1. Watu wengi wanofanikiwa sio kwamba wana ujuzi au uwezo kuzidi ambao unao bali ni kiwango cha maarifa walochonacho ndicho kinatofautisha. Ni muhimu kuwa na hamu na kiu kubwa ya kupata maarifa yanayohusu eneo unalotaka kuwa bora zaidi
2. Ukiwa kiongozi unapoletewa tatizo na mteja usipende sana kujua historia ambayo haitakusaidia katika utatuzi wa tatizo , jitahidi kulichambua tatizo kwa lengo la kukusaidia kupata maarifa zaidi ya jinsi ya kulitatua, halafu uwajibike kulibeba tatizo na kisha ufanye maamuzi sahihi kwa kupata ufumbuzi wa tatizo husika
3. Mara nyingi huwa tunavutiwa sana na hatua fulani mtu mwingine anayofikia ya mafanikio, kikubwa ni kufahamu matokeo ya kiwango cha juu wanayoyafikia kunakuwa kuna gharama wanayolipia ya kuwa na nidhamu, kujitoa hasa kutimiza ilo jambo na Kujituma kwa jali ya juu
4. Mara nyingi huwa tunapenda kuona mtu fulani ni mbaya kutokana labda ameshindwa kutekeleza jambo fulani, ni vema ukiwa kiongozi kuyatazama mambo katika jicho la kuelewa nini kinaendelea na pia kupenda kuweka mkazo kutazama upande wa uzuri wa mtu
5. Kunahitajika kuwa na mkazo katika yale mambo ambayo ni muhimu na yanafaida kwako, na kuyaondoa yale ambayo hayana faida au hayaongezi thamani kwako, ni vizuri kila siku unaandika mambo yale ambayo yana umuhimu , na ambayo unahitaji kuyafanyia kazi kuelekea ndoto yako, na pia ni vema ukaweka jitihada kufanya yaliyobora kwa maisha yako ili uvune yaliyobora pia, na ni muhimu kufurahia pia maisha kadiri unavyoelekea kutimiza ndoto yako
6. Vile unavyofikiri ndivyo unavyokuwa , mara nyingi watu hutazama jambo katika lenzi ya kutowezekana, uwoga, vikwazo na mambo ya kufikiria kutokana na vile anavyoamini au unafahamu, ni vizuri ukajiwekea viwango ambavyo unaviamini na unaweza kuvunja rekodi kwa kuvitimiza, siku zote tazama mambo katika lenzi ya kuwekezekana bila kujali nani alifanya nini
7. Watu wa familia yako ndio ambao watakuwa na wewe muda wote katika hali yoyote hawawezi kuacha peke yako , ni vizuri hata katika shida na mafanikio yako ukaambatana nao, ni vema kujizoesha kuwapigia simu wazazi wako, kumbusu mwenza wako na kuwakumbatia watoto wako hii huongeza upendo na ukaribu
8. Mambo mengi ambayo tunayafanya hutanguliwa kwanza na fikra ambayo tunawaza juu ya jambo husika hivyo ni muhimu sana kuwaza chanya na kuwezekana kwa jambo ili kusaidia kukupa msukumo na nguvu ya kulifanya liweze kutokea
9. Njia nzuri ya kupata kile unachokitaka ni kwa kuomba, na siku zote watu wapo tayari kukupatia kike kitu ambacho tu kitaleta maana kwako au kinaongeza thamani kwako na kuweza kuwasaidia watu wengine
10. Inashauriwa kuamka mapema na kufanya mazoezi kutokana unakuwa upo na nguvu na hamasa ya kufanya jambo , akili inakuwa na uwezo mkubwa kutokana na mifumo kufanya kazi ipasavyo, na unakuwa na muda wa kutosha kutekeleza ndoto yako
11. Vipindi vya maisha ambavyo vina changamoto au vigumu ndivyo vipindi ambavyo ni vizuri kwa sababu hutusaidia kujua ujasiri wetu, kujifahamu zaidi na kuwa na shauku zaidi ya kufanikiwa katika jambo husika
12. Unapoanguka hakikisha unaamka tena unapukuta vumbi unaendelea kusonga mbele usikubali kubaki pale ulipo kuwa bora zaidi ya kabla hujaanguka
13. Unahitaji kutoulisha udhaifu wako , tunaweza kuwa bora sana kwa kufanya yale mambo yanayotufanya tuwe bora sana , tunakuwa waoga kwa kuendelea kuyatazama yale mambo yanayotuogopesha
Hayo ni baadhi kati ya mengi yaliyo katika kitabu cha Stunning Success kilichoandikwa na mwandishi Robin Sharma
0 comments:
Post a Comment