Sunday, 6 November 2016

Uchambuzi wa Kitabu cha " SUCCESS SECRETS OF THREE TIME OLYMPIAN"

Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio!




Ruben Gonzalez ni mwandishi wa kitabu "SUCCESS SECRETS OF THREE TIME OLYMPIAN" . Katika kitabu hiki ameeleza mambo ambayo amekuwa akiyafuatilia na kujifunza kutoka kwa watu waliofanikiwa. Baada ya kujifunza alianzia  kuweka katika matendo yale ambayo alijifunza kutoka kwa watu waliofanikiwa, na hatimaye kanuni au mbinu zile zile zilimsaidia kufanikiwa pia. Hapa ni nakushirikisha mbinu au kanuni ambayo Ruben ameyaleeza.
1. Fanya maamuzi leo ya kuwa mwanamafanikio kwa kuwa tayari/nia ya kulipa gharama inayohitajika ili kuweza kufikia ndoto yako
2. Mafanikio hayapimwi na hatua uliyofikia leo bali hupimwa na vizuizi ambavyo umevivuka mpaka kufikia mafanikio
3. Watu waliofanikiwa hujiandaa na kujiweka katika nafasi sahihi kuweza kutumia fursa yoyote ambayo inaweza kujitokeza kuwasaidia katika safari ya mafanikio
4. Mtazamo wako juu ya jambo fulani unaamua kiwango chako cha kufanikiwa, kufikiri chanya kunakupa njia nyingi za kuweza kukusaidia kufanikiwa
5. Jipe nafasi ya kujifunza ujuzi, maarifa yanayoweza kukufikisha kupata ndoto zako
6. Iruhusu sheria ya wastani ifanye kazi katika maisha yako, kwa kadiri unavyoshindwa katika jambo fulani unapata mafunzo mengi ambayo yatakusaidia kufanikiwa kutokana na kujaribu njia nyingi za kufanikiwa
7. Unahitaji kujiamini wewe mwenyewe na kuamini kuwa utafikia ndoto yako.
8. Unapokuwa na mtazamo wa kuwa na utayari wa kufanya lolote linalokuhitaji bila kujali muda utakaoutumia ili kufikia mafanikio basi   kufanikiwa ni suala ambalo la kitambo kidogo
9. Vinaweza vikachakuliwa vitu vyote katika maisha yako ukabaki hauna kitu lakini kitu kimoja hubaki na wewe muda wote ni nguvu ya kuchagua, chagua leo namna unavyoitikia (react) katika hali yoyote inayokutokea
10. Daima weka malengo yako mbele yako
11. Fikiria mawazo ambayo yatakuhamasisha kufikia malengo kwa kuwa like unachokifikiria muda wote ndicho kitakachokutokea katika uhalisia
12. Kila kitu hutokea kwa sababu, changamoto tunazopata katika safari ya mafanikio ni kwa ajili ya kutupatia masomo makubwa ya kujifunza ili kuweza kuwa na uuanzaji sahihi katika jambo tunalofanya na pia kuweza kufikia mafanikio
13. Unahitaji kuwekeza nguvu zako katika lengo moja mpaka ufanikiwe ndio uelekeze nguvu zako katika lengo lingine mpaka malengo yako yote yaishe/yakamilike, usielekeze nguvu katika lengo zaidi ya moja kwa kuwa kiwango cha kufanikiwa kitapungua
14. Ujasiri hutokana na muda ambao umewekeza katika masaa, siku ili kujijengea maarifa na ujuzi wa kuwa bora katika fani unayoifanya
15. Changamoto kubwa kuliko zote kuelekea kufanikiwa ni kujitawala mwenyewe, utashawishika kufanya vitu ambavyo vitakuweka nje ya mstari wa Mafanikio, lakini siku zote katika Yale unayofanya jiulize swali moja kuwa je unachokifanya kinakusaidia kukusogeza Karibu na kufanikiwa
16. Jifunze masuala ya uongozi na uwasaidie wengine kwa kuwajenga kiujuzi ili waweze kuwa na ujasiri wa kuungana na timu yako ili kuