Tuesday 3 January 2017

Uchambuzi wa Kitabu cha " SOMETIME YOU WIN SOMETIME YOU LEARN"

Mafunzo tunayoyapata kutoka shuleni yanatusaidia kutupa maarifa na msingi wa kutusaidia kutuongoza katika kuelekea maisha yetu nje ya shule au maisha yetu ya kila siku. Ukuaji wa mtu unachangiwa sana na fursa anazojipa katika kujifunza mambo mapya, kujifunza huku kunagunduliwa kutokana na maswali ambayo tunakuwa tunawauliza makocha wetu ili kujua sehemu gani ya kuboresha zaidi. Maisha ni kujifunza.

1. Baadhi ya makosa ambayo tunayafanya yanachangiwa sana na usahaulifu ambao unasababishwa na kutokufanya mambo kwa wakati pale tunapokumbuka kuwa hatujaweka jambo fulani sawa na badala yake tunapuuza na kuahirisha na kuamini tutafanya wakati ujao. Hii huleta gharama kubwa aidha kifedha au muda.

2. Ni vizuri kufikiria kuwa na mlinganyo katika mafunzo tusichague mafunzo ya kufanikiwa tuu , mafunzo yanayotokana na kushindwa ni muhimu pia katika kutujenga kuwa na uwezo wa kuhimili kushindwa bila kuwa na majuto kutokana na kushindwa au kuwa na hofu ya kushindwa kwa mambo yaliyo mbele yetu ya baadaye.

3. Kuna pengo kati ya matendo au kufanya na kujua kile unachopaswa kukifanya, unapoweza kuziba au kuondoa pengo husika ndipo utaweza kufanikiwa

4. Mara nyingi tunafanya ulinganisho kati ya udhaifu tulionao na ubora wa wengine na wakati mwingine hata kinyume chake pia. Ni muhimu kuwa makini na yale unayojisemea binafsi au unafikiri juu yako binafsi

5. Kushindwa au kupoteza kunatarajiwa kutufundisha mambo mengi sana kuliko kututawala na kutufanya tuwe tumezimia moyo au kukatishwa tamaa, kushindwa ni kipindi cha mpito tuu mara baada ya kipindi kupita hatutakiwi kuendelea kubaki hapo.

6. Asilimia kubwa ya watu wanapitia vipindi mbalimbali vigumu, ni katika vipindi hivi hivi wanatarajia kuona fursa iliyojificha katika hali wanazopitia, fursa ya kujifunza, kukua, kukusaidia kusogea viwango vingine, kamwe usikubali kuruhusu kukosa au kushindwa kutumia fursa ya kujifunza katika kipindi kigumu.

7. Majigambo huzuia kujenga roho ya kujifunza kutokana na kuridhika kuona kuwa uko bora kuliko wengine wakati kiuhalisia unakuwa bado unawahitaji wengine pia na kuendelea kujifunza. Majigambo yanakujengea hali ya kulaumu badala ya kukubali kuwajibika.

8. Ni rahisi kufanikiwa mara baada ya kushindwa kunakotokana na kujaribu kufanya jambo kuliko kuweza kufanikiwa kutokana na kutoa sababu za kushindwa kufanya jambo husika. Ni muhimu kufahamu hakuna jambo unalolipata kiurahisi bila kukubali kulipa gharama na kuweka jitihada ya kuweza kulipata jambo husika.

9. Hakuna mtu ambaye kwa namna moja au nyingine hapitii vipindi vigumu katika maisha , kukwepa kupitia vipindi hivi vigumu vya maisha hakutakusaidia kukua, zaidi unapoteza fursa ya kufanikiwa.

10. Ili kuweza kufanya maboresho katika maeneo mbalimbali ya maisha yako unahitaji kujiboresha kwanza wewe binafsi. Suala la kujiboresha binafsi ndiyo linaweka msingi kwa mambo yote mengine ambayo yanayofuata.

11. Hitaji la kiwango cha chini kinachohitajika ili uweze kujiboresha zaidi ni kuamua kutumia angalau kwa saa moja kila siku kwa miaka mitano mfululizo kujifunza katika eneo unalolipenda , basi baada ya hapo utakuwa mahiri katika eneo ambalo umelipenda. Na ni muhimu kujitoa kwa kukusudia na kikamilifu kuhakikisha inajengeka na kuwa tabia.

