Kutegemeana mtu na mtu kuna tofauti kati ya vitu vinavyoleta bugudha wakati unafanya jambo. Mfano kuna mtu hawezi kufanya kazi katika mazingira yenye kelele au wakati redio inazungumza wakati huo huo kuna mwingine anaweza kufanya katika mazingira ambayo redio inazungumza.
Katika ulimwengu huu wa sasa ambao umetawaliwa na maendeleo ya sayansi na teknolojia kuna aina nyingi za bugudha zimeongezeka pia, mfano kwa wale wanaoutumia kompyuta kuna bugudha kama vile michezo (games), mitandao ya kijamii, barua pepe, utafutaji wa kitu katika tovuti (web search) hata ujumbe katika simu (SMS- chatting)
Unaweza kufikiri kwamba kwa kuanza kuchukua hatua ya kulitekeleza basi ndio suluhisho la wewe kuelekea kukamilisha jambo husika. Unahitaji kuwa makini kwa kufanya maandilizi ya kutosha namna ambavyo utashughulikia bugudha, vizuizi na vikwazo katika harakati zako za kutimiza malengo yako.
Njia rahisi ni kuondoa kila bugudha unayoifahamu itaathiri utendaji wako mapema kabla hujaanza kufanya jambo, mfano kuiweka simu katika hali ya ukimya (silent mode) , kuondoka katika mitandao ya kijamii wakati unatekeleza jambo (facebook, twitter n.k) na vitu vingine vyote vinavyoweza kuondoa umakini wako katika kazi husika (magazeti, majarida n.k)
Lakini sio mara zote tunaweza kukisia bugudha, kikwazo au kizuizi tunachoweza kukutana nacho katika harakati za kufikia malengo, kwa zile zote ambazo tumeshindwa kuzikisia na kuziwekea mikakati mapema tunaweza kuzishughulikia kwa kujua kusudi kubwa la kile unachokitekeleza. Kusudi likiwa kubwa kuliko kikwazo, bugudha au kizuizi unapata nguvu na sababu ya kusonga mbele
0 comments:
Post a Comment