Habari rafiki!
Katika makala ya leo ninapenda kukushirikisha namna ya "kushare" intaneti kutoka kwenye kompyuta na kwenda kwenye vifaa vingine vyenye uwezo wa kupokea intaneti.
Katika makala ya leo ninapenda kukushirikisha namna ya "kushare" intaneti kutoka kwenye kompyuta na kwenda kwenye vifaa vingine vyenye uwezo wa kupokea intaneti.
Kompyuta yoyote ambayo ina kifaa kinachoitwa "Wireless Network Card" inayo uwezo wa "kushare" intaneti ambayo inaipokea kwenda katika vifaa vingine ambavyo pia vinauwezo wa kupokea intaneti bila kutumia waya kati ya vifaa hivyo.
Vifaa vyote vyenye uwezo wa kupokea intaneti bila ya kutumia waya kati yake na chanzo cha intaneti huwa katika maelezo au sifa za kifaa husika utakuta wameandika neno "Wifi" kwa matamshi neno hili linatamkwa "waifai".
Kompyuta ambayo itatumika kama chanzo cha intaneti inatakiwa iwe imewekwa programu ya "Microsoft Windows 7 Operating System"
Hatua za Kufanya:
1. Hakikisha kompyuta yako imewaka na imeshapokea intaneti kwa kutumia waya
2. Nenda upande wa kushoto chini katika "screen" ya kompyuta kisha kwa kutumia kitufe cha kushoto cha "mouse" bofya katika sehemu iliyoandikwa "start" yenye alama kama ya dirisha yenye rangi nne (bluu,kijani,nyekundu na njano)
3. Tumia "keyboard" kuandika neno "cmd" katika kiboksi kilichoandikwa maneno yaliyofifia yaliyolala kuelekea kulia yanayosemeka "Search programs and files"
4. Bonyeza kitufe cha kulia cha "mouse" katika sehemu yenye alama nyeusi inayofuatiwa na maneno "cmd" kisha chagua maneno yaliyoandikwa "Run as administrator" kwa kutumia kitufe cha kushoto cha "mouse"
5. (a) Ikiwa mara baada ya hatua ya 4 utaulizwa neno siri basi itabidi uliandike katika kwa usahihi ili uweze kuendelea. Hii ina maana akaunti unayotumia siyo "Administrator"
(b) Ikiwa mara baada ya hatua ya 4 itatokea maelezo yenye kichwa "User Account Control" ikikuhitaji uchague kati ya "Yes" na "No", chagua "Yes" ili uweze kuendelea. Hii ina maana akaunti unayotumia ni "Administrator"
6. Katika kiboksi cheusi kilichojitokeza andika neno lifuatalo kisha bofya kitufe cha "Enter" katika keyboard;
netsh wlan set hostednetwork mode="allow" ssid="Intaneti" key="tehama" keyUsage=persistent
7. Ikiwa baada ya hatua ya 6 utapata maneno yaliyoandikwa "The hosted network started" basi andika tena neno lifuatalo kisha bofya kitufe cha "Enter" katika keyboard;
netsh wlan start hostednetwork
8. Rudia hatua ya 2
9. Bofya kwa kutumia kitufe cha kushoto cha "mouse" katika maneno yaliyoandikwa "Control Panel", kisha bofya sehemu iliyoandikwa "View network status and tasks" , kisha bofya tena sehemu iliyoandikwa "Change adapter settings"
10. Bofya kwa kutumia kitufe cha kulia cha "mouse" sehemu iliyoandikwa "Local Area Connection" kisha uchague kwa kubofya kitufe cha kushoto cha "mouse" sehemu iliyoandikwa "Properties"
11. Bofya kwa kutumia kitufe cha kushoto cha "mouse" sehemu iliyoandikwa "Sharing" , kisha bofya kwa kutumia kitufe cha kushoto cha "mouse" ndani ya kiboksi kidogo chenye maneno yaliyoandikwa "Allow other network users to connect..."
12. Bofya kwa kutumia kitufe cha kushoto cha "mouse" sehemu iliyoandikwa "Home networking connection" kisha chagua kwa kitufe cha kushoto cha "mouse" sehemu yenye maneno "Wireless Network Connection 2"
13. Bofya kwa kutumia kitufe cha kushoto cha "mouse" ndani ya kiboksi kidogo chenye maneno yaliyoandikwa "Allow other network users to control..." ili kuondoa alama ya vema ndani ya kiboksi, kisha bofya sehemu iliyoandikwa "OK"
Sasa unaweza kutumia intaneti hiyo hiyo inayoingia katika kompyuta yako kwenda katika vifaa vingine. Jina la intaneti ni lile lililoandikwa katika ssid hapa tumetumia Intaneti na neno la siri litatumika tehama
NB:
1. ssid hili hutumika kutambulisha netiweki yako katika makala hii tumetumia Intaneti
1. ssid hili hutumika kutambulisha netiweki yako katika makala hii tumetumia Intaneti
2. key hili ni neno siri utakalotumia kuweka ulinzi na kuamua watu ambao wanaweza kutumia netiweki yako
3. ssid na key unaweza kuandika maneno yoyote unayopendelea
Ili kuendelea kupata makala mpya kadiri zinavyowekwa au kutumiwa vitabu katika mfumo wa nakala tete, unaweza kuandika barua Pepe yako sehemu ya juu kulia iliyoandikwa Jiunge
0 comments:
Post a Comment