12. Unapopoteza kitu chochote katika maisha yako, huwa jambo hili haliambatani na furaha, lakini katika mambo ambayo hautakiwi kuyapa nafasi ya kupoteza mojawapo ni tumaini. Haijalishi unapitia hali gani lakini usikubali kutoa nafasi ya kupoteza tumaini katika jambo lolote.

Rafiki napenda kukuarifu kuwa ikiwa una maswali au mada ambayo ungependa niiandikie makala , unaweza tuma katika anuani yangu luckmoshi@gmail.com

Goodluck Moshi
Mwandishi
StadizaMafanikio

Wednesday 21 December 2016

Sababu Kumi (10) Zinazokuzuia Kuanza Biashara

Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala mbalimbali zinazowekwa katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio.

Napenda kukupongeza kwa hatua uliyochukua ya kuamua kutembelea mtandao huu kwa ajili ya kuchota maarifa ambayo yatakusaidia katika maisha yako na pia kukushukuru kwa ajili ya kuwashirikisha marafiki wengine waungane nasi kwa ajili ya kuendelea kuboresha maisha yetu.

Katika makala yetu ya leo napenda kukushirikisha sababu kumi (10) ambazo zinatumika kama pazia la kujifichia au kisingizio cha kusababisha watu wasianze kutengeneza biashara zitakazohudumia watu na hatimaye kuwaingizia kipato.

1. Kukosa fedha (mtaji) kwa ajili ya kuanza biashara.

2. Kuwa na idadi kubwa ya ndugu au jamaa wanaokutegemea kwa ajili ya kuwasaidia kwa huduma mbalimbali kama mahitaji muhimu, elimu na kadhalika.

3. Kukosa mawasiliano na watu ambao wataweza kukuunga mkono katika biashara yako.

4. Kukosa uwezo wa kutosheleza wa kuanza , kuendesha na kusimamia biashara yako.

5. Kukosa muda wa kuendesha na kusimamia biashara kutokana na kutingwa na shughuli nyingine.

Soma Makala Hii Inayohusiana : Mambo Matano (05) Yanayosababisha Kushindwa

6. Kukosa mtu sahihi ambaye anaweza kukuongoza hatua kwa hatua katika biashara mpaka uweze kusimama mwenyewe.

7. Umri wako umeshakwenda sana.

8. Uhitaji wa muda mwingi kutoka kuanza biashara mpaka kukua na kuendelea.

9. Kuchukia kushughulika na wafanyakazi ambao unatakiwa kuwasimamia.

10. Hofu ya kuwa na biashara ni hatari (risky).

Rafiki hizi ni baadhi tu ya sababu zinazotumiwa, je ni sababu ipi umeitumia kujitetea kama hoja ya msingi ambayo inakuzuia mpaka sasa kuanza kutengeneza biashara?

Tafadhali nishirikishe maoni yako kwa kutaja sababu ipi ambayo unaona ndiyo kikwazo kikubwa au kunitajia sababu nyingine unazozifahamu, ili tuweze kuzijadili katika makala zijazo.

Rafiki napenda kukuarifu kuwa ikiwa una maswali au mada ambayo ungependa niiandikie makala , unaweza tuma katika anuani yangu luckmoshi@gmail.com

Goodluck Moshi
Mwandishi
StadizaMafanikio

Monday 5 December 2016

Jinsi ya Kuinstall Kapersky KIS 2017 Katika Microsoft Windows 7

Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio!

Ili kulinda programu na data zilizopo katika kompyuta muhimu kuweka programu ambazo zitazuia programu hatarishi kuathiri ufanyaji kazi wa kompyuta. Programu hatarishi hufahamika kwa jina la virusi (virus).
Na programu ambayo inazuia kompyuta kuathiriwa na virusi huitwa antivirus.

Kuna watengenezaji wengi ambao wanaandaa na kuuza hizi programu za antivirus. Baadhi ya antivirus ni Kapersky, McAfee, Avira, Escan, AVG na kadhalika.

Soma Makala Hii Inayohusiana Jinsi ya Kutatua Tatizo la Barua Pepe Kutoingia Katika Inbox

Katika makala hii napenda kukushirikisha namna ya kutatua changamoto ambayo unaweza kukutana nayo wakati unainstall Kapersky Internet Security 2017 (KIS 2017).

