Monday, 14 November 2016

Uchambuzi wa Kitabu " HOW SUCCESSFUL PEOPLE THINK"

Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio!
John C. Maxwell ni mmoja wa waandishi maarufu ambao amedumu akitushirikisha mambo mbalimbali ambayo amejifunza katika maisha yake. John ni mwanafalsafa mzuri sana katika eneo la Uongozi. Hapa chini ninakushirikisha maarifa machache kwa muhtasari ambayo nimejifunza kutoka katika kitabu chake cha "HOW SUCCESSFUL PEOPLE THINK".



1. Ikiwa utabadili namna unavyofikiri, utabadili maisha yako
2. Kufikiri vema huleta faida tatu:
a) Kutengeneza mapato
b) Kupata ufumbuzi wa matatizo
c) Kutengeneza fursa
3. Tunahitaji kuwa na sehemu maalum tuliyoitenga kwa ajili ya kufikiri, sehemu hii ni ile ambayo itakufanya uweze kucapture mawazo yote mazuri na mema kutoka kichwani mwako na kuyahamisha katika karatasi kwa ajili ya hatua zaidi bila ya kuwa na usumbufu wowote
4. Ili kuweza kufikiri vizuri unahitaji kuwa makini na inputs unazozipata kupitia vitu unavyovisoma, unavyovisikiliza au unavyovitazama. Kupitia hizi inputs unaweza kunote vile vitu ambavyo unaona ni mawazo yanayoweza kukusogeza hatua moja mbele
5. Unapofikiri wazo vema linahitaji hatua moja zaidi ya kuliboresha kwa kujaribu kulifanyia uchunguzi wa kina kuweza kuona namna ambavyo linaweza kwenda katika uhalisia wa kutekelezeka
6. Unapokuwa na wazo sahihi, unatakiwa uwashirikishe watu sahihi kwa ajili ya wazo husika, wazo pia lazima lishirikishwe katika mazingira sahihi, muda pia unatakiwa uwe sahihi kwa ajili ya wazo hilo, na sababu ni lazima iwe sahihi, hakuna namna ambavyo hilo wazo halitakuwa kubwa zaidi na kutoa matokeo sahihi
7. Ili kuweza kujifunza na kukua kwa mafanikio inatakiwa kujua maswali ambayo utawauliza watu wanaojua vitu vingi kuliko wewe unavyovifahamu na pia namna ya kuweka katika matendo yale majibu wanayokupatia katika maisha yako
8. Ni vizuri kuwa na agenda kabla ya maongezi na mtu yoyote itakusaidia kuyaongoza maongezi katika kujifunza kwa kina
9. Namna nzuri ya kuamua vipaumbele:
a) Kuelekeza nguvu zako katika vitu ambavyo vitatumia kwa ubora zaidi strengths zako na vipaji alivyokuzawadia Mungu
b) Kufanya vitu ambavyo vinakupatia matokeo makubwa na tuzo/malipo makubwa
c) Wekeza asilimia 80 ya juhudi zako katika asilimia 20 ya kazi zenye umuhimu zaidi
d) Kuelekeza umakini katika fursa za kipekee zenye matokeo makubwa mno
10. Unapofikiri kwa umakini (focused thinking) inakusaidia pia kutambua ndoto yako katika maisha ikiwa hujaweza kuitambua
11. Jitahidi kuwa na ubora sana katika vitu vichache kuliko kuwa na utendaji bora katika vitu vingi
(Strive for excellence in a few things rather than a good performance in many)
12. Namna ya kujizuia na vitu vinavyoweza kuondoa umakini katika shughuli unayoitenda:
a) Dumisha nidhamu ya kuzingatia vipaumbele vyako
b) Jizuie na vitu vinavyokuletea usumbufu
13. Kuna thamani kubwa sana katika kuunganisha wazo moja na wazo jingine haswa pale ambapo mawazo yanayounganishwa hayahusiani
14. Ubunifu ni uwezo wa kuona kila kitu ambacho kila mmoja amekiona, kufikiri tofauti ambavyo hakuna aliyefikiri hivyo na kutenda tofauti na ambavyo hakuna aliyetenda hivyo
15. Tumaini sio mkakati
16. Ukiwa na tumaini pekee inamaanisha kufanikiwa kwako kuko nje ya uwezo wako
17. Mabadiliko pekee hayawezi kuleta ukuaji, ila pia ukuaji hauwezi kutokea bila mabadiliko
18. Ukweli utakuweka huru, ingawa kwanza utakufanya ukasirike
19. Unahitaji kuitazama kiuhalisia ndoto yako ili kujua vitu vinavyohitajika ili kuweza kuikamilisha/kuifanikisha
20. Maswali muhimu ya kujiuliza unapounda mpango mkakati:
a) Kitu kinachofuata kufanywa na kwa nini?
b) Nani anawajibika kwa ajili ya kitu gani? Na nani anawajibika lwa nani?
c) Nini makisio yetu ya mapato na matumizi?
d) Je tupo katika lengo?
e) He tunafanikiwa kupata ubora tunaotazamia na mahitaji yetu?
f) Je tunawezaje kuwa na utendaji bora zaidi na ufanisi zaidi katika kuelekea kulifanikisha jambo kiuhalisia?
21. Ni vizuri kuoanisha/kulinganisha kati ya mkakati na tatizo husika linalotafutiwa ufumbuzi
22. Mwongozo unaohitaji katika kutengeneza na kutekeleza mipango ya kukuwezesha kufikia malengo yako:
a) Vunjavunja suala husika katika vipengele vidogo vinavyoweza kusimamiwa. Kuvunjwavunjwa kwa suala kunaweza kufanyika kwa kutegemea ratiba, kusudi, kazi (function), wajibu au kwa mbinu/njia nyingine
b) Jiulize kwa nini kabla ya kujiuliza jinsi/namna gani. Inasaidia kukupatia sababu kwa ajili ya maamuzi yako. Itafungua akili yako kwa ajili ya uwezekano na fursa. Ukubwa wa fursa unaamua kiwango cha rasilimali na jitihada unayohitaji kuwekeza.
c) Kusanya taarifa za kutosheleza zinazofafanua suala husika katika uhalisia wake.
d) Fanya mahesabu kuhusu rasilimali ulizonazo. Una muda kiasi gani? Una fedha kiasi gani? Una vifaa gani? Una mali gani nyingine?
Madeni au wajibu gani utakaojitokeza? Watu gani wanaohitajika kuunda timu ili kuweza kukamilisha lengo?
e) Unapoanza kutengeneza mpango anza na masuala yaliyo dhahiri/wazi
f) Kuwa na watu sahihi katika sehemu/mahali sahihi
23. Jifunze kutafakari kwa ajili ya kujifunza kutoka katika mafanikio na kushindwa kwako kulikotangulia, gundua kipi unatakiwa kujaribu kurudia, na amua kipi unatakiwa kubadilisha
24. Adui mkubwa wa mafanikio yako ya kesho ni mafanikio yako ya leo
25. Watu wengi sana wameridhishwa na matatizo ya zamani kuliko nia ya kutafuta ufumbuzi mpya
26. Awamu tatu za maisha:
a) Moja ya tatu ya kwanza inakwenda katika elimu  (Education)
b) Moja ya tatu ya pili katika kutengeneza ujuzi na maisha (Building Career and Making Living)
c) Moja ya tatu ya mwisho ni kwa kujitolea kwa shukrani (Returning something in gratitude)
27. Maswali mawili ya kutathmini nia yako:
a) Unapoamka asubuhi jiulize ni kitu gani chema/kizuri unaenda kufanya leo?
b) Unapoenda kulala jiulize ni kitu gani chema/kizuri umekifanya leo?
Rafiki unaweza kuwashirikisha wengine kuhusu blogu hii kwa ajili ya kupata maarifa mbalimbali na pia unaweza kubofya hapa ili kuweza kupata makala kila inapowekwa kupitia barua pepe yako.
Goodluck Moshi
Author
StadizaMafanikio

0 comments:

Post a Comment