Ni asili yetu kuwa na matumaini mema juu ya jambo fulani ambayo yamepitiliza uhalisia. Mfano tunadhani kuwa tutafanya mambo mengi kwa muda mchache kuliko inavyotakiwa kiuhalisia au kudhani jambo unalolifanya litachukua muda mchache kufanyika kuliko muda halisi ambao jambo husika linaweza kuchukua.
Kimsingi huwa tunasahau kufikiri katika uhalisia muda ambao jambo litachukua kwa kuzingatia uzoefu wetu wa awali. Tunaweka mkazo (focus) katika jambo hilo moja na kusahau kuzikusanya taarifa mbalimbali zilizosambaa ambazo zimetokana na uzoefu wetu katika utekelezaji wa jambo linalofanana au linaloendana nalo. Taarifa hizi zingetusaidia kuweka uhalisia na hivyo kutupatia uwekaji mipango bora iliyo halisi.Hii hutupatia matokeo ya uwekaji mpango hafifu au mbovu.
0 comments:
Post a Comment