Mambo ya msingi niliyojifunza kutoka katika kitabu cha My Philosophy for Successful Living kilichoandikwa na Jim Rohn.
Hiki ni kitabu kifupi sana ambacho ukikisoma utagundua muda uliotumia ni uwekezaji bora ambao umefanya katika maisha yako.
Haya ni baadhi ya mambo kati ya mengi ambayo utayapata katika kitabu hichi:
1. Unapokuwa katika biashara ya kuwashirikisha mawazo yanayohusu eneo lolote unahitaji kuongozwa na mambo makuu mawili
a) Hakikisha watu wanapata thamani ya fedha ambayo wanaitoa kulipia gharama ya huduma unayowapa
b) Hakikisha muda wao ambao wanautumia kwa ajili yako wanaona ni muda ambao wameutumia vizuri na kufuarahi
2. Maarifa na hamasa unayohitaji kupata kwa ajili ya kubadilisha maisha yako hayaji kwa mara moja huja katika vipande vipande kupitia semina , vitabu, na njia nyingine mbalimbali ambazo zinaweza kukupatia mawazo mapya
3. Faida kubwa unazopata kutokana na kujiendeleza binafsi ni unalipwa kutokana na thamani unayoleta katika soko la hicho unachofanya na unalipwa kutokana na vile ambavyo umekuwa kutokana na kujiendeleza
4. Unapokuwa umedhamiria kufanya mabadiliko katika maisha yako ni vizuri ukampata kocha au mkufunzi muongozaji ambaye atakupatia maarifa sahihi yatakayowezesha utoe huduma ya kipekee na thamani katika soko unalohudumia
5. Mitaji mikuu mitatu unayohitaji kuwa nayo ili uweze kufanikiwa zaidi:
a) Stadi au ujuzi ulionao ambao unaweza kuwasaidia watu kuboresha maisha yao
b) Tafuta wateja ambao unaweza kuwahudumia na uwe na bidhaa bora ya kuwapatia
c) Kuwa na mtandao wa watu wanaokusaidia kuendelea na kupiga hatua katika eneo ulilopo
6. Ni vizuri kukubali na kuwapongeza watu kutokana na mchango wanaoutoa katika shughuli fulani, hii inasaidia kuwahamasisha kufanya vizuri zaidi
7. Ni muhimu kutenga muda na kujitahidi kuwa na uwezo/stadi/ujuzi wa kuwasiliana (skilled communicator)
8. Unahitaji kuwa na mfumo binafsi unaokuongoza ukiwa na miongozo wa yapi unayafanyia kazi na yapi ambayo huyafanyii kazi
9. Ni vizuri kujifunza kutokana na uzoefu ulioupitia wewe binafsi au uzoefu wa watu wengine ambao pia wamefanya kile unachotaka kufanya, uzoefu huu utakusaidia kupunguza hatari ambazo unaweza kuzikwepa kutokana na kufahamu na pia kutusaidia kujua fursa zilizopo na kuzitumia ipasavyo
10. Maamuzi tunayoyafanya yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na hisia tulizonazo kutokana na hali za zamani tulizozipitia na hali za wakati ujao
11. Kukiwa na sababu kwa nini kitu fulani kinafanywa na malengo kwa ajili ya hicho kinachofanywa husababisha msukumo katika kukitenda kitu husika. Na sababu huweza kugawanyika katika ngazi kuanzia ngazi binafsi,ya familia, na jamii inayokuzunguka kwa ujumla
12. Kwa kitu chochote ambacho unakifanya ni muhimu kitathimini na kupima kama kweli unafikia na upo katika uelekeo sahihi kama ulivopanga katika malengo yako
13. Mambo muhimu ya kuzingatia
a) Hakikisha unakuwa mzalishaji
b) Thamini mahusiano
c) Heshimu asili yako
d) Jali afya yako ya kiroho
e) Fanya majukumu yanayokupasa mengine mwachie Mungu
Falsafa ya Jinsi ya Kuishi Maisha ya Mafanikio
Related Posts:
Usipuuze TatizoMatatizo mengi kamwe hayatatuliwi au hayadhibiti kwa ufanisi kutokana na kutoyapa uzito wa kutosheleza. Hakuna tatizo ambalo halina umuhimu kiasi kuwa hatuhitaji kujali kuhusu hilo tatizo. Mfano kwa mwanafunzi inawezekena hap… Read More
Usifanye Kosa Hili Katika BiasharaUnapoamua kuchagua kuwa utashirikiana na mtu mwingine kufanya biashara ya ndoto yako, usitumie kigezo cha huyo mshirika kuwa ni mmoja wa wanafamilia wako au ni mmoja wa marafiki zako wa karibu sana, utakuwa umejiingiza katika… Read More
Fanya Haya ili Ukue1. Usitamani mambo yangekuwa marahisi, tamani ungekuwa bora mno Don't wish it were easier; wish you were better 2. Usitamani ungekutana au ungekuwa na matatizo machache,tamani ungekuwa na ujuzi zaidi Don't wish for less prob… Read More
Je, Unajua?Ni bora kufanya kitu kisicho kamili kuliko kutokufanya chochote kisicho na dosari Better to do something imperfectly than to do nothing flawlessly… Read More
Tazama Kushindwa kwa Jicho HiliKushindwa hakuamaanishi wewe ndiye uliyeshindwa bali kunamaanisha hujafanikiwa bado Kushindwa hakumaanishi haukutimiza/haujafanikisha kitu bali kunamaanisha umejifunza kitu Kushindwa hakumaanishi wewe ni mjinga bali kunamaa… Read More
Safi sana
ReplyDelete🦻 good one
ReplyDelete