Sunday 25 September 2016

Uchambuzi wa Kitabu cha ONE MINUTE MANAGER

Habari rafiki yangu ambaye unaendelea kufuatilia makala katika blogu hii, wiki hii nilifanikiwa kusoma kitabu kinachoitwa One Minute Manager, hapa chini nimekushirikisha mambo ambayo nilijifunza na kuyanote ili kuweza kutusaidia kupata maarifa ambayo yatatusaidia katika maisha yetu ya kila siku. Karibu tujifunze



Utangulizi
Mambo ambayo tunajishughulisha nayo katika ratiba zetu za kila siku ikiwa kama ni ya kazi au hata biashara kwa namna moja au nyingine inahusisha kushirikiana na watu wenye weledi au ujuzi mbalimbali ili kutekeleza.

Kitabu hichi kinaelezea kwanza juu ya thamani ya hawa watu ambao ni rasilimali muhimu katika muhimili wako wa kuweza kukufanikisha kwa shughuli unayofanya, lakini pia waandishi wanajikita zaidi katika kujenga mazingira bora ya mahusiano kati yao na wewe kiongozi kuweza kusaidia kufanikisha malengo yenu.


Mambo  sita niliyojifunza:
1. Ukichunguza mameneja wengi utakuta ama wamejikita zaidi katika kusimamia watendaji wao wa chini kwa kuwatawala au kusimamia katika kuhakikisha matokeo yanapatikana, lakini sifa za meneja mzuri ni yule ambaye anaweza kujisimamia kwanza yeye binafsi, pili anawasimamia wale anaowaongoza na tatu ni yule ambaye anasimamia upatikanaji wa matokeo katika yale yanayotekelezwa. Huitwa mameneja wenye ufanisi


2. Ni muhimu kuzingatia kwa watu ambao unawategemea wafanye uzalishaji katika shughuli yako waweze kuwa vizuri na hali ya kuridhika na unavyofanya nao, kuridhika kwao na matokeo unayoyapata ni vitu vinavyohitaji kwenda sambamba.


3. Uzalishaji wowote usipimwe kwa kigezo cha idadi tu bali kigezo cha ubora pia, katika uzalishaji ubora na idadi ni mambo ambayo yanahitaji kwenda sambamba


4. Ili kuweza kuwasaidia watu unaowaongoza kuwa na utaratibu wa kufanya vikao ambavyo utaweza kuwasikiliza kuhusu mambo ambayo wamefanikiwa kuyakamilisha na yale ambayo bado wanaendelea kuyafanyia kazi kuyakamilisha, na kikubwa unahitaji kuwapatia nafasi ya wao kufanya maamuzi na siyo kila maamuzi uyafanye wewe tuu


5. Meneja mzuri ni yule ambaye anakupa majukumu yako na nini kinachotarajiwa kutoka kwako kabla hujaanza kazi husika, na mnakuwa mmekubaliana vigezo vya utendaji kazi ambavyo unaweza kujipima kati ya kile unachokifanya na unachotarajia kutoa matokeo


6. Kazi inapofanyika vizuri watu wanatakiwa kupongezwa au kusifiwa kwa kile ambacho wamekifanya na upongezaji ni muhimu uwe unaamuliwa na takwimu za kile anachozalisha


Tuendelee kuyaweka katika matendo ili tuweze kuyabadilisha maisha yetu