Habari na karibu ndugu
mpenzi msomaji wa blogu hii ya. Ni matumaini yetu umekuwa na wiki ya mafanikio
sana.
Leo nitazungumzia namna
ya kuwaandaa watu wenye sifa za uongozi ambao umewatambua upo nao katika timu
yako katika taasisi. Kuwaandaa viongozi hawa watarajiwa kunahusisha wewe ambaye
tayari ni kiongozi pamoja na hao viongozi watarajiwa , nah ii inaweza
kulinganishwa kwa kiasi Fulani kama unawawapatia mafunzo.
- Tengeneza Mahusiano
na Viongozi Chipukizi Unaowaandaa
Viongozi
chipukizi ambao umeshawatambua unahitaji kuwafahamu, kuwasikiliza historia za
maisha yao ili uweze kuwajua zaidi ya vile unavowajua tu kiofisi. Huhitaji
kujua kuhusu uwezo au ubora wao tu bali unahitaji pia kujua kuhusu madhaifu yao
pia ili uweze kujua namna ya kuwafanya wakamilifu kwa hayo mapungufu
uliyoyatambua. Na ukiweza kujenga mahusiano mazuri maanake utafanya wakupende
na pia kuongeza nia na kiu kwao kujifunza kutoka kwako
- Washirikishe ndoto
yako
Wakati
unaendelea kuwafahamu usiwaache wao peke yao tu wakuambie ya kwao, na wewe pia
unahitaji kuwashirikisha pi historia ya maisha yako na unahitaji kwenda hatua
ya ziada kwa kuwashirikisha ndoto yako kuhusiana na taasisi ambayo unaiongoza.
Na hii itawasaidia kujua ni wapi unataka kwenda na hivo kujiunga kujitoa
kufuatana nawe mpaka mwisho wa safari yako
- Waombe utayari wao
kujitoa kiuongozi
Moja
ya kiungo muhimu ambacho kinaweza kumfanya kiongozi chipukizi kuwa kiongozi
mwenye mafanikio, ni utayari wa kujitolea kiuongozi. Ni muhimu sana kwa hawa
viongozi chipukizi unaowaandaa wawe wamejitoa kwa ajili ya uongozi pamoja na
taasisi. Na unahitaji kuwaeleza gharama ambayo itawachukua kwa wao kuwa
viongozi, na jambo la muhimu ni uwe mkweli kuhusu mambo ambayo watahitaji
kuzingatia au kuyajua hata kabla ya hatua yenyewe ya kufanya maamuzi ya
kukubali kuweza kujitoa kiuongozi.
- Weka malengo kwa
ajili ya ukuaji
Viongozi
hawa chipukizi wanahitaji kujua malengo yaliyo fasaha ambayo wanatakiwa
kuyapigania au kuyafanikisha, nah ii itawasaidia kujua ni nini wnatakiwa
kufanya na pia ni vitu gani vinatarajiwa kutoka kwao. Jambo muhimu zaid la
kuzingatia ni unapoweka malengo zingatia malengo yawe yako wazi, fasaha na
yanayoeleweka. Malengo yawe ni sahihi kwao lakini pia yawe yanaweza kupimika.
Baada ya kuyafahamu hayo malengo ni vizuri yawekwe katika maadnishi ili kila
mmoja aweze kujitoa kikamilifu katika malengo hayo
- Weka mambo ya msingi
sawa
Ni
muhimu sana kuweka misingi kwa kuwaelewesha majukumu yao na wayafahamu kwa
undani. Weka kwa ufasaha mategemeo yako kwao lakini pia na wao wajue vipaumbele
ni vipi katika majukumu yao. Na uhakikishe wanaweza kujua tofauti kati ya kazi
iliyo ya umuhimu sana na ile kazi yenye umuhimu kiasi.
- Mfumo wa
ufundishaji unaofaa
Kuna
hatua tano muhimu zinazoweza kukupatia matokeo mazuri hasa inapohusisha
kuwaandaa kiuongozi viongozi chipukizi
i.
Kuwa mfano kwanza kwa kila unachotaka
waweze kukifanya
ii.
Wafundishi au waelekeze
iii.
Simamia maendeleo ya kile
unachowaelekeza
iv.
Wahamasishe
v.
Wape fursa pia ya kutengeneza viongozi
kati yao viongozi chipukizi
- Simamia maendeleo
yao bila kuacha
Ni muhimu ukawa na mikutano iliyo rasmi na isiyo
rasmi pia ili kuweza kujua mahitaji, matatizo ambayo wanakumbana nayo pia. Na
hii itakusaidia kuwapatia vifaa sahihi zaidi na kuendelea kuwapa ujasiri na
kuwahamasisha.
0 comments:
Post a Comment