Thursday, 10 November 2016

Mambo Matano (05) Yaliyojificha Katika Mafanikio Yako

Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio!
Rafiki watu wengi wamekuwa wakipima mafanikio kwa kiwango cha vitu vinavyomilikiwa na mhusika. Kutokana na hili kunakuwa na maana mbalimbali kwa kila mtu kuhusu mafanikio. Leo ninapenda kukushirikisha mambo ambayo utayakuta katika kila mafanikio.



(a) Lengo
Kutokuwa na lengo ni adui mbaya sana wa mafanikio. Chochote unachofanya kinakuongoza kuelekea katika kutimiza lengo fulani. Ni muhimu kuwepo kwa lengo sababu litasababisha uwe kwanza  na nguvu ya kukusukuma na pili uwe na fikra za ubunifu ambazo zinakupeleka hatua fulani ya kufikia lengo. Lakini pia kunakuwa na hali ya kuridhika wakati upo katika mchakato wa kufikia lengo.
(b) Safari ya mafanikio ina kupanda na kushuka.Siku zote au vipindi vyote haviwezi kufanana. Kuna vipindi vitafika utakuwa unakutana na hali ya kushindwa ,hii isiwe sababu ya wewe kuamua kuchoka na kukata tamaa bali ni ushahidi kuwa mafanikio yanahitaji juhudi au bidii , na mafanikio siyo rahisi kama unavyofikiri. Na mtu yoyote ambaye hataki kupokea vipindi vya kushindwa katika safari yake hayuko tayari kupambana ili kuweza kuonja ladha ya mafanikio.
Ukiweza kushinda hali hii, utakuwa umeishinda hali ya kufanya mambo kwa kawaida (mediocre) , utajenga ujasiri, na utaongeza uwezo wako wa kupokea (absorb) kushindwa.
(c) Gharama
Hakuna mafanikio ambayo utayapata bure. Furaha ya mafanikio imo ndani ya jitihada iliyowekwa kufikia mafanikio.Gharama na mafanikio ni vitu ambavyo vinakwenda pamoja au sambamba hauwezi kuvitenganisha.
(d) Kuridhika
Mafanikio ni muhimu yakufanye upate furaha ya ndani (inner joy au satisfaction). Mtazamo imewekwa sana kupima mafanikio kwa kiwango cha vitu vinavyomilikiwa. Ikiwa hata mafanikio yamefikiwa kwa machozi ni muhimu yavishwe yako la furaha inayotoka ndani yaani kuridhishwa na hatua uliyofikia, na hii inasaidia kutambua kiwango cha jitihada kilichokufikisha katika ngazi ya mafanikio husika.
(e) Imani
Kwa wewe kuwepo hapa duniani kuna kusudi maalum ambalo aliyekuumba anataka ulitimize hapa duniani. Ni muhimu ufahamu mafanikio unayoyapata pia yanaletwa na kusababishwa na uwepo wa aliyekuumba katika kuyapata mafanikio. Kwa kutegemeana na imani yako ni muhimu kutambua uhusiano huo uliopo kati ya maisha yako au malengo makubwa ya maisha yako (greater purpose) na mwandishi wa hayo malengo (author of greater purpose au maker).
Kama ambavyo alama za vidole (finger prints) zilivyo pekee kwa kila mtu haziwezi kufanana na mtu mwingine yoyote, basi mafanikio pia kwa kila mtu yako pekee. Tunachohitaji ni ujasiri wa kufanikiwa na kuwa vile ambavyo tumekusudiwa na aliyetuumba kuyafikia mafanikio.
Rafiki unaweza kuwashirikisha wengine kuhusu blogu hii kwa ajili ya kupata maarifa mbalimbali na pia unaweza kubofya hapa ili kuweza kupata makala kila inapowekwa kupitia barua pepe yako.
Goodluck Moshi
Author
StadizaMafanikio

Related Posts:

  • Usifanye Kosa Hili Katika BiasharaUnapoamua kuchagua kuwa utashirikiana na mtu mwingine kufanya biashara ya ndoto yako, usitumie kigezo cha huyo mshirika kuwa ni mmoja wa wanafamilia wako au ni mmoja wa marafiki zako wa karibu sana, utakuwa umejiingiza katika… Read More
  • Je, Unajua?Ni bora kufanya kitu kisicho kamili kuliko kutokufanya chochote kisicho na dosari Better to do something imperfectly than to do nothing flawlessly… Read More
  • Tazama Kushindwa kwa Jicho HiliKushindwa hakuamaanishi wewe ndiye uliyeshindwa bali kunamaanisha hujafanikiwa bado Kushindwa hakumaanishi haukutimiza/haujafanikisha kitu bali kunamaanisha umejifunza kitu Kushindwa hakumaanishi wewe ni mjinga bali kunamaa… Read More
  • Fanya Haya ili Ukue1. Usitamani mambo yangekuwa marahisi, tamani ungekuwa bora mno Don't wish it were easier; wish you were better 2. Usitamani ungekutana au ungekuwa na matatizo machache,tamani ungekuwa na ujuzi zaidi Don't wish for less prob… Read More
  • Usipuuze TatizoMatatizo mengi kamwe hayatatuliwi au hayadhibiti kwa ufanisi kutokana na kutoyapa uzito wa kutosheleza. Hakuna tatizo ambalo halina umuhimu kiasi kuwa hatuhitaji kujali kuhusu hilo tatizo. Mfano kwa mwanafunzi inawezekena hap… Read More

0 comments:

Post a Comment