Changamoto moja kubwa ambayo nimekutana nayo wakati nafanya installation ya KIS 2017 katika Operating System ya Windows 7 Professional ni kuwa programu hizi mbili kutokuendana (compatible).

KIS 2017 inahitaji Windows 7 Professional Service Pack 1 ili ikubali kuwa installed. Ikiwa una Windows 7 Professional isiyo Service Pack 1 unahitaji kupakua (download) Service Pack 1 kwa kusearch katika Google na kisha kufanya installation.

Baada ya kufanya installation ya Service Pack 1 kwa mafanikio ndipo uendelee na kuinstall KIS 2017.

Tatizo hili la kuhitaji Service Pack 1 utalipata ikiwa Windows 7 ndiyo inatumika. Lakini hautakutana na tatizo hili ikiwa unatumia Windows 8 au Windows 10.

Rafiki unaweza kuwashirikisha wengine kuhusu blogu hii kwa ajili ya kupata maarifa mbalimbali na pia unaweza kubofya hapa ili kuweza kupata makala kila inapowekwa kupitia barua pepe yako.

Goodluck Moshi
Author
StadizaMafanikio

Tuesday 29 November 2016

Shule Mbili (02) Bora Unazopaswa Kuhudhuria Katika Maisha

Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio!

Rafiki suala la kujifunza ni endelevu halina ukomo. Pale unapopata ukomo wa kujifunza maana yake unajiandaa na kushindwa. Mara baada ya kumaliza elimu ya darasani kamwe usikubali kufanya hitimisho la kusoma.

Masomo mengi ambayo tunahitaji kujifunza inatakiwa kuwa na sehemu ambapo mtaala umeandaliwa utakaokuongeza hatua kwa hatua mpaka uweze kufuzu katika masomo hayo. Tofauti na elimu rasmi ya darasani ambapo unakuwa na mtaala maalum.

Huku katika maisha ya kila siku hakuna mtaala maalum bali unajifunza kutegemeana na mahitaji ya ujuzi husika. Hapa chini nakushirikisha shule mbili ambazo unaweza kuhudhuria masomo na kujifunza mambo mengi.

Soma Makala Hii Inayohusiana : Namna ya Kutambua Dalili Za Kushindwa

Shule ya kwanza unayoweza kuhudhuria ni uzoefu ulionao. Angalia historia yako mambo ambayo umekuwa ukiyafanya yamekujengea uwezo ambao una makosa uliyoyafanya unayoyaweza kuyakwepa kwa kutoyarudia lakini pia mambo uliyofanikiwa ambayo yanaweza kukusaidia kujikita zaidi na kuendelea kuyaboresha kuyatumia ili kukupatia mafanikio zaidi.

Shule ya pili unayoweza kuhudhuria ni kujifunza kwa wale walioshindwa na kufanikiwa katika lile eneo ambalo unalifanyia kazi. Angalia katika wale walioshindwa mambo yaliyowapelekea kushindwa na uyaepuke wakati huo huo ungalie pia wale waliofanikiwa uzingatie yale yaliyowasababisha wafanikiwe ili yakusaidie pia.

Rafiki unaweza kuwashirikisha wengine kuhusu blogu hii kwa ajili ya kupata maarifa mbalimbali na pia unaweza kubofya hapa ili kuweza kupata makala kila inapowekwa kupitia barua pepe yako.

Goodluck Moshi
Author
StadizaMafanikio

Monday 28 November 2016

Jinsi Ya Kutambua Uwezo wa Kompyuta Yako

Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio!

Rafiki kompyuta ni kifaa ambacho kinachukua nafasi kubwa katika matumizi ya kazi mbalimbali katika zama hizi za habari. Kompyuta zina sifa mbalimbali kutegemeana na mahitaji ya kazi zinazokwenda kufanya. Hivyo ni muhimu kujua namna ya kuthibitisha sifa zilizobebwa na kompyuta husika kabla hujanunua.

Katika makala ya leo napenda kukushirikisha njia ya kuangalia sifa tatu muhimu za kompyuta ambazo ni muhimu kuzikagua.

