Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio!
Rafiki makala unazoziandika kila siku ni muhimu zikahifadhiwa katika sehemu salama. Si vema sana kuacha zikawepo pale zilipo tuu kwa sasa na kujiamini kuwa inatosha bila kuwa na sehemu mbadala ambapo unaweza kuzipata tena. Mimi natumia mtandao wa blogger kuhifadhi makala za blogu yangu. Hivi karibuni nilifanya maboresho katika blogu yangu katika muonekano wake , lakini kabla sijafanya maboresho nilihakikisha nimechukua tahadhari kwa kuhifadhi nakala ya makala zangu zote. Hii ilinisaidia pale ambapo sikuridhishwa na muonekano kuweza kurejesha katika hali iliyokuwa mwanzo kabla ya maboresho. Zoezi hili huitwa "backup". Unaweza kulifanya kila siku, wiki au mwezi kutegemeana na kiwango cha maboresho unayoyaweka katika blogu yako.
SOMA : Jinsi ya Kukabili Changamoto za Uandishi Katika Blogu
Hapa nakushirikisha hatua ambazo unapaswa kuzifuata ili kuweza kufanya backup.
(a) Fungua "browser" katika kompyuta yako na uingie katika akaunti yako uliyoitumia kufungulia blogu. Bila shaka akaunti itakuwa ni ya Gmail.
SOMA : Faida Nne (04) Unazopata Ukiwa na Akaunti ya Gmail.
(b) Katika "browser" yako fungua tab nyingine mbele ya hiyo ya hapo juu kipengele (a) kwa kubofya sehemu palipoandikwa "new tab". Baada ya kufunguka "new tab", nenda sehemu ya address na uandike www.blogger.com
(c) Bofya sehemu iliyoandikwa jina unalotumia kwa ajili ya blogu yako. Mfano, kwa upande wangu inasomeka hivi "Stadi za Mafanikio", hii ni kwa sababu jina la blogu yangu ni www.stadizamafanikio.blogspot.com
(d) Katika upande wa kushoto utaona kuna sehemu imeandikwa maneno "Template". Bofya katika maneno hayo. Mara baada ya kubofya utaona aina mbalimbali za template.
(e) Ukiwa bado katika ukurasa huo huo, angalia upande wa kulia juu utaona maneno "Backup/Restore". Bofya katika hayo maneno. Mara baada ya kubofya kutatokea kisanduku kingine kwa juu, bofya sehemu iliyoandikwa maneno "Download full template".
(f) Utaona faili limepakuliwa linaloanzia na neno template ikifuatiwa na namba na itaishia na neno xml. Faili hili linakuwa makala zote ambazo umeziweka katika blogu yako.
SOMA : Jinsi ya Kutumia Kompyuta Yako Kuwa Chanzo cha Intaneti
Baada ya kulipata faili hili linaloishia na xml unaweza kulihifadhi mtandao kwa kutumia barua pepe, au Dropbox. Au unaweza kuhifadhi sehemu ambako unahifadhi data zako za kieletroniki mfano katika flash.
NB:
Hatua hizi huwezi kuzitumia katika mtandao wa WordPress kwa sababu ya tofauti ya kimuundo.
Rafiki unaweza kuwashirikisha wengine kuhusu blogu hii kwa ajili ya kupata maarifa mbalimbali na pia unaweza kubofya hapa ili kuweza kupata makala kila inapowekwa kupitia barua pepe yako
0 comments:
Post a Comment