Tuesday, 11 October 2016

Maana za Vibao Vya Namba Za Magari (Plate Number)

Habari rafiki!
Katika kila gari kuna sehemu mbili ambapo huwekwa vibao vyenye namba kwa ajili ya kulitambulisha gari husika. Vibao hivi huwekwa mbele na nyuma ya gari. Katika lugha ya kiingereza huitwa "plate number". Katika makala ya leo ninakushirikisha namna ya kupata ujumbe unaowasilishwa na pindi unaposoma kibao husika cha namba ya gari.


Aina za Vibao vya Namba za Magari
1. Kibao chenye rangi ya njano na namba inayoanza na herufi T
Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika limesajiliwa kutumika kwa ajili ya shughuli binafsi. Kwa kiingereza inasemwa "private use". Magari yenye vibao hivi hayaruhusiwi kutumika kwa ajili ya biashara.
2. Kibao chenye rangi nyeupe na namba inayoanza na herufi T
Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika limesajiliwa kwa ajili ya matumizi ya biashara. Kwa kiingereza inasemwa "commercial use". Mfano mzuri daladala au basi za kubeba abiria na taxi.
3. Kibao chenye rangi ya njano na namba haianzi na herufi T
Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika linamilikiwa na taasisi ya umma au serikali. Hapa kuna makundi yafuatayo:
(a) SU - shirika la umma , mfano vyuo vikuu vya serikali
(b) SM - Serikali za Mitaa , mfano ni halmashauri
(c) STK,STL,STJ - serikali, mfano ni wizara
4. Kibao chenye rangi nyekundu na namba inayoanza na herufi DFP au DFPA
Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika limetolewa kwa ajili ya matumizi ya miradi inayofadhiliwa na wafadhili kutoka nje ya nchi.
5. Kibao chenye rangi ya bluu na namba inayoanza na herufi T kufuatiwa na namba na kisha herufi CD
Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika linamilikiwa na moja ya shirika la umoja wa mataifa. Mfano shirika la Afya Duniani (WHO).
6. Kibao chenye rangi ya kijani na namba inayoanza na herufi T kufuatiwa na namba na kisha herufi CD
Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika linamilikiwa na ofisi za ubalozi wa nchi fulani. Mfano ubalozi wa Ufaransa.
7. Kibao chenye rangi nyeusi na namba zimeandiwa kwa rangi ya njano
Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika linamilikiwa na Jeshi la  Polisi. Namba hizi huwa na herufi PT
8. Kibao chenye rangi nyeusi na namba zimeandiwa kwa rangi ya njano
Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika linamilikiwa na Jeshi la Wananchi (JW). Namba hizi huwa na herufi JW.
9. Kibao chenye rangi ya kijani na namba zenye herufi MT
Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika linamilikiwa na Jeshi la Magereza.
Unaweza kubofya hapa ili kuweka barua pepe yako au rafiki yako ambaye unapenda makala hizi azipate moja kwa moja katika barua pepe.

Related Posts:

  • Namna Bora ya Kugawa Mapato YakoWakati unapopokea mapato/mshahara wako ugawe katika makundi haya 5 : a) Sadaka Kundi hili la fedha utalitumia kwa kufuata imani yako. Mara nyingi huwa ni asilimia kumi ya mapato. b) Matumizi Kundi hili la fedha ni kwa a… Read More
  • Mambo 17 niliyojifunza katika kitabu cha SPEED WEALTH Mambo niliyojifunza kutoka katika kitabu cha SPEED WEALTH kilichoandikwa na T Harv Eker 1. Ili uweze kufanikiwa na kuchomoza katika mafanikio unahitaji kumiliki biashara, ukitumia njia ya ajira ya kuwa umesoma ,umepata… Read More
  • Mambo 3 ya Msingi Kuhusu MalengoUnapoweka lengo lolote ni muhimu liwe limejengwa katika misingi ya mambo yafuatayo: Jambo la kwanza: Lengo liwe linahamasisha (inspiring) Jambo la pili: Lengo liwe linaaminika (believable) Jambo la tatu: Lengo… Read More
  • Mambo 13 ya kuzingatia katika kuelekea mafanikio 1. Watu wengi wanofanikiwa sio kwamba wana ujuzi au uwezo kuzidi ambao unao bali ni kiwango cha maarifa walochonacho ndicho kinatofautisha. Ni muhimu kuwa na hamu na kiu kubwa ya kupata maarifa yanayohusu eneo unalotaka … Read More
  • Falsafa ya Jinsi ya Kuishi Maisha ya MafanikioMambo ya msingi niliyojifunza kutoka katika kitabu cha My Philosophy for Successful Living kilichoandikwa na Jim Rohn. Hiki ni kitabu kifupi sana ambacho ukikisoma utagundua muda uliotumia ni uwekezaji bora ambao umefanya kat… Read More

24 comments:

  1. Nzuriii hii nimeipenda..👏👏

    ReplyDelete
  2. Kuna ambazo zina kibao cha kijani namba zinaanza RAC halafu zinafuatia namba, hizo zina maana gani?

    ReplyDelete
  3. Kuna gari plate number yake ina nyota tatu (***)

    ReplyDelete
  4. Hii ni nzuri.... itapendeza pia tukijua kirefu cha STL, STK,STJ...

    ReplyDelete
  5. Vip huhusu kibao cha rangi nyeusi na namba zake rangi nyeupe na nyingine rangi ya njano na inaanza na J harafu namba na nyingine njano na inaanza heruf M harafu inafuatiwa na namba vip nayo imekaaje?

    ReplyDelete