Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio!
Flash ni kifaa ambacho hutumika kwa ajili ya kuhifadhi data kutoka katika kompyuta. Flash inaweza kuchomekwa na kutolewa katika kompyuta. Kwa kiingereza kifaa hiki huitwa Flash Disk au USB Flash Drive.
Uwezo wa kifaa hiki hupimwa kwa kipimo cha MB au GB. MB ni kifupi cha neno Megabyte wakati GB ni kifupi cha neno Gigabyte. GB ni kubwa kuliko MB.
Operating System ambazo huwa zinakuwa installed katika kompyuta hupatikana katika CD au DVD. CD ni kifupi cha neno Compact Disk na DVD ni kifupi cha neno Digital Versatile Disk. CD au DVD ambayo itatumika kuinstall operating system huwa zimetengenezwa kuwa na uwezo wa kuboot moja kwa moja.
Changamoto kubwa iliyopo sasa ni utunzaji wa CD au DVD. CD au DVD huwa zinakwaruzika au kupata scratch na hii husababisha kushindwa kuendelea kutumika. Kwa kutengeneza bootable flash inasaidia kuepuka hii changamoto. Ili kutengeneza bootable flash unahitaji kufuata hatua zifuatazo:
(a) Hakikisha umeinstall programu inaitwa PowerISO katika kompyuta yako, umehifadhi operating system yako katika kompyuta na unayo flash disk.
(b) Fungua programu ya PowerISO. Bofya katika sehemu ya Tools na uende kuchagua "create bootable USB drive".
(c) Katika sehemu iliyoandikwa image file litafute faili ambalo lina operating system. Faili lina kuwa linaishia na .iso
(d) Katika sehemu iliyoandikwa destination USB drive , chagua flash unayoitaka kuitengeneza iwe bootable.
(e) Baada ya kumaliza hatua hizo hapo juu utakuwa tayari umetengeneza bootable flash.
Rafiki unaweza kuwashirikisha wengine kuhusu blogu hii kwa ajili ya kupata maarifa mbalimbali na pia unaweza kubofya hapa ili kuweza kupata makala kila inapowekwa kupitia barua pepe yako
0 comments:
Post a Comment