Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio!
Robin Sharma ni mwandishi wa kitabu cha MEGALIVING, 30 DAYS TO PERFECT LIFE. Katika kibao hiki Robin anaeleza namna ambavyo unaweza kuyabadilisha maisha yako kwa kutumia uwezo wako na kuyafanya kuwa bora. Hapa nakushirikisha mambo ambayo nimejifunza katika kitabu hiki.
1. Hakuna shaka Unayo nguvu ya ajabu inayoweza kukuwezesha kufanikiwa katika lolote ulilolipanga/unalotazamia
2. Kuwa bora kwa kadiri inavyowezekana
3. Ukitaka kuweza kuingoza familia, kampuni ni lazima uanze kujiongoza / kujitawala wewe mwenyewe kwanza
4. Hakuna makosa katika maisha bali kuna masomo ya kujifunza kutoa fursa ya kukua na kupanda ngazi katika njia ya mafanikio
5. Usiwe mfungwa wa maisha yako yaliyopita bali uwe mbunifu/msanifu anayeunda maisha ya baadae
6. Mawazo yako ya leo yanatengeneza ndoto zako za kesho
7. Ni muhimu ukaanza kujiendeleza mwenyewe kwa kutengeneza uwezo wa akili na nidhamu kubwa mno katika maisha yako
8. Mafanikio ili yaonekane nje ni lazima yaanzie ndani kwako
9. Kitu chochote akili ya binadamu kinachoweza kukiwaza na kukiamini kinaweza kukipata
10. Yatambue mawazo uliyonayo yanayokuletea kikwazo na uyaondoe kabisa katika ufahamu na badala yake uweke mawazo yanayokupa nguvu, tumaini, hamasa pamoja na utimizaji wa ndoto zako
11. Ukiweza kutawala akili yako, unaweza kutawala maisha yako na ukiweza kutawala maisha yako utaweza kutawala hatima ya maisha yako (destiny)
12. Ukiendelea kufanya mambo yale yale kila siku utapata matokeo yale yale kila siku
13. Ushindi mdogo mdogo ndio hupelekea ushindi mkubwa
14. Kuwa na ari ya kuboresha kila siku maeneo ya msingi katika maisha yako na kuwa bora kadiri inavyowezekana
15. Hakuna kitu kinachoweza kumkwamisha mtu ambaye amekataa kukwamishwa
16. Watu waliofanikiwa daima wana kiu ya mawazo mapya na maarifa mapya
Soma Makala Hii Inayohusiana : Uchambuzi wa Kitabu " LUNCHTIME TRADER"
17. Mambo 3 muhimu kuhusu akili yako
a) Kujifunza namna ya kuiongoza/kuiendesha akili yako kama mshindi
b) Akili yako Ina uwezo wa kufanya mambo makubwa mazuri ya kushangaza Kama utairuhusu kufanya hivo
