Unapofanya maamuzi ya kutaka kufanikiwa unahitaji kufanya mabadiliko ya msingi (fundamental change).Ili kufanya mabadiliko unahitaji namna nzuri ya kuelewa sehemu ambayo unatakiwa kuanzia.
Sehemu iliyo bora kabisa ya kuanza ni kwa kujiuliza maswali. Kwa nini ujiulize maswali? Kwa sababu karibia matatizo ya aina yoyote yanaweza kupatiwa ufumbuzi kwa kuuliza maswali sahihi ya kutosha.
a) Ninahitaji nini?
b) Nini machaguo yangu?
c) Mawazo gani ninayo?
d) Nini wajibu wangu?
e) Nawezaje kuwaza tofauti kuhusu jambo husika?
f) Watu wengine wanafikirije, wanahisije na wanahitaji nini?
g) Kitu gani napoteza au nakikwepa?
h) Nini naweza kujifunza kutoka kwa huyu mtu/hali iliyotokea/kosa nililofanya/mafanikio niliyoyapata?
i) Ni hatua zipi za kutiliwa maanani/kupewa kipaumbele?
j) Maswali gani nijiulize mwenyewe/niwaulize wengine?
k) Nawezaje kubadili jambo husika kuweza kupata ushindi pande zote mbili?
l) Kipi kinawezekana?
Kuuliza maswali hayo yanasaidia kuliangalia tatizo/jambo kwa undani na kwa kadiri unavyoweza kuliangalia tatizo/jambo kwa undani zaidi ndivyo unavyoweza kutumia ujuzi/maarifa uliyonayo na mikakati iliyo bora kufanya mabadiliko unayoyahitaji
0 comments:
Post a Comment