Ili kuweza kuwa na
utajiri endelevu katika maisha yako na unaojitosheleza ni muhimu ukawa
mwekezaji. Uwekezaji upo wa aina nyingi. Hapa ninakuletea aina za uwekezaji
unazoweza kuzifanya ili kukuwezesha wewe na wale watu wako wa karibu kuishi
maisha ya utajiri wa kujitosheleza:
- Uwekezaji binafsi
Watu
ambao wanatengeza utajiri wanafanya uwekezaji binafsi . hawa wanakuwa wasomaji
kwa kujifunza. Daima huweka jitihada ya kujiboresha wao wenyewe siku hadi siku
na kuongeza mipaka ya maeneo ambayo wanona wakijaribu watafanikiwa. Wanaongeza
maarifa na uwezo wa kushawishi siku hadi siku. Na kiwango cha jitihada
wanachoweka katika kujiboresha huwa kipo katika hali ya kukua siku hadi siku.
- Kuwekeza kwa
wengine
Mwanamafanikio
maarufu duniani Zig Ziglar alisema ukitaka kupata kitu chochote katika maisha
ni vizuri uwasaidie wengine wapate vile wanavyovihitaji katika maisha yao. Watu
wenye utajiri utagundua wamewekeza kuwasaidia wengine wafikie malengo yao na
hivyo kusababisha na wao kufanikiwa kwa kuwafanikisha wenzao
- Wekeza katika
taasisi
Katika
taasisi unayofanya wekeza katika kuijenga taasisi hiyo ili iweze kuwa bora na
taasisi inapoweza kuwa bora inawezesha kuongeza upataji wa mapato. Kuongezeka
kwa mapato kwa taasisi kwa ujumla kunasaidia pia wale waliosababisha kuongezeka
kwa mapato kuneemeka na hiyo faida. Kwa hivyo hili likifanyika katika kipindi
chako cha kutumikia taasisi yako maanake utaongeza kujenga utajiri siku hadi
siku.
- Wekeza katika mali
zinazoongezeka thamani
Ubadilishaji
wa fedha kwenda katika mali ambazo zinaongezeka thamani na zinafanya kazi
badala yako siku hadi siku huongeza utajiri kwako. Mfano wa hili ni nyumba
ambayo imejengwa kwa lengo la kupangasha au kukodisha. Sasa ile fedha
uliyowekeza katika hiyo nyumba utaipata kwa kuendelea kuongezeka mwaka hadi
mwaka bila yaw ewe kufanya kazi.
- Wekeza katika
mawazo
Vitu
vingi tunavyoviona leo havikuanza moja kwa moja bila kupitia hatua Fulani,
vingi vilianza kama wazo na kuendelezwa. Mawazo amabyo ni mazuri yakichanganywa
na uchukuaji hatua wa kuyaweka katika matendo huleta matokeo mazuri ambayo
yanaleta utajiri
Haise nimejifunza mengi
ReplyDelete