Friday, 18 November 2016

Uchambuzi wa Kitabu cha "ACT LIKE A SUCCESS THINK LIKE A SUCCESS"

Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio!

Steve Harvey ni mchekeshaji maarufu sana ambaye ameanza fani hii kati ya miaka ya 1980. Pamoja na fani hii ya uchekeshaji Steve ameandika vitabu mbalimbali kama Act Like A Lady, Think Like A Man and Straight Talk , No Chaser na Act Like A Success Think Like A Success.

Katika makala hii ya leo natumia kitabu cha Act Like A Success, Think Like A Success kukushirikisha mambo ambayo Steve anasema yakizingatiwa yatakusaidia jinsi ya kutumia kipaji ulicho nacho kwa ufanisi kukupatia mafanikio katika maisha.

1. Tunapotumia vipawa/vipaji vyetu ipasavyo, ulimwengu hutushukuru kwa kutupatia wingi wa utajiri, kwa kuanzia na wingi wa fursa ,wingi wa afya bora na wingi wa utajiri wa kifedha

2. Kipindi unapoamua kupambana na hofu, utagundua kuwa hofu sio kubwa kama ulivokuwa unawaza. Kitu kinachofanya hofu kuwa kubwa ni kama usipogeuka na kukubali kuanza kuzikabili. Na jinsi unavyochukua muda mrefu kukwepa hofu ndivyo zinavyozidi kuongezeka ukubwa katika akili.

3. Kushindwa ni sehemu ya mchakato unapokuwa katika njia ya mafanikio. Kushindwa huibuka kutokana na ukosefu wa mpango wa kifedha, ukosefu wa rasilimali, ukosefu wa watu sahihi katika timu yako.

4. Usiruhusu kushindwa kukusimamishe eneo moja na kuacha kutafuta/kukamilisha ndoto zako.

5. Kila siku unapoamka ni kwa sababu Mungu ana mipango mikubwa kwa ajili yako na bado haijamalizwa/haijatekelezwa

6. Fursa zipo katika maamuzi yako unayofanya

7. Maswali muhimu ya kujiuliza kwa ajili ya kuchagua chombo sahihi cha kukusafirisha kwenda katika mafanikio ya ndoto yako:
a) Wapi ni mwisho wako wa safari?
b) Kituo chako kinachofata ni kipi?
c) Je unajua namna ya kukiendesha chombo chako kwa kiasi ambacho hakitaweza kukupatia ajali(yaani kukuzuia kukua)?

8. Heshimu muda wako na muda wa wengine pia

9. Usiogope kupokea msaada unaohitaji ili kuweza kuishi maisha unayostahili kuishi

10. Mpangilio muhimu unaopaswa kuufata kwa ajili ya mafanikio:
a) Kwanza ni Mungu
b) Pili ni Familia
c) Tatu ni Elimu/Maarifa katika kile unachofanya
d) Nne ni biashara

11. Mungu ameshawapanga katika foleni watu wote unaowahitaji katika njia yako ya kutimiza ndoto zako na maono yako; unachotakiwa kufanya ni kuwaondoa watu wasio sahihi (wasio sawasawa na maono/ndoto zako

12. Kitu ambacho huhitaji kujua ni jinsi gani hautafanikiwa katika kitu fulani unachofanya; unachohitaji kujua ni jinsi gani utafanikiwa katika kitu fulani unachofanya

Soma Makala Hii Inayohusiana : Uchambuzi wa Kitabu cha " EAT THAT FROG"

13. Kuweka mambo katika matendo ndiyo dawa ya kusonga mbele

14. Kumbuka sio kila mtu unayeanza naye safari yako anaweza kwenda mpaka mwisho wa safari unayoelekea

15. Kanuni 6 za kukuwezesha kupata NDIO unapoomba kitu unachohitaji:
a) Jua thamani yako
b) Tambua unachostahili
c) Kuwa maalum (specific) na kile unachokihitaji
d) Kamwe usidhani kuwa wanajua unachohitaji
e) Waeleshe maadili yako kwa vitendo
f) Tambua HAPANA haimaanishi umekataliwa

16. Kuwa na ujasiri wa kuingiza ujuzi wako katika fursa ambazo zitakupatia ukuaji au kupanda ngazi katika eneo lako

17. Chagua kuwa makini na kushiriki katika mabadiliko yanayotokea maishani mwako

18. Kwa kadiri unavyoyakubali mabadiliko na kuwa sehemu ya mabadiliko, ndivyo utakavyofanikiwa zaidi

19. Usiruhusu asili yako ikuwekee mipaka

20. Chagua kila siku kutoruhusu wanaowaza hasi kukusimamisha kutumia karama/kipawa alichokupa Mungu

21. Mlinganyo sahihi kwa ajili ya mafanikio:
a) Nyumbani (home)
b) Afya (health)
c) Fedha (finances)

22. Mafanikio si kitu asipokuwepo yule umpendaye ili kuweza kumshirikisha mafanikio uliyoyapata

23. Usiruhusu mtu kuja nyumbani na kuvuruga amani na utulivu ulioutengeneza kwa ajili yako na familia yako

24. Mungu anakubariki ili uwe mtoa baraka

Rafiki unaweza kuwashirikisha wengine kuhusu blogu hii kwa ajili ya kupata maarifa mbalimbali na pia unaweza kubofya hapa ili kuweza kupata makala kila inapowekwa kupitia barua pepe yako.

Goodluck Moshi
Author
StadizaMafanikio

0 comments:

Post a Comment