Unapofanya maamuzi ya kutaka kufanikiwa unahitaji kufanya mabadiliko ya msingi (fundamental change).Ili kufanya mabadiliko unahitaji namna nzuri ya kuelewa sehemu ambayo unatakiwa kuanzia.
Sehemu iliyo bora kabisa ya kuanza ni kwa kujiuliza maswali. Kwa nini ujiulize maswali? Kwa sababu karibia matatizo ya aina yoyote yanaweza kupatiwa ufumbuzi kwa kuuliza maswali sahihi ya kutosha.
a) Ninahitaji nini?
b) Nini machaguo yangu?
c) Mawazo gani ninayo?
d) Nini wajibu wangu?
e) Nawezaje kuwaza tofauti kuhusu jambo husika?
f) Watu wengine wanafikirije, wanahisije na wanahitaji nini?
g) Kitu gani napoteza au nakikwepa?
h) Nini naweza kujifunza kutoka kwa huyu mtu/hali iliyotokea/kosa nililofanya/mafanikio niliyoyapata?
i) Ni hatua zipi za kutiliwa maanani/kupewa kipaumbele?
j) Maswali gani nijiulize mwenyewe/niwaulize wengine?
k) Nawezaje kubadili jambo husika kuweza kupata ushindi pande zote mbili?
l) Kipi kinawezekana?
Kuuliza maswali hayo yanasaidia kuliangalia tatizo/jambo kwa undani na kwa kadiri unavyoweza kuliangalia tatizo/jambo kwa undani zaidi ndivyo unavyoweza kutumia ujuzi/maarifa uliyonayo na mikakati iliyo bora kufanya mabadiliko unayoyahitaji
Unahitaji Wastani wa Maswali 12 Kufanikiwa
Related Posts:
Je, Unafahamu Kifaa Kinachoitwa Mouse? Habari rafiki, Kompyuta huundwa na vifaa vilivyogawanyika katika makundi makuu matatu. Makundi haya yamewekwa kutegemeana na kazi zinazotekelezwa na vifaa vinavyoundwa kundi husika. 1. Kundi la kwanza linajumuisha vi… Read More
Mfumo Pekee Utakakokusaidia Kukidhi Mahitaji ya Mteja Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio! Suala la kukidhi mahitaji ya mteja unaowahudumia linakwenda sambamba na utoaji wa huduma bora kwa mteja. Kiwango cha kukidhi mahita… Read More
Uchambuzi wa Kitabu " TOUGH TIMES NEVER LAST BUT TOUGH PEOPLE DO" Robert H Schuller ni mwandishi wa kitabu cha "TOUGH TIMES NEVER LAST BUT TOUGH PEOPLE DO" . Katika kitabu hiki mwandishi anatupa mbinu za kutumia tunapokuwa tunapitia vipindi vigumu katika maisha yetu ya kila siku. Hapa nina… Read More
Hatua Nne (04) Katika Uandishi wa Blogu Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio! Rafiki unapoanza kuandika makala katika blogu kuna changamoto mbalimbali ambazo utakutana nazo. Changamoto hizi zinatokana na kuwa … Read More
Matumizi Bora ya Siku za Wikiendi na Sikukuu Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio! Rafiki katika wiki tuna siku saba, kati ya siku hizi kuna baadhi ya watu kutegemea na ratiba ya majukumu pale anapofanya kazi anaku… Read More
0 comments:
Post a Comment