Tuesday, 18 October 2016

Jinsi ya Kuandaa Tangazo la Semina au Mafunzo

Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio!

Waandaji mbalimbali wa kozi fupi au semina au mikutano huwa na kawaida ya kutuma taarifa zinazoeleza masuala yatakayofundishwa katika mafunzo husika.

Kupitia kiwango cha taarifa anazozituma aliyeandaa mafunzo , unaweza kutambua ni kwa kiasi gani mafunzo husika yatakuwa ya msaada katika kuongeza maarifa yako. Lakini pia itakusaidia kujua umakini na kiwango cha utaalamu wa aliyeandaa mafunzo katika mada atakayoifundisha.

Hapa ninapenda kukushirikisha vipengele ambavyo unahitaji kuvitazama katika taarifa unazotumiwa na aliyeandaa mafunzo. Lakini pia vipengele hivi vinaweza kukusaidia kufahamu mambo ambayo unahitaji kuyaweka ili uweze kueleweka kwa wale wenye uhitaji na mafunzo kipindi ambacho utahitaji kuandaa semina au kozi fupi au mafunzo.

SOMA : Mambo 3 ya Msingi Kuhusu Malengo

(a) Kichwa cha Mafunzo
Hapa unahitaji kuandika mada kuu inayobeba mafunzo yako utakayoyaendesha. Kichwa hiki ni lazima kiwe kifupi, kinachoeleweka, kinachomvutia msomaji ili aweze kufuatilia mafunzo yaliyobebwa na mada husika. Lakini pia kiwe kinaweza kumhamasisha msomaji kuchukua hatua ya kujiunga na mafunzo.

(b) Muda na Mahali
Hapa utaandika idadi ya siku mafunzo yatachukua , muda ambao utakuwa unaanza mafunzo katika siku husika. Ukumbi au eneo ambapo mafunzo yataendeshwa utaueleza hapa ili anayehudhuria aweze kujua namna ya kujipanga. Ikiwa mafunzo yanaendeshwa kwa njia ya mtandao basi unahitaji kusema muda ambao mafunzo yatakuwa katika mtandao unaoutumia. Na kuhusu mahali utataja kama ni kupitia akaunti zao za barua pepe ndipo watapokea mafunzo au kupitia sehemu maalum katika mtandao ambayo utakuwa umeiandaa watakapopatumia kuyapata mafunzo.

(c) Gharama ya Mafunzo
Hapa utaandika ada ambayo mshiriki mmoja mmoja atalipa au kikundi kitalipa kwa ajili ya kugharamia uendeshaji wa mafunzo. Ni vizuri pia umweleze mwanasemina atarajie atapata nini kutokana na ada aliyolipa.


(d) Njia ya Malipo
Hapa utaandika njia mbalimbali ambazo zinaweza kutumika kwa ajili ya kupokea malipo ya ada ya semina. Kwa njia utakayotumia kupokea ada hakikisha inaonesha uthibitisho wa mpokeaji fedha
kuwa ni wewe muandaaji wa semina. Kufanana kwa majina utakayomwelekeza mlengwa wa semina itamjengea ujasiri, kukuamini ,kuona kiwango chako cha umakini na kuweza kuzuia kutapeliwa na watu wasio waaminifu. Lakini pia anayehudhuria mafunzo aweze kutambulika kuwa amelipa ada na itumike kuwa ni njia ya kumpa ruhusa ya kuhudhuria mafunzo

Rafiki unaweza kuwashirikisha wengine kuhusu blogu hii kwa ajili ya kupata maarifa mbalimbali na pia unaweza kubofya hapa ili kuweza kupata makala kila inapowekwa kupitia barua pepe yako.

Related Posts:

  • Unawezaje Kutofautisha TABLET na iPAD? Habari rafiki, Kutokana na maendeleo makubwa yanayotokea katika teknologia kumekuwa na vifaa vya aina mbalimbali vinatengenezwa ili kusaidia kwanza  kuendana na kasi ya ukuaji katika teknologia lakini pili kurahisha ut… Read More
  • Tafsiri Sahihi ya Tarehe Zinazoandikwa Katika Bidhaa Habari rafiki, Mwili wa binadamu hutumia bidhaa mbalimbali za afya. Kutegemeana na namna ambayo inatumika katika mwili wa binadamu tunaweza kuzigawa hizi bidhaa katika makundi mawili. 1. Kundi la kwanza linahusisha b… Read More
  • Jinsi ya Kutumia Kompyuta Yako Kuwa Chanzo cha Intaneti Habari rafiki! Katika makala ya leo ninapenda kukushirikisha namna ya "kushare" intaneti kutoka kwenye kompyuta na kwenda kwenye vifaa vingine vyenye uwezo wa kupokea intaneti. Kompyuta yoyote ambayo ina kifaa kinachoitwa "… Read More
  • Maana za Vibao Vya Namba Za Magari (Plate Number) Habari rafiki! Katika kila gari kuna sehemu mbili ambapo huwekwa vibao vyenye namba kwa ajili ya kulitambulisha gari husika. Vibao hivi huwekwa mbele na nyuma ya gari. Katika lugha ya kiingereza huitwa "plate number". Katik… Read More
  • Utaratibu Sahihi wa Uandishi wa Saa Habari rafiki! Kumekuwa na changamoto katika kujua namna sahihi ya uandishi wa muda kutoka katika saa.Saa ni kifaa ambacho kinatumika kusoma muda ambao huwa katika mpangilio wa kuanza na saa, kisha kufuata dakika na kuishia… Read More

2 comments: