Monday, 21 November 2016

Tofauti Ya Matumizi Ya Copy na Cut

Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio!

Katika matumizi ya kompyuta kila siku kuna operations ambazo hufanywa mara kwa mara ili kukuwezesha kukamilisha kazi (task) uliyokuwa unaifanya. Kwa bahati nzuri teknologia hii imeenea sana mpaka kugusa pia simu za mkononi.

Rafiki moja ya operations ambazo hufanyika mara kwa mara katika kompyuta ni cut na copy. Katika makala hii napenda kukuelezea kwa kina tofauti ya hizi operations.

(a) Cut
Operation hii imebeba lengo la kuondoa bila kuacha kitu kutoka katika eneo la awali ambapo kitu kinatolewa (source) na  kwenda eneo lingine ambalo limekusudiwa (destination).

Ikiwa cut itatumika katika maneno , sharti kwanza maneno yawekewe kivuli (highlight), alafu ndipo operation ya cut ifuate. Baada ya kufanya operation hii maneno yaliyotiwa kivuli yataondolewa kabisa (permanently ) kutoka katika source na yataweza kuwekwa katika destination kwa kufanya operation ya paste.

Cut pia inaweza kutumika kwa folder, folder ni kundi lililokusanya vitu aidha vinavyofanana ama mbalimbali katika sehemu moja kwa lengo la kusaidia upatikanaji wakati vinatafutwa.

(b) Copy
Operation hii imebeba lengo la kunakili kitu kutoka katika source na kupeleka katika destination. Kwa hiyo operation hii husababisha vitu vilivyomo katika source kufanana na vile vilivyopo katika destination.

Soma Makala Hii Inayohusiana : Jinsi ya Kuzuia Kupoteza Makala Katika Blogu Yako (Backup)

Kama ilivyokuwa kwa upande wa cut , vile vile ukihitaji kucopy maneno utahitaji kwanza kuyaweka kivuli ,kisha utayacopy. Hali kadhalika katika folder.

(c) Matumizi
Tumia cut ikiwa unataka kuhamisha au kuondoa kabisa file, document au folder kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine.

Tumia copy ikiwa unataka kuweka nakala sehemu zaidi ya moja kwa ajili ya kuchukua tahadhari na upotevu wa kazi (backup).

(d) Mipaka (Limitations)
Katika cut ikiwa source na destination ni ile ile (yaani si sehemu tofauti) , unapofanya hii operation hautaona mabadiliko itabaki kama ilivyokuwa kabla ya kufanya cut

Katika copy ikiwa source na destination ni ile ile (yaani si sehemu tofauti), unapofanya hii operation itatengenezwa nakala nyingine yenye jina linalofanana na lile la awali likiwa limeongezewa mabano na namba 1 yaani (1). Namba hii inaonesha ni mara ya ngapi umefanya hii operation, ukifanya tena kwa mara ya pili basi itaandika jina kama la awali na kuongeza (2).

Rafiki unaweza kuwashirikisha wengine kuhusu blogu hii kwa ajili ya kupata maarifa mbalimbali na pia unaweza kubofya hapa ili kuweza kupata makala kila inapowekwa kupitia barua pepe yako.

Goodluck Moshi
Author
StadizaMafanikio

0 comments:

Post a Comment