Kwa kila unayemuongoza unahusiana naye kwa kulingana na mojawapo kati ya ngazi hizi tano. Ngazi ya chini kabisa ni ngazi ya kwanza na ngazi ya juu kabisa ni ngazi ya tano:
1. Ngazi ya kwanza ambayo tunaanza nayo katika safari ya uongozi ni kupewa nafasi ya kuongoza (leadership position).
Katika nafasi hii watu walio chini yako wanakufuata kwa sababu ya nafasi yako hawaendi zaidi ya uwezo walionao na muda walio nao.
2. Ngazi ya pili inajengwa katika misingi ya mahusiano (relationship) na wale unaowaongoza. Watu unaowaongoza wanakufuata sio kwa sababu ya nafasi yako ya uongozi kama ngazi ya kwanza bali kwa sababu wanapenda namna unavyohusiana nao katika kuwaongoza. Hapa unakuwa umewapa nafasi ya kukusikiliza, kuona unachofanya na kujifunza.
3. Ngazi ya tatu inajengwa katika misingi ya uzalishaji/ufanisi.
Unaowaongoza watu kwa kuwa mfano katika uzalishaji na ufanisi katika mambo unayoyafanya. Hii itawasaidia kufanya kile wanachokiona na hivyo utakuwa umewavutia kuzalisha na kuweka mkazo katika ufanisi. Hapa ndipo matatizo mengi katika sehemu unayoongoza yanaweza kushughulikiwa.
4. Ngazi ya nne inajengwa katika misingi ya kuwaendeleza wale unaowaongoza ili kuongeza uwezo wao wa ufanisi/uzalishaji (developing people). Na hii itachangiwa kwa kuchagua watu sahihi na kuwaweka sehemu sahihi ambazo zinaendena na uwezo wao
5. Ngazi ya tano inajengwa katika misingi ya heshima. Umefanya mengi yanayowagusa wale unaowaongoza na hivyo kusababisha wakufuate. Wanakufuata kwa sababu ya mambo mengi uliyoyafanya kwa ubora kwa muda mrefu. Hii ni ngazi ya juu kabisa katika uongozi
0 comments:
Post a Comment