Monday 28 November 2016

Jinsi Ya Kutambua Uwezo wa Kompyuta Yako

Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio!

Rafiki kompyuta ni kifaa ambacho kinachukua nafasi kubwa katika matumizi ya kazi mbalimbali katika zama hizi za habari. Kompyuta zina sifa mbalimbali kutegemeana na mahitaji ya kazi zinazokwenda kufanya. Hivyo ni muhimu kujua namna ya kuthibitisha sifa zilizobebwa na kompyuta husika kabla hujanunua.

Katika makala ya leo napenda kukushirikisha njia ya kuangalia sifa tatu muhimu za kompyuta ambazo ni muhimu kuzikagua.

(a) Bofya kitufe cha kulia cha mouse katika neno Computer mara baada ya kuwasha kompyuta yako. Kisha chagua sehemu iliyoandikwa Properties , bofya. Hapa utapata taarifa kuhusu aina ya processor iliyowekwa katika kompyuta na memory iliyowekwa katika kompyuta pia. Processor hupimwa kwa kipimo cha GHz.

Soma Makala Hii Inayohusiana : Jinsi ya Kutumia Kompyuta Yako Kuwa Chanzo cha Intaneti

Katika kipengele cha System kwenye kurasa ya properties iliyofunguka taarifa za processor utazikuta katika sehemu iliyoandikwa Processor.
Na taarifa za memory utazikuta katika sehemu iliyoandikwa Installed memory (RAM). RAM hupimwa kwa kipimo cha GB.

(b) Bofya kitufe cha kulia cha mouse katika neno Computer mara baada ya kuwasha kompyuta yako. Kisha chagua sehemu iliyoandikwa Manage, bofya.
Chagua tena sehemu iliyoandikwa Disk Management, kisha angalia sehemu iliyoandikwa Disk 0 ndiyo sehemu utakayopata ukubwa wa hard disk iliyowekwa katika kompyuta. Hard disk hupimwa kwa kipimo cha GB kama ilivyo kwa RAM.

Rafiki unaweza kuwashirikisha wengine kuhusu blogu hii kwa ajili ya kupata maarifa mbalimbali na pia unaweza kubofya hapa ili kuweza kupata makala kila inapowekwa kupitia barua pepe yako.

Goodluck Moshi
Author
StadizaMafanikio

0 comments:

Post a Comment