Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio!
Rafiki katika maisha watu wamekuwa wakitawaliwa na hofu, wameipa hofu nafasi kubwa ya kutawala maisha yao. Hofu huzaa malalamiko kunakosababishwa na hali ya kutoridhika na hatua au hali uliyonayo. Lakini ukifanya ulinganisho kati ya vile ulivyonavyo na walivyonavyo wengine,utagundua unahitaji kuwa na moyo wa shukrani.
Utafiti unaonesha asilimia tisini ya mambo au vitu katika maisha yetu ni sahihi au sawa (right), wakati asilimia kumi ya mambo au vitu katika maisha ndiyo haviko sahihi (wrong). Ikiwa unataka kuwa na furaha hakikisha unaegemea zaidi katika upande wa mambo yaliyo sahihi (asilimia tisini) kuliko yasiyo sahihi (asilimia kumi). Na ikiwa unataka kuishi maisha ya masikitiko au huzuni hakikisha unachagua kuegemea zaidi katika upande wa mambo yasiyo sahihi (asilimia kumi) kuliko yaliyo sahihi (asilimia tisini).
Soma Makala Hii Inayohusiana : Mambo Matano (05) Yaliyojificha Katika Mafanikio Yako
Ni mara chache sana tunatumia wakati kufikiri yale ambayo tunayo, badala yake utakuta tunawaza kuhusu yale ambayo hatuna. Usilalamike kama vile upo wewe peke yako ndiye mwenye matatizo au ambaye hana. Ukichunguza utagundua una mambo mengi sana ya kukufanya uwe na shukrani kutokana na kuwa na upekee hasa ukilinganisha na wengine ambao hawana vitu ulivyonavyo. Hapa rafiki ninapenda kukusisitiza kuamua kwa kukusudia kuangalia upande wa uzuri kuliko upande wa ubaya wa kila tukio linalokuja katika maisha yako.
Rafiki napenda kusisitiza usihesabu idadi ya matatizo uliyonayo anza kuhesabu mambo mazuri uliyonayo, hii itakusaidia kuondoa hofu ya kuishi.
Rafiki unaweza kuwashirikisha wengine kuhusu blogu hii kwa ajili ya kupata maarifa mbalimbali na pia unaweza kubofya hapa ili kuweza kupata makala kila inapowekwa kupitia barua pepe yako.
0 comments:
Post a Comment