c) Vizuizi ni vile tu ambavyo unajiwekea we mwenyewe
18. Ngazi ya mafanikio yako inategemea kile unachofikiria kila sekunde, kila dakika kila siku
19. Ukitaka kubadili maisha yako unahitaji kubadili aina ya mawazo unayoweka akilini mwako
20. Unawajibika kwa kile unachofikiria Unao uwezo wa kuamua kuacha na kuondoa kufikiri hasi.
21. Taswira zetu binafsi zinazopita katika akili zetu ndo zinaamua sisi kuwaje
22. Unaweza kufanikiwa katika chochote ikiwa Una taarifa sahihi
23. Kila mtu mwenye mafanikio ni kwa sababu amekuwa na nidhamu ya kutosha
24. Kuwa na matarajio mazuri na siku zote uwaze mambo makubwa
25. Vikwazo vyote vinavyokuchelewesha kufikia mafanikio vinaweza kubadilishwa kwa kuwa na mikakati sahihi
26. Inatakiwa kuwaza chanya ili kuweza kufanikisha kisichowezekana na kuweza kuwa vile unavyotakiwa kuwa
27. Hatua 7 za kufikia malengo yako:
a) Fahamu nini unachokitaka
b) Weka malengo sahihi na tarehe ya mwisho ya kuyafikia pamoja na mikakati
c) Kuhusu malengo yako yatawale mawazo yako
d) Weka msukumo kwa ajili ya faida yako
e) Tafuta network ya watu watakaokusapoti
f) Kumbuka kanuni ya 21
g) Furahia na ujipatie tuzo
28. Tumia muda wako vizuri
29. Unaweza kujifunza kitu kutoka kwa kila mtu
30. Hekima inayopatikana kwa kujifunza huwa haisahauliki
31. Unahitaji kulala si zaidi ya masaa 6, jifunze kuamka mapema kwa siku 21 mfululizo na utakuwa umeshajenga tabia hiyo
32. Tenga lisaa limoja kila siku asubuhi kwa ajili ya maendeleo binafsi (personal development)
33. Ubongo wa binadamu ukishatanuka kwa kupata wazo jipya hauwezi kurudi katika size yake ya swali
34. Tumia kila jumapili jioni kupangilia namna ambavyo unataka wiki yako iende mfano vitabu unavyotaka kusoma, kazi utakazozifanya
35. Kile unachokiwekea mkazo (focus) ndicho utalachokipata
36. Bakia katika lengo na sio matokeo
37. Kuwa mtu mwenye nidhamu ya hali ya juu ya kutunza muda
38. Njia ya kujisomea ni njia yenye nguvu ya kujizolea miaka mingi ya uzoefu ndani ya muda mchache wa kujifunza
39. Jipatie tuzo hata kwa mafanikio madogo
40. Kuwa mkweli na mvumilivu
41. Usikatishwe tamaa pale majibu yanapochelewa kujitokeza
42. Tumia shajara (diary) kupima maendeleo yako na kunakili mawazo unayopata kila wakati
43. Jaribu kufunga (fasting) siku moja kila baada ya wiki 2. Na ule matunda na juice ya matunda tuu.
44. Samehe hata kama mazingira ni magumu
45. Tazama kila fursa Kama nafasi ya kujifunza
46. Kunywa kikombe cha maji ya moto kabla hujaanza kuhutubia ili kupata stamina nzuri ya kuhutubu
47. Kuwa na ujasiri, wahamasishe wengine kupitia matendo yako na pia uwe unawafikiria wengine
48. Usiulize ulimwengu utakufanyia nini bali jiulize utaufanyia nini ulimwengu, kuwa na lengo la kutoa huduma ulimwenguni
49. Nenda katika semina mbalimbali kwa ajili ya kupata uzoefu wa watu mbalimbali katika Yale unayotaka kufanya ambayo wengine wametumia muda mwingi kujifunza au kuyajua
50. Tembea kwa muda wa nusu saa kila unapomaliza kula chakula cha usiku
51. Uwe na kiasi kwa kila unachokifanya usipitilize
52. Katika vitabu vya maendeleo binafsi, chukua kile unachokihitaji na ambacho kinaweza kufanyika kwako na kile ambacho hakiendani nawe kiache
53. Siku iliyotumiwa vizuri huleta usingizi mzuri
54. Tafuta mshauri ambaye atakuongoza katika maendeleo yako
55. Orodhesha madhaifu yako yote na tafuta mbinu za kuboresha
56. Usilalamike
57. Kuwa na huruma, mwenye kufikiria wengine na mwenye adabu
58. Watu waliofanikiwa hufikiri mara tatu kabla ya kutamka neno
59. Zungumza mambo mazuri tuu kuhusu watu
60. Fanya mambo yawe mepesi kwa watu
61. Jifunze namna ya kupangilia muda wako
62. Mambo ambayo tusiyoyapenda huwa yanaendelea kuja na yale tunayoyapenda hayaji tunapotaka kuyakumbuka
63. Andaa mpango wa kina wa kifedha wa miaka kadhaa ambao utaufata
64. Furahi kwa kile ulichonacho
65. Jenga tabia ya kutoa zaidi kuliko kupokea
66. Usiongee wakati unasikiliza
67. Watu waliofanikiwa wana kiu na shauku kubwa ya maarifa
68. Weka mkazo katika malengo yako na soma yale mambo ambayo ni ya manufaa tu kwako
69. Kile ambacho unakitafuta utakipata
70. Tumia dakika 10 kila siku kabla hujalala kujitathmini
71. Fikiria mambo mazuri ambayo umeweza kuyafanya na yale mabaya ili ujifunze kwa ajili ya kukua na kusonga mbele
72. Kabla hujatoka kitandani hakikisha unasema maneno chanya au unafanya maombi kwa ajili ya kuifanya siku yako ya mafanikio
73. Kuwa mbunifu ambae unampa maoni yako 10 kila wiki msimamizi wako wa kazi kwa ajili ya kuboresha kazi mnayofanya
74. Kila siku fanya mambo mawili ambayo hupendi kuyafanya hata Kama ni madogo we fanya tuu
75. Lala kidogo, tumia fedha kidogo ,fanya kazi zaidi
Goodluck Moshi
Author
StadizaMafanikio
Read, Apply and Share!