Mambo ya msingi niliyojifunza kutoka katika kitabu cha My Philosophy for Successful Living kilichoandikwa na Jim Rohn.
Hiki ni kitabu kifupi sana ambacho ukikisoma utagundua muda uliotumia ni uwekezaji bora ambao umefanya katika maisha yako.
Haya ni baadhi ya mambo kati ya mengi ambayo utayapata katika kitabu hichi:
1. Unapokuwa katika biashara ya kuwashirikisha mawazo yanayohusu eneo lolote unahitaji kuongozwa na mambo makuu mawili
a) Hakikisha watu wanapata thamani ya fedha ambayo wanaitoa kulipia gharama ya huduma unayowapa
b) Hakikisha muda wao ambao wanautumia kwa ajili yako wanaona ni muda ambao wameutumia vizuri na kufuarahi
2. Maarifa na hamasa unayohitaji kupata kwa ajili ya kubadilisha maisha yako hayaji kwa mara moja huja katika vipande vipande kupitia semina , vitabu, na njia nyingine mbalimbali ambazo zinaweza kukupatia mawazo mapya
3. Faida kubwa unazopata kutokana na kujiendeleza binafsi ni unalipwa kutokana na thamani unayoleta katika soko la hicho unachofanya na unalipwa kutokana na vile ambavyo umekuwa kutokana na kujiendeleza
4. Unapokuwa umedhamiria kufanya mabadiliko katika maisha yako ni vizuri ukampata kocha au mkufunzi muongozaji ambaye atakupatia maarifa sahihi yatakayowezesha utoe huduma ya kipekee na thamani katika soko unalohudumia
5. Mitaji mikuu mitatu unayohitaji kuwa nayo ili uweze kufanikiwa zaidi:
a) Stadi au ujuzi ulionao ambao unaweza kuwasaidia watu kuboresha maisha yao
b) Tafuta wateja ambao unaweza kuwahudumia na uwe na bidhaa bora ya kuwapatia
c) Kuwa na mtandao wa watu wanaokusaidia kuendelea na kupiga hatua katika eneo ulilopo
6. Ni vizuri kukubali na kuwapongeza watu kutokana na mchango wanaoutoa katika shughuli fulani, hii inasaidia kuwahamasisha kufanya vizuri zaidi
7. Ni muhimu kutenga muda na kujitahidi kuwa na uwezo/stadi/ujuzi wa kuwasiliana (skilled communicator)
8. Unahitaji kuwa na mfumo binafsi unaokuongoza ukiwa na miongozo wa yapi unayafanyia kazi na yapi ambayo huyafanyii kazi
9. Ni vizuri kujifunza kutokana na uzoefu ulioupitia wewe binafsi au uzoefu wa watu wengine ambao pia wamefanya kile unachotaka kufanya, uzoefu huu utakusaidia kupunguza hatari ambazo unaweza kuzikwepa kutokana na kufahamu na pia kutusaidia kujua fursa zilizopo na kuzitumia ipasavyo
10. Maamuzi tunayoyafanya yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na hisia tulizonazo kutokana na hali za zamani tulizozipitia na hali za wakati ujao
11. Kukiwa na sababu kwa nini kitu fulani kinafanywa na malengo kwa ajili ya hicho kinachofanywa husababisha msukumo katika kukitenda kitu husika. Na sababu huweza kugawanyika katika ngazi kuanzia ngazi binafsi,ya familia, na jamii inayokuzunguka kwa ujumla
12. Kwa kitu chochote ambacho unakifanya ni muhimu kitathimini na kupima kama kweli unafikia na upo katika uelekeo sahihi kama ulivopanga katika malengo yako
13. Mambo muhimu ya kuzingatia
a) Hakikisha unakuwa mzalishaji
b) Thamini mahusiano
c) Heshimu asili yako
d) Jali afya yako ya kiroho
e) Fanya majukumu yanayokupasa mengine mwachie Mungu
Falsafa ya Jinsi ya Kuishi Maisha ya Mafanikio
Related Posts:
Uchambuzi Kitabu cha " MEGALIVING, 30 DAYS TO PERFECT LIFE"Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio! Robin Sharma ni mwandishi wa kitabu cha MEGALIVING, 30 DAYS TO PERFECT LIFE. Katika kibao hiki Robin anaeleza namna ambavyo unaweza k… Read More
Tofauti Kati Ya Save Na Save As Katika Programu Za KompyutaHabari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio! Katika programu zinazotumika katika kompyuta , njia ya pekee ya kukulinda usipoteze kazi uliyofanya ni kusave. Katika kila programu m… Read More
Uchambuzi wa Kitabu cha "ACT LIKE A SUCCESS THINK LIKE A SUCCESS"Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio! Steve Harvey ni mchekeshaji maarufu sana ambaye ameanza fani hii kati ya miaka ya 1980. Pamoja na fani hii ya uchekeshaji Steve amean… Read More
Tofauti Ya Matumizi Ya Copy na CutHabari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio! Katika matumizi ya kompyuta kila siku kuna operations ambazo hufanywa mara kwa mara ili kukuwezesha kukamilisha kazi (task) uliyokuwa… Read More
Uchambuzi wa Kitabu " LUNCHTIME TRADER"Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio! Marcus de Maria ni mwandishi wa kitabu cha THE LUNCH TIME TRADER. Katika kitabu hiki mwandishi ametueleza namna ambavyo unaweza kutum… Read More
Safi sana
ReplyDelete🦻 good one
ReplyDelete