Saturday, 29 October 2016

Namna Bora ya Kuandika Kichwa cha Habari (Title) Katika Makala

Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio!
Rafiki katika moja ya makala zilizopita nilikushirikisha kuhusu jinsi ya kukabili changamoto za uandishi katika blogu .Katika hiyo makala nilieleza kwa undani mambo makuu matatu; jambo la kwanza ni kusoma vitabu, jambo la pili ni kuandika kila siku na jambo la tatu ni kufanya tathmini ya makala unazoandika. Kama hujasoma makala hiyo unaweza kubonyeza maandishi hapa chini kufungua usome kabla hujaendelea.



Katika makala hii ninapenda kukushirikisha changamoto nyingine inayohusiana na kichwa cha habari (title) cha makala husika katika blogu yako.
Kichwa cha habari cha makala ndicho kinachobeba ujumbe mkuu katika makala yako. Kichwa hiki ni muhimu kiwe na sifa zifuatazo:
(a) Kiwe na maneno machache (kifupi) kadiri inavyowezekana.
(b) Kiwe kinavutia au kumhamasisha msomaji kuweza kufungua na kuangalia maarifa yaliyobebwa na kichwa husika.
(c) Kiwe na muundo wa herufi ya kwanza ya kila neno kuwa herufi kubwa.
Faida kubwa unazozipata kwa kichwa cha habari kuwa na sifa hizo ni:
(a) Kupata wasomaji wengi ambao watakuwa wanakufuatilia.
(b) Kuonesha kiwango cha umakini katika uandishi wako.
Kuna njia mbili unazoweza kutumia kuandika kichwa cha habari bora, kifupi na kinachovutia au kuhamasisha wasomaji wako.
(a) Njia ya kwanza ni kuanza kuandika ujumbe na kumaliza na kichwa cha habari.
Katika njia hii unaandika makala yako yote ukiwa umeipangilia kuwa na sehemu kuu tatu; utangulizi (introduction), mada kuu (body) na hitimisho (conclusion).
Baada ya kukamilisha kuandika sehemu zote hizo tatu, unaipitia na kuanza kutafakari maneno machache ambayo yanaweza kubeba ujumbe wote ulioandika.
Faida ya njia hii ni kuwa haikubani wakati wa uandishi kuwa ni mambo gani uyaandike kutokana na kuwa haujaanza na kichwa cha habari ambacho kingekupa mipaka ya vitu gani vya kuandika. Kwa hiyo unakuwa huru zaidi kuweka mawazo na maarifa yako yote kuhusu mada unayoandika.
(b) Njia ya pili ni kuanza kuandika kichwa cha habari na kumaliza na ujumbe.
Njia hii ipo kinyume cha njia (a) niliyoeleza hapo juu. Hapa unaanza na kichwa cha habari ambacho kinakupa mipaka ya vitu vya kuandika maana unakuwa tayari umeshaweka mwongozo. Ni njia ambayo unahitaji kuweka jitihada sana ili kichwa cha habari kiweze kuendana na ujumbe uliomo ndani.
Pamoja na hiyo changamoto rafiki napenda nikushirikishe kifaa cha mtandaoni ambacho kinaweza kukusaidia kupata kichwa cha habari  kizuri na kinachovutia. Nenda katika Google tafuta Portent Content Idea Generator . Ukishafungua tovuti yao unaweza kuweka mada na ukawa unabofya kupata vichwa mbalimbali.
Rafiki unaweza kuwashirikisha wengine kuhusu blogu hii kwa ajili ya kupata maarifa mbalimbali na pia unaweza kubofya hapa ili kuweza kupata makala kila inapowekwa kupitia barua pepe yako.

Related Posts:

  • Namna Bora ya Kugawa Mapato YakoWakati unapopokea mapato/mshahara wako ugawe katika makundi haya 5 : a) Sadaka Kundi hili la fedha utalitumia kwa kufuata imani yako. Mara nyingi huwa ni asilimia kumi ya mapato. b) Matumizi Kundi hili la fedha ni kwa a… Read More
  • Mambo 3 ya Msingi Kuhusu MalengoUnapoweka lengo lolote ni muhimu liwe limejengwa katika misingi ya mambo yafuatayo: Jambo la kwanza: Lengo liwe linahamasisha (inspiring) Jambo la pili: Lengo liwe linaaminika (believable) Jambo la tatu: Lengo… Read More
  • Jinsi ya Kukabili Changamoto za Uandishi Katika Blogu Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio! Pasipo kutegemea lugha gani unaitumia katika uandishi wa makala ambazo unaziweka katika blogu yako, bado suala la uandishi lina cha… Read More
  • Aina Tano (05) za Uwekezaji Zinazoweza Kubadili Maisha Yako Ili kuweza kuwa na utajiri endelevu katika maisha yako na unaojitosheleza ni muhimu ukawa mwekezaji. Uwekezaji upo wa aina nyingi. Hapa ninakuletea aina za uwekezaji unazoweza kuzifanya ili kukuwezesha wewe na wale watu wako… Read More
  • Mambo 13 ya kuzingatia katika kuelekea mafanikio 1. Watu wengi wanofanikiwa sio kwamba wana ujuzi au uwezo kuzidi ambao unao bali ni kiwango cha maarifa walochonacho ndicho kinatofautisha. Ni muhimu kuwa na hamu na kiu kubwa ya kupata maarifa yanayohusu eneo unalotaka … Read More

4 comments: