Watu wengi hufikiri
kuwa na lengo lilio fasaha pamoja na kuwa na mtazamo chanya kuhusiana na
ukamilishaji wa lengo ndio msingi mkuu wanaohitaji ili kuweza kuwa na furaha
pamoja na kufanikiwa. Lakini kumbe hata kabla hujaanza safari yako ya
kukamilisha lengo lako ni muhimu kuwa na mipango hatua kwa hatua
inayokuhakikishia uwezekano mkubwa wa kukamilisha lengo lako.
Haa ninakuletea hatua
saba zitakazokuwezesha kukamilisha lengo lolote ambalo unajiwekea
- Amua
ni nini hasa unakihitaji katika kila eneo la maisha yako. Unahitaji
kufafanua lengo lako katika lugha rahisi kiasi kwamba motto mdogo aweze
kuelewa. Mfano unaweza kusema lengo lako ni kuwa na fedha nyingi, lakini
uwingi wa fedha unazotaka haujaweka ni fedha nyingi kiasi gani. Sasa
kutokuwa fasaha katika lengo kunakupelekea kutokuwa na hamasa na kufanya
maamuzi ya kukamilisha lengo.
- Andika
lengo lako na lifanye liwe linaweza kupimika. Lengo ambalo halijaandikwa
linakuwa ni lengo ambalo halihuishwa au halijapewa nguvu ya kuwa hai.Ukilifanya
lipimike maanake unakuwa umetengeneza tageti unayotaka kuifikia.
- Weka
ukomo wa kukamilisha. Unahitaji kuwa fasaha ni lini unahitaji kukamilisha
lengo husika. Sehemu ya ubongo inayoitwa “subconscious” inapenda kuwa na ukomo nah ii inakusaidia
kuwa na nguvu na kukupa hamasa ya kuelekea kufanikisha lengo husika
- Ainisha
vikwazo ambavyo unahitaji kuvivuka ili kukamilisha lengo. Fahamu kitu gani
kinaweza kwenda tofauti. Fahamu ni kitu gani kipo kati yako na lengo.
Fahamu kwa nini bado haupo katika lengo lako.
- Tambua
maarifa na ujuzi wa ziada ambao utahitaji ili kuweza kufikia lengo lako.
Ili kuweza kufanikiwa kukamilisha malengo ambayo hujawahi kuyakamilisha
hapo kabla unahitaji kujifunza na kuwafanya vitu vya tofauti ambavyo
hujwahi kufanya kabla.
- Watambue watu ambao utwahitaji wakusaidie au waungane nawe ili uweze kufikia malengo yako. Kufikia malengo makubwa unahitaji kuwa natimu ya watu wengi wa kukusaidia. Kwa hiyo unahitaji kuwa na ufasaha ni watu wa aina gani hasa unaowahitaji ili uweze kuwa na timu ambayo itakupa msada unaouhitaji.
- Tengeneza
orodha ya maelezo kwa kila kipengele ambavyo nimeanisha hapo juu na uweke
mpangilio katika mfuatano yaani kipi kinaanza na kipi kinafuata na pia ni
muhimu kuwa na kipaumbele. Ni muhimu kujua kipi unahitaji kwanza, kipi ni
muhimu.
Baada ya kukamilisha
hatua hizo saba ni muhimu kufanya kila siku japo kwa udogo sehemu ya kufikia
lengo lako.
0 comments:
Post a Comment