Inawezekana umefika katika hatua ambayo unaona kama
ungekuwa na kiasi fulani cha fedha basi matatizo yako yote ambayo
yamekuwa yanakusumbua au yanakukabili bila kujali yana umri kiasi gani
yangekuwa yamepatiwa ufumbuzi wa kudumu.
Kama
ingekuwa kuwa na fedha ni kupata ufumbuzi wa matatizo tuliyonayo ina
maana tungetarajia watu wenye fedha nyingi wangekuwa hawana matatizo
kabisa. Lakini katika maisha ya leo baadhi ya hawa watu ambao wana fedha
sana ndiyo ambao wana matatizo zaidi kama ya magonjwa, kukosa furaha
n.k ukiwalinganisha na wale ambao hawana fedha au wana fedha kiasi
kidogo.
Kwa mfano fedha haiwezi kukulinda usiumwe lakini inaweza
kukusaidia kupata huduma bora zaidi ya kiafya baada ya kuumwa. Kwa hiyo
tungekosea sana kusema kwa kuwa una hela basi umeshapona mara baada ya
kugundua unaumwa, bali unapokuwa unaumwa hatua ya kwanza ni kuanza
kufikiri namna ya kukupatia huduma ya afya inayoweza kutibu ugonjwa
unaokusumbua halafu hatua ya pili inafuata namna ya kutumia kiasi cha
fedha uliyonayo kupata huduma husika kutatua tatizo linalokukabili. Kwa
hiyo fedha huja katika hatua ya mbele sana na siyo hatua ya kwanza
katika utatuzi wa tatizo bali ni kitu kinachowezesha utatuzi wa tatizo.

Kwa maana nyingine fedha haina ubaguzi kwamba wewe ni
wa rangi gani au umetoka katika kundi gani la uchumi (mtu masikini au
mtu wa daraja la kati au mtu tajiri) au wazazi wako walikuwa na hali
gani ya kifedha au hata unafikiri kuwa wewe ni nani (nafasi yako katika
jamii).
Fedha haiwezi kubagua kwa kuwa
haijui mambo mengi yanayomhusu yule anayemiliki kiasi husika cha fedha.
Fedha haijui una kiwango gani cha elimu au maarifa, fedha haina masikio
wala macho wala uwezo wa kuhisi. Bali fedha ipo kwa ajili ya kutumiwa,
kuwekwa akiba, kuwekezwa.
Kila mmoja wetu
anayo haki na fursa sawa kuweka jitihada ya kupata fedha zaidi bila
kujali jana yako ilikuwaje. Inawezekana ukaona ni ngumu na kuna
changamoto na vikwazo zaidi lakini inawezekana kufanya na kuibadili
maisha yako.
Kwa hiyo ni muhimu sana kukaa chini na kutafakari na
kufafanua kwa kina ni nini hasa kusudi la wewe kuwa na kiasi cha fedha
unachokihitaji. Kuwa na ufafanuzi au maana sahihi ya wewe kuwa na kiasi
cha fedha unachokihitaji itakusaidia kuendana vema na tabia hizo kuu
tatu za fedha nilizoziainisha hapo juu (kutumiwa, kuwekwa akiba na
kuwekezwa).
0 comments:
Post a Comment