Tukio lolote linapotutokea bila kujali ni zuri au baya katika akili kuna mambo matatu huwa yanaendelea:
a) Fikra (thoughts)
b) Hisia (feelings)
c) Hali (circumstances)
Bila kujali hali ya tukio mambo hayo 3 ndiyo yanayotuongoza kwa sehemu kubwa namna tutakavyochagua jinsi tutaitikia (kurespond) katika tukio husika.
Mara nyingi husahaulika kuwa hatua ya utekelezaji katika matendo hufuata baada ya hatua ya kuuliza maswali.
Kwa nini hatua ya kuuliza maswali itangulie kabla ya hatua ya utekelezaji katika matendo? Umuhimu wa kuuliza maswali upo katika:
a) Kukusanya taarifa za kina
b) Kujenga uelewa na kujifunza
c) Kujenga, kuboresha na kuendeleza mahusiano
d) Kufafanua na kuthibitisha ulichosikiliza/ulichokiona/ulichokipokea
e) Kuchochea ubunifu na uvumbuzi
f) Kujenga ushirikiano
g) Kuweka malengo na kutengeneza mpango kazi
h) Kuchunguza, kugundua na kutengeneza nafasi/fursa mpya
Hivyo maswali tunayojiuliza wenyewe hutupatia fursa kwa ajili ya kufikiri na kuwezekana kwa namna ya kipekee kwa jambo husika tofauti na vile kabla hatujajiuliza hayo maswali.
Na jinsi utakavyoweza kuuliza maswali kwa ufasaha/kina zaidi ndivyo utaweza pia kupata matokeo makubwa zaidi