Saturday, 14 March 2015

Jenga Mtazamo Huu Unapouliza Maswali

Tukio lolote linapotutokea bila kujali ni zuri au baya katika akili kuna mambo matatu huwa yanaendelea:

a) Fikra (thoughts)
b) Hisia (feelings)
c) Hali (circumstances)

Bila kujali hali ya tukio mambo hayo 3 ndiyo yanayotuongoza kwa sehemu kubwa namna tutakavyochagua jinsi tutaitikia (kurespond) katika tukio husika.

Mara nyingi husahaulika kuwa hatua ya utekelezaji katika matendo hufuata baada ya hatua ya kuuliza maswali.

Kwa nini hatua ya kuuliza maswali itangulie kabla ya hatua ya utekelezaji katika matendo? Umuhimu wa kuuliza maswali upo katika:

a) Kukusanya taarifa za kina
b) Kujenga uelewa na kujifunza
c) Kujenga, kuboresha na kuendeleza mahusiano
d) Kufafanua na kuthibitisha ulichosikiliza/ulichokiona/ulichokipokea
e) Kuchochea ubunifu na uvumbuzi
f) Kujenga ushirikiano
g) Kuweka malengo na kutengeneza mpango kazi
h) Kuchunguza, kugundua na kutengeneza nafasi/fursa mpya

Hivyo maswali tunayojiuliza wenyewe hutupatia fursa kwa ajili ya kufikiri na kuwezekana kwa namna ya kipekee kwa jambo husika tofauti na vile kabla hatujajiuliza hayo maswali.
Na jinsi utakavyoweza kuuliza maswali kwa ufasaha/kina zaidi ndivyo utaweza pia kupata matokeo makubwa zaidi

Related Posts:

  • Mambo ya Kuzingatia UnaposhirikianaUnapoamua kushirikiana na mtu mwingine ni vizuri muweke msingi katika masuala 3 yafuatayo ili kuepuka kukatishwa tamaa kwa kutokuwa na ulinganifu wa matarajio na matokeo Jambo la kwanza: Fahamu kila mshirika nini atamiliki (… Read More
  • Salamu ya Mwezi AprilJambo la kwanza Simamia mawazo na shughuli zako kwa ufanisi wa hali ya juu Jambo la pili Kila unachokifanya kifanye kiwe na muonekano tofauti na ambavyo wengine wamezoea kukifanya kwa kuhakikisha kinaleta manufaa kwako pamoj… Read More
  • Mbinu ya Kuishi Kila SikuAnza na kuimaliza siku vizuri kadiri inavyowezekana Begin and end each day properly… Read More
  • Swali la WikiNi kitu gani ungethubutu kukifanya ikiwa kama umehakikishiwa mafanikio kupitia kukifanya hicho kitu? What would you dare to try to do if you were guaranteed to succeed?… Read More
  • Usifanye Kosa Hili Katika BiasharaUnapoamua kuchagua kuwa utashirikiana na mtu mwingine kufanya biashara ya ndoto yako, usitumie kigezo cha huyo mshirika kuwa ni mmoja wa wanafamilia wako au ni mmoja wa marafiki zako wa karibu sana, utakuwa umejiingiza katika… Read More

0 comments:

Post a Comment