Saturday, 14 March 2015

Umakini Unaouhitaji Kabla Hujaanza Kufanya Lolote

Kutegemeana mtu na mtu kuna tofauti kati ya vitu vinavyoleta bugudha wakati unafanya jambo. Mfano kuna mtu hawezi kufanya kazi katika mazingira yenye kelele au wakati redio inazungumza wakati huo huo kuna mwingine anaweza kufanya katika mazingira ambayo redio inazungumza.

Katika ulimwengu huu wa sasa ambao umetawaliwa na maendeleo ya sayansi na teknolojia kuna aina nyingi za bugudha zimeongezeka pia, mfano kwa wale wanaoutumia kompyuta kuna bugudha kama vile michezo (games), mitandao ya kijamii, barua pepe, utafutaji wa kitu katika tovuti (web search) hata ujumbe katika simu (SMS- chatting)

Unaweza kufikiri kwamba kwa kuanza kuchukua hatua ya kulitekeleza basi ndio suluhisho la wewe kuelekea kukamilisha jambo husika. Unahitaji kuwa makini kwa kufanya maandilizi ya kutosha namna ambavyo utashughulikia bugudha, vizuizi na vikwazo katika harakati zako za kutimiza malengo yako.

Njia rahisi ni kuondoa kila bugudha unayoifahamu itaathiri utendaji wako mapema kabla hujaanza kufanya jambo, mfano kuiweka simu katika hali ya ukimya (silent mode) , kuondoka katika mitandao ya kijamii wakati unatekeleza jambo (facebook, twitter n.k) na vitu vingine vyote vinavyoweza kuondoa umakini wako katika kazi husika (magazeti, majarida n.k)

Lakini sio mara zote tunaweza kukisia bugudha, kikwazo au kizuizi tunachoweza kukutana nacho katika harakati za kufikia malengo, kwa zile zote ambazo tumeshindwa kuzikisia na kuziwekea mikakati mapema tunaweza kuzishughulikia kwa kujua kusudi kubwa la kile unachokitekeleza. Kusudi likiwa kubwa kuliko kikwazo, bugudha au kizuizi unapata nguvu na sababu ya kusonga mbele

Related Posts:

  • Mambo ya Kuzingatia UnaposhirikianaUnapoamua kushirikiana na mtu mwingine ni vizuri muweke msingi katika masuala 3 yafuatayo ili kuepuka kukatishwa tamaa kwa kutokuwa na ulinganifu wa matarajio na matokeo Jambo la kwanza: Fahamu kila mshirika nini atamiliki (… Read More
  • Usipuuze TatizoMatatizo mengi kamwe hayatatuliwi au hayadhibiti kwa ufanisi kutokana na kutoyapa uzito wa kutosheleza. Hakuna tatizo ambalo halina umuhimu kiasi kuwa hatuhitaji kujali kuhusu hilo tatizo. Mfano kwa mwanafunzi inawezekena hap… Read More
  • Swali la WikiNi kitu gani ungethubutu kukifanya ikiwa kama umehakikishiwa mafanikio kupitia kukifanya hicho kitu? What would you dare to try to do if you were guaranteed to succeed?… Read More
  • Usifanye Kosa Hili Katika BiasharaUnapoamua kuchagua kuwa utashirikiana na mtu mwingine kufanya biashara ya ndoto yako, usitumie kigezo cha huyo mshirika kuwa ni mmoja wa wanafamilia wako au ni mmoja wa marafiki zako wa karibu sana, utakuwa umejiingiza katika… Read More
  • Fanya Haya ili Ukue1. Usitamani mambo yangekuwa marahisi, tamani ungekuwa bora mno Don't wish it were easier; wish you were better 2. Usitamani ungekutana au ungekuwa na matatizo machache,tamani ungekuwa na ujuzi zaidi Don't wish for less prob… Read More

0 comments:

Post a Comment