(a) Bofya kitufe cha kulia cha mouse katika neno Computer mara baada ya kuwasha kompyuta yako. Kisha chagua sehemu iliyoandikwa Properties , bofya. Hapa utapata taarifa kuhusu aina ya processor iliyowekwa katika kompyuta na memory iliyowekwa katika kompyuta pia. Processor hupimwa kwa kipimo cha GHz.

Soma Makala Hii Inayohusiana : Jinsi ya Kutumia Kompyuta Yako Kuwa Chanzo cha Intaneti

Katika kipengele cha System kwenye kurasa ya properties iliyofunguka taarifa za processor utazikuta katika sehemu iliyoandikwa Processor.
Na taarifa za memory utazikuta katika sehemu iliyoandikwa Installed memory (RAM). RAM hupimwa kwa kipimo cha GB.

(b) Bofya kitufe cha kulia cha mouse katika neno Computer mara baada ya kuwasha kompyuta yako. Kisha chagua sehemu iliyoandikwa Manage, bofya.
Chagua tena sehemu iliyoandikwa Disk Management, kisha angalia sehemu iliyoandikwa Disk 0 ndiyo sehemu utakayopata ukubwa wa hard disk iliyowekwa katika kompyuta. Hard disk hupimwa kwa kipimo cha GB kama ilivyo kwa RAM.

Rafiki unaweza kuwashirikisha wengine kuhusu blogu hii kwa ajili ya kupata maarifa mbalimbali na pia unaweza kubofya hapa ili kuweza kupata makala kila inapowekwa kupitia barua pepe yako.

Goodluck Moshi
Author
StadizaMafanikio

Sunday 27 November 2016

Namna Ya Kudelete File Katika Kompyuta

Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio!

Rafiki moja ya operation ambayo inafanyika mara kwa mara katika matumizi ya kompyuta ni delete. Delete hufanya kazi ya kufuta file lililopo katika sehemu au location katika kompyuta.

Kuna namna mbili ambazo unazoweza kutumia kufuta file katika kompyuta:

(a) Katika namna hii ya kwanza unachagua file unalotaka kulifuta kisha unabofya kitufe katika keyboard kilichoandikwa delete au unabofya kitufe cha kulia cha mouse na kuchagua delete.

Soma Makala Hii Inayohusiana : Jinsi ya Kutengeneza Bootable USB Drive

Mara baada ya kubofya, file litondolewa kutoka sehemu iliyopo kwenda katika recycle bin. Unaweza kulirudisha file ikiwa umelifuta kwa makosa kwa kubofya na kuchagua restore. Ikiwa pia unataka ulifute katika recycle bin basi rudia hatua za kawaida za kufuta file kama nilivyoelekeza hapo juu.

(b) Katika namna hii ya pili unachagua file unalotaka kulifuta kisha unabofya kwa pamoja (simultaneously) vitufe katika keyboard shift na delete.

Mara baada ya kubofya, file litaondolewa kutoka sehemu iliyokuwa lakini halitapelekwa katika recycle bin. Hapa unakuwa hauwezi kulirudisha file lilipokuwa. Hii hufahamika kama kudelete permanently

Rafiki unaweza kuwashirikisha wengine kuhusu blogu hii kwa ajili ya kupata maarifa mbalimbali na pia unaweza kubofya hapa ili kuweza kupata makala kila inapowekwa kupitia barua pepe yako.

Goodluck Moshi
Author
StadizaMafanikio

Saturday 26 November 2016

Uchambuzi Kitabu cha " THE COMPOUND EFFECT"

Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio!

Darren Hardy ni mwandishi wa kitabu cha THE COMPOUND EFFECT. Katika kitabu hiki mwandishi anatueleza siri kubwa iliyopo katika kufanya mambo hatua kwa hatua kidogo kidogo ili kufikia mafanikio. Hapa tunajifunza kuwa mafanikio ni mchakato na sio kitu ambacho kitatokea mara moja. Hapa chini ninakushirikisha yale mambo ambayo nimejifunza.

1. Fanya maamuzi ya kudhibiti/kuyaongoza maisha yako kwa kutafuta kujifunza kutoka kwa watu waliofanikiwa na kuyaweka katika katika miaka yako ambayo una nguvu/mapema kabla umri haujaongezeka sana

2. Kama unahitaji mafanikio makubwa wasaidie wengine wafanikiwe zaidi

3. Amua kufanya maisha yako kuwa maabara yako binafsi kwa ajili ya kujaribu kanuni mbalimbali za mafanikio kufanyiwa mafunzo na utafiti

4. Maamuzi yako yanatengeneza hatma yako

5. Maamuzi yako unayoifanya kila siku yanaamua kukuwezesha kufikia maisha unayotaka au kufikia maafa ya maisha unayotaka

6. Kama hujui kitu fulani weka jitihada na unadhifu katika kujifunza mpaka uweze kukivuka kikwazo

7. Si jambo/hatua nzuri ya mafanikio katika maisha kwenda pamoja na kundi (kimazoea) kuwa mtu ambaye anafanya mambo ya tofauti na makubwa

8. Unahitaji ari na uwajibikaji ili kuweza kuyafikia mafanikio unayoyahitaji

9. Tengeneza fedha na mali za kutosheleza kutunza familia yako maisha yao yote hata kipindi ambacho huna uwezo wa kufanya kazi au haupo kabisa

10. Hatua ndogo unazochukua na kuzifanya kwa muda kwa msimamo bila kusitisha au kuruka huleta mabadiliko kwa kiasi kikubwa

11. Machaguo nadhifu madogo + Msimamo + Muda = Tofauti kwa kiasi kikubwa

12. Siri ya mafanikio ambayo wazazi wetu wametumia katika maisha yao ni jitihada, bidii, nidhamu na tabia njema

13. Unashindwa pale unapoanza kuacha kufanya vile ambavyo vilikufanya ufanikiwe

14. Maisha yetu huishia kuwa ni matokeo ya machaguo tunayofanya

15. Ukiamua kukaa na kutokufanya uchaguzi maanake umeamua kupokea machaguo yoyote yanayokuja kwako

16. Bila kujali maamuzi unayofanya ni madogo kiasi gani, pale yanapofanywa kwa kulimbikizwa kwa muda mrefu huleta athari/faida

Soma Makala Hii Inayohusiana : Uchambuzi wa Kitabu " TOUGH TIMES NEVER LAST BUT TOUGH PEOPLE DO"

17. Unapofanya uchaguzi hakikisha unafikiria kwanza

18. Pale unapoamua kuwajibika 100% kitu kifanikiwe ndipo utapata mafanikio katika kitu hicho

19. Unawajibika kwa kila unachokifanya, usichokifanya na vile ambavyo utaitikia vile ulivyofanyiwa

20. Fursa inapokutana na maandalizi mazuri hutengeneza bahati

21. Kanuni ya bahati
     Maandalizi + Mtazamo + Fursa + Matendo = Bahati

22. Hatua ya kwanza kuelekea mabadiliko ni kufahamu/kutambua (awareness)

23. Huwezi kuboresha kitu bila kukifatilia na kukipima

24. Kitu chochote hakiwezi kuwa tabia mpaka ukifanyie kazi kwa wiki 3

25. Fanya machaguo sahihi kila siku kila wiki na mapema utaanza kuona utoshelevu kifedha katika maisha yako

26. Kila siku fanya uchaguzi wa kusonga mbele

27. Marekebisho kidogo katika mambo yale yale ya kila siku hubadilisha kwa kasi matokeo katika maisha yako

28. Fanya kitu cha tofauti ili upate matokeo tofauti na bora zaidi

29. Watu waliofanikiwa wanajua malengo yao kwa ufasaha ,wanajua wao ni nani na wanataka kuwa nani

30. Watu wasiofanikiwa wanajua malengo yao katika vichwa vyao hawayaandiki sehemu ambayo watajikumbusha mara kwa mara

31. Unatakiwa kuwa na malengo katika kila sehemu ya maisha yako
sio malengo ya upande mmoja mfano fedha peke yake

32. Unatakiwa uwe na ulinganifu katika kila eneo la maisha yako: biashara, fedha, afya, kiroho, kifamilia na mahusiano

33. Mafanikio ni kitu ambacho unakivuta kwa kuwa mtu anayevutia

Rafiki unaweza kuwashirikisha wengine kuhusu blogu hii kwa ajili ya kupata maarifa mbalimbali na pia unaweza kubofya hapa ili kuweza kupata makala kila inapowekwa kupitia barua pepe yako.

Goodluck Moshi
Author
StadizaMafanikio

Read, Apply and Share!