Matatizo mengi kamwe
hayatatuliwi au hayadhibiti kwa ufanisi kutokana na kutoyapa uzito wa
kutosheleza. Hakuna tatizo ambalo halina umuhimu kiasi kuwa hatuhitaji kujali
kuhusu hilo tatizo. Mfano kwa mwanafunzi inawezekena hapati A au B lakini
anafaulu. Kwa mwanafunzi anaweza akalipuuzia kwa kigezo kuwa hajafeli.
Kamwe
usilipuuze tatizo wala usipuuze uwezo wako wa kukabiliana na tatizo. Tambua
kuwa tatizo unalokutana nalo kuna mamilioni ya watu duniani wameshapitia tatizo
kama hilo. Ukiwa na mtazamo chanya kuhusu tatizo utabadili tatizo na
litakupatia uzoefu. Na unapokosa mtazamo sahihi kuhusu tatizo unalokumbana nalo
itasababisha tatizo husika kuwa kubwa zaidi.
Siri kubwa ambayo imewafanya watu waliofanikiwa
kuendelea vizuri ni mtazamo juu ya matatizo wanayokutana nayo. Hapa nakuletea
kanuni sita kuhusu matatizo na ambazo ukizifanyia kazi ipasavyo wewe pia
utakuwa mshindi kwa kuwa kila unapokutana na tatizo utakuwa sehemu ya utatauzi
wa tatizo husika.
1. Kila mtu
anayo matatizo
Usifikiri
ukishafanikiwa utakuwa ndio umeyaaga matatizo, kadiri unavyofanikiwa ndivyo
matatizo unayatengeneza mapya. Mafanikio huwa hayaondoi matatizo bali
hutengeneza matatizo mapya. Kwa mfano inawezekana unafikiri ukipata kazi fulani
ndo utakuwa umefanikiwa Sana, lakini kumbe unaweza kupata hiyo kazi lakini bosi
wako akawa ni mkorofi. Sawa suluhisho unaweza kufikiri ni kujiajiri hapo pia
utakutana na matatizo ya kushughulika na wafanyakazi wako ili wazalishe zaidi. Kubaliana
na uhalisia kuwa Hakuna mtu ambaye yuko huru hana matatizo bali kutegemeana na
shughuli unayojishughulisha nayo basi utakutana na matatizo yanayoendana na
shughuli husika
2. Kila
tatizo lina ukomo wake
Hakuna tatizo
ambalo ni la kudumu yaani litakuwepo milele. Muda wa uhai wa tatizo ukiisha
litakufa kwa kuisha/kutokuwepo kabisa na litapita. Kila tatizo huwa lina muda
wake ambao kiuhalisia ni mdogo kwa hivyo hakuna haja ya kukwepa au kukimbia
tatizo kwa kuwa ukikwepa tatizo sio kuwa unatatua tatizo bali unatengeneza
matatizo mapya.
3. Kila
tatizo lina fursa
Tatizo linaweza
kuwa tatizo kwa mtu mmoja ila kwa mtu mwingine linaweza kuwa fursa. Mfano hospitali
zipo kwa sababu watu wanaumwa au wanasheria wapo kwa sababu kuna matatizo ya
kisheria. Kwa hiyo kwa mgonjwa ana tatizo la kuumwa lakini mtu mwingine amabaye
anafikiria kuhusu kutatua matatizo ya magonjwa mbalimbali atafungua hospitali
kutibu magonjwa yanayosumbua jamii na hivyo kumpatia fursa kwa kuwa atalipwa
anapotoa huduma hiyo.
4. Kila
tatizo litakubadilisha
Hakuna tatizo
ambalo litakuja katika maisha yetu na kutuacha kama lilivyotukuta. Tatizo
litakufanya uamke au uchangamke na usonge mbele. Na hii ni kwa sababu ya wewe
kuwa na uwezo wa kuchagua tatizo husika likkufanyie nini katika ujuzi wako,
uzoefu wako, au likufundishe nini ili uweze kuwa na uwezo stahihi wa kutatua
tatizo husika
5. Unao uwezo wa
kuchagua tatizo likuathiri vipi/kwa kiwango gani
Namna ambavyo
unavyolikabili tatizo linavyokutokea inaamua pia athari ya tatizo husika
kwako.Inawezekana usiwe na uwezo wa kuchagua tatizo linalokutokea lakini unao
uwezo wa kuchagua namna unavyolikabili tatizo.
6. Kuna
namna chanya na hasi jinsi ya kukabili kila tatizo
Mara zote chagua
namna chanya ya kutatua tatizo kuliko namna hasi ya utatuzi wa tatizo. Jambo la
msingi ni kuwa kama huwezi kutatua tatizo basi unahitaji kulisimamia kwa
ubunifu. Unapotatua tatizo leo unakuwa ni sehemu ya suluhisho la tatizo na
hivyo itakupelekea kufaidika na faida zinazoambayana na kutatua tatizo husika.
Kumbuka utatuzi
wa matatizo hufanywa rahisi kama matatizo yatachukuliwa au kutazamwa kama
changamoto.
0 comments:
Post a Comment