Sunday, 9 October 2016

Faida Nne (04) Unazopata Ukiwa na Akaunti ya Gmail.

Habari rafiki yangu unayefuatilia makala zinazowekwa katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio!
Leo napenda kukuletea mambo manne (04) ambayo unaweza kuyafanya kwa kuwa na akaunti ya barua pepe kutoka kampuni ya Google. Akaunti hii hufahamika kwa jina la Gmail.

1. Nafasi ya ukubwa wa kiasi cha Gigabyte 15 kwa ajili ya kuhifadhi taarifa zako mtandaoni
Kila mtu ambaye ana akaunti ya Gmail anapata sehemu ya kuhifadhi "data" yenye ukubwa wa kiasi cha Gigabyte 15. Hii nafasi inapatikana bure bila malipo yoyote. Na unaweza kuzitumia taarifa zako sehemu yoyote duniani ambapo umeunganishwa na mtandao.

2. Kuhifadhi orodha ya majina kutoka katika kumbukumbu ya simu yako
Kila mtu ambaye ana akaunti ya Gmail anapata nafasi ya kuhifadhi majina, namba za simu kutoka katika kumbukumbu ya mawasiliano ya simu husika. Hii huduma pia inapatikana bila ya malipo yoyote. Ni huduma ambayo huwa inasaidia sana wakati aidha unapotaka kubadili simu yako ama simu inapokuwa imeharibika ama simu imepotea. Ikiwa umehifadhi orodha yako katika Gmail utaweza kurejesha orodha ya majina na namba za simu kwa haraka na urahisi.

3. Kuwa na blogu katika mtandao wa blogspot.com
Kila mtu ambaye ana akaunti ya Gmail anaweza kufungua blogu ambapo ataweza kuweka taarifa au maarifa mbalimbali kwenda kwa jamii husika. Blogu hii ataifungua bila ya malipo yoyote. Jina lake la blogu atalipendekeza kutegemeana na anavyoona inafaa na baada ya jina hilo ambalo amependekeza litafuata neno .blogspot.com

4. Kuweka programu mbalimbali katika simu zinazotumia Google Android OS
Programu mbalimbali ambazo zinatumika katika smartphone unaweza kuzipata kutoka katika Play Store. Ili uweze kuziona na kuchagua programu hizi kutoka play store unahitaji kuwa na akaunti ya Gmail. Mfano tunapowapelekea mafundi wa simu watuwekee programu kama vile WhatsApp, You tube, Facebook na kadhalika, wanachofanya hasa ni kutumia akaunti ya Gmail kuingia playstore, kutafuta programu ulizomwambia na kuziweka, ambapo ni kitendo ungeweza pia kukifanya ikiwa unayo akaunti ya Gmail.
Endelea kutembelea mtandao huu kujifunza zaidi.

Related Posts:

  • Je, Umepoteza Ujasiri (Confidence)?Katika jambo lolote unalofanya unahitaji kuwa na ujasiri ili uweze kuwa na nguvu au stamina ya kuweza kulileta katika uhasilia(kulikamilisha) bila kujali vikwazo utakavyokutana navyo njiani. Zifuatazo ni njia au namna ambavy… Read More
  • Mbinu za Kustahimili MatatizoSiri moja kubwa ambayo imewafanya watu waliofanikiwa kuendelea vizuri ni mtazamo juu ya matatizo wanayokutana nayo. Ukizielewa kanuni hizi 6 kuhusu matatizo na kuzifanyia kazi ipasavyo wewe pia utakuwa mshindi. 1. Kila mtu a… Read More
  • Sumu ya MafanikioUnapokosa lengo kubwa katika maisha yako kwa kutokujua nini hasa unahitaji na unakipataje, mara nyingi hupelekea kutegemea maoni au ushauri wa watu wengine zaidi katika kuamua kitu cha kufanya kwa ajili ya maisha yako badala … Read More
  • Kanuni Inayoamua Wewe Kufanikiwa au KushindwaKatika mambo tunayofanya kuna matokeo mawili; aidha kufanikiwa sawasawa na malengo tuliyojiwekea kabla hatujanza kutekeleza jambo au kutokufanikiwa ambapo tunaweza kukuita kushindwa kutokana na kutofikia vigezo tulivyoviweka … Read More
  • Fahamu Haya Kama KiongoziKwa kila unayemuongoza unahusiana naye kwa kulingana na mojawapo kati ya ngazi hizi tano. Ngazi ya chini kabisa ni ngazi ya kwanza na ngazi ya juu kabisa ni ngazi ya tano: 1. Ngazi ya kwanza ambayo tunaanza nayo katika safar… Read More

0 comments:

Post a Comment