Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio!
Keith Cameron Smith ni mwandishi wa kitabu "THE TOP TEN DISTINCTIONS BETWEEN WINNERS AND WHINERS ". Keith anatushirikisha mbinu ambazo washindi wamekuwa wakizitumia kila mara wanapokuwa wanafanya kazi yoyote ili kuwasaidia kuwapa ushindi. Keith anasisitiza kuwa adui mkubwa anayechangia katika kushindwa ni tabia ya ulalamikaji, hali ya kukataa kuwajibika.
Keith anaamini kwa kusoma kitabu hiki ni njia mojawapo ya kuweza kukushirikisha mambo chanya yatakayochangia katika kukufanya uwe mshindi. Hivyo katika makala napenda kukushirikisha mambo ambayo nimeyapata kutoka katika kitabu hiki.
1. Kuwa mshindi sio tukio linalotokea katika muda mfupi, ni safari ndefu ya maisha
2. Maisha hayakwendi sawa sawa na mipango inasemekana maisha ni vile yanavyokwenda wakati unaendelea kupanga mipango
3. Uwajibikaji ni kufanya kile kilicho bora kwa nafasi yako au uwezo wako ukiwa na imani kuwa utapata matokeo mazuri
4. Ushindi ni mchezo unaohitaji timu na umoja
5. Hofu ni imani ya kuwa kitu kibaya kabisa kitatokea
6. Hofu imejengwa katika mizizi kuwa hauna machaguo
7. Ili uweze kuwa mshindi unahitaji kuwajibika kwa kufanya uchaguzi wa imani chanya zidi ya hofu
8. Washindi hujua kuwa daima wana machaguo na wanawajibika na hayo machaguo
9. Machaguo yanaamua hali, hali haiamui machaguo
10. Ni sahihi kusikitika kuhusu mategemeo fulani lakini si sahihi kukata tamaa
11. Ushindi huanza na mawazo na kuwaibika kufanya machaguo yale yaliyo chanya tuu
12. Washindi wana mtazamo wa mawazo yao ndio mbegu, na akili yao ndio udongo wa kukuzia mbegu, mawazo unayoyaweka katika akili yako huota mizizi na kisha kukua kuwa mti unaozaa matunda, kwa hiyo ni muhimu sana kuchagua ni mawazo ya aina gani unayoyaruhusu kukaa akili mwako
13. Washindi huamini wanawajibika na matokeo wanayoyapata
14. Kwa kudhibiti mawazo yako unabadilisha matokeo yako, washindi huwajibika kwa matokeo yao kwa kudhibiti mawazo yao
15. Washindi wako tayari kulipia gharama inayohitajika ili waweze kushinda
16. Washindi hujifunza kutoka kwa wale walio bora zaidi yao kufanya vile wanavotakiwa kuvifanya ili kufikia hatua kama za hao walio mbele yao
17. Inawezekana ukajifunza na kupata kile unachotamani kukipata
18. Gharama kubwa washindi wanayolipa ni kupata maarifa
19. Mipaka uliyonayo katika kufanikiwa ni kwa sababu ya kukosa maarifa, waliofanikiwa zaidi yako ni kwa kuwa wana maarifa ambayo hauna na pia wameamua kuweka katika matendo yale maarifa waliyoyapata
20. Gharama nyingine inayolipwa na washindi ni upinzani, washindi hawajali watu wengine wanawafikiriaje bali wanajali wao wenyewe washindi wanajifikiriaje binafsi
21. Washindi hawawasikilizi wapinzani bali wanasikiliza mioyo/nia yao inavowaelekeza
22. Watu hawana muda na maisha yako hata kukufikiria, hata pale mtu anapokuwa mpinzani wako dakika tano baadae hata hana mawazo kuhusu wewe
23. Washindi wako tayari kulipa gharama ya kuwahudumia wengine kwa moyo mmoja kwa sababu kwa kuwahudumia wengine kupata kile wanachokihitaji kunakusaidia kuweza kupata chochote unachohitaji
24. Ongeza maarifa juu ya kile unachokitaka katika maisha yako, wapuuzie wapinzani na wahudumie watu kwa moyo mkunjufu
25. Malipo ya gharama hayatupatii tunachokitaka bali yanatupa fursa ya kukipata ( The payments don't give you what you want they only give you the opportunity to get it)
26. Usiruhusu mtu akuambie nini huwezi kufanya, ukihitaji kitu nenda ulipe gharama unayohitaji ukipate
27. Washindi huamini kuna njia ya kutupeleka katika mafanikio kwa kila jambo
28. Washindi hutazama matokeo wanayoyataka kwa umakini, wakiona hawajapati kama wanavotarajia wanarekebisha matendo yao (actions) hadi waweze kupata matokeo wanayoyahitaji
29. Washindi hulisha imani yao na kuifisha hofu
30. Kwa kawaida maono hutuonesha mwisho wa safari
31. Baadhi ya masomo utakayojifunza wakati was kuelekea mafanikio yako ni kushindwa, kukataliwa na kupoteza vitu.
32. Washindi hawalalamiki bali huthamini maisha. Huthamini kwa kuongea vitu vizuri vilivyotokea awali, vinavyotokea sasa na vitakavyotokea baadaye
33. Changamoto ya mabadiliko katika maisha
Nenda kwa siku kumi mfululizo bila kulalamika, ikiwa utalalamika kabla ya siku kumi hazijaisha bila kujali upo siku ya ngapi utakuwa umefuta zile siku zote ambazo ulifanikiwa kupita bila kulalamika kwa hivyo unatakiwa uanze mpya
Nenda kwa siku kumi mfululizo bila kulalamika, ikiwa utalalamika kabla ya siku kumi hazijaisha bila kujali upo siku ya ngapi utakuwa umefuta zile siku zote ambazo ulifanikiwa kupita bila kulalamika kwa hivyo unatakiwa uanze mpya
34. Unahitaji kuwa msikivu zaidi kuliko unavyoongea, sikiliza kwa lengo la kuelewa unachoambiwa na si kwa lengo la haraka ya kujibu ulichokuwa unaambiwa
35. Kama unapitia wakati mgumu sasa kuna uwezekano mkubwa kuna baraka zilizojificha
Rafiki unaweza kuwashirikisha wengine kuhusu blogu hii kwa ajili ya kupata maarifa mbalimbali na pia unaweza kubofya hapa ili kuweza kupata makala kila inapowekwa kupitia barua pepe yako.
0 comments:
Post a Comment