa tayari kubadilika kwa haraka ili urejeshe tena furaha yako ya awali kabla ya mabadiliko

Kumbuka mabadiliko hutokea na yataendelea kutokea bila kujali ulikuwa unayatarajia , umeyapenda au hujayapenda.
Kuwa tayari kwa ajili ya mabadiliko.

Msingi wa kutimiza maisha yenye ufanisi

Uwezo uliopo ndani yetu ni mkubwa sana kuliko kile ambacho tumeshakitendea haki kwa nafasi zetu tulizonazo kwa kutendea ulimwengu.
Maswali haya yatakusaidia kutafakari kitu gani ambacho unacho ndani yako bado hujakileta ulimwenguni kwa ajili ya kubadili hali ya sasa, maisha n.k

1. Mimi ni nani?
2. Kwa nini nipo hapa duniani/sehemu ulipo?
3. Nina uwezo kiasi gani au kwa kiwango gani?
4. Kitu gani ninao uwezo wa kukifanya?
5. Vigezo gani vinaweza kupima uwezo wangu?
6. Nani anaviweka au anapanga viwango (standards)?
7. Mchakato au mfumo gani naweza kutumia kuongeza uwezo wangu?
8. Nina mapungufu gani?

Ndani ya majibu ya maswali haya kuna msingi wa kuweza kutimiza maisha uliyokusudiwa kuishi, maisha ambayo yana ufanisi mkubwa.

Wednesday 11 March 2015

Fursa nyingi, Muda mchache na Rasilimali chache, Nifanyaje?

Ukifanya uchambuzi kwa kulinganisha kundi la "shughuli na fursa" na kundi la "muda na rasimali" utapata hitimisho ya kuona katika kundi la "shughuli na fursa" zipo nyingi kuliko kundi la "muda na rasilimali" tulizonazo kwa ajili ya kuwekeza.

Kitu cha kuzingatia ni kujua tofauti, kujifunza namna ya kuchuja na kuchagua "shughuli na fursa" chache kati ya "shughuli na fursa" nyingi ambazo ni halisi na zenye umuhimu ambazo zitaweza kukusogeza kufikia malengo yako katika maisha.

Tuesday 10 March 2015

Unachohitajika Kukifanya Sasa

Ukienda kula hotelini, mezani utakuta kuna chumvi, iko pale na unaweza kutumia vyovyote utakavyo. Lakini huwezi kuweka chumvi yote kwenye chakula kwa sababu ipo pale na umeshalipia kwenye chakula.

Tukiakisi uzoefu huo wa hotelini katika maisha yetu ya kila siku tunaweza kujifunza kwamba chochote unachofanya kwenye maisha usifanye kwa sababu kipo, au kwa sababu kila mtu anafanya. Ila fanya kwa sababu ndicho unachohitaji kufanya.