Kila mtu anapokuja hapa
ulimwenguni anakuwa amebeba maagizo maalum ambayo anatakiwa ayatekeleze kwa
ajili ya kufanya ulimwengu kuwa sehemu bora ya kuishi. Njia nzuri ya kuweza
kujua kile unachofanya kama ni sahihi ni kwa kuyafahamu maagizo uliyobeba
ambayo hakuna mwingine zaidi yakeo anaweza kuatekeleza. Na maagizo hayo unaweza
kuyafahamu kwa kuanza kujitathimini kwa njia ya maswali kama je umeshatambua
maagizo uliyoyabeba? Au je una kipaji, uwezo, shauku gani ambayo ni ya kipekee
kwako na hakuna mtu mwingine wa aina yoyote anayo isipokuwa wewe tu? Au ya
mwisho ambayo ni nzuri zaidi ni kwa kuangalia kile unachokifanya na kujiuliza
je unachokifanya ndicho ulichokusudiwa au sababu ya wewe kuwepo hapa
ulimwenguni?
Hapa ninakuletea
viashiria ambavyo vitakusaidia kujitathmini kama kwanza upo katika kada au eneo
sahihi lakini la muhimu zaidi ni lile unalofanya katika hilo eneo ndilo lile
unalopaswa au sababu yaw ewe kuwepo hapa ulimwenguni.
- Unakuwa
unapenda kile unachokifanya kwa kuwa kinakuvutia , kinakupa shauku na
mvuto wa kipekee kukifanya
- Unakuwa
unataka kuwa bora sana katika kile unachokifanya. Na miongoni mwa asilimia
kumi ya watu walio bora katika eneo au kada yako unataka na wewe uwepo
- Unawapenda
wale wote ambao wako katika eneo au kada uliyopo na pia unapenda kufikia
mafanikio ambayo wao pia wameyafikia
- Unapenda
kujifunza kuhusiana na hilo eneo au kada yako kwa kusoma mambo yanayohusu
kada yako, kuhudhuria semina au mihadhara ambayo inazungumzia mambo
yanayohusu eneo au kada yako, kusikiliza program za sauti zilizorekodiwa
kuhusiana na kada yako. Na zaidi hata iweje unakuwa huchoki kujifunza
katika hilo eneo lako.
- Kada
au eneo sahihi kwako ni lile ambalo kwako ni rahisi kujifunza na pia ni
rahisi kuweka katika matendo yale uliyojifunza. Ila kwa wengine inaonekana
ni vigumu na kwako inakuwa kawaida sana kufanya.
- Kutokana
na kufurahia kile unachofanya unakuta muda unakuwa kama umesimama kwako na
inaweza ikawa imekukolea sana hadi unasahau kula, kunywa hata kwend
mapumziko
- Mafanikio
unayoyapata katika eneo ndiyo inayokupa hamasa ya kipeekee na furaha
adimu. Na pia unakuwa huwezi kuacha kusubiri au kukaa muda mrefu bila
kufanya kitu kikusogeze hatua moja mbele upate mafanikio mengine
- Unapenda
kufikiri kuhusu hilo eneo au kada yako na pia wakati haufanyi kitu
unapenda kuzungumza kuhusu eneo au kada yako. Masiha yako yote yanakuwa
yamezngukwa na mambo yanayohusu eneo au kada yako
- Unapenda
kuwa na mahusiano na kuwa karibu na watu zaidi ambao wapo katika eneo
lako.
- Na
mwisho ni kuwa unapenda kufanya hayo unayofanya kwa maisha yako yote,
hutaki kustaafu kuyafanya kwa kuwa unafarahia jinsi unavyoyafanya
Kwa kuweza kutambua
eneo au kada yako sahihi ambayo unatakiwa uwe itakusaidia kupata mafanikio nah
ii itakusaidia kuwelekeza moyo wako kufanya vizuri na vizuri zaidi.
0 comments:
Post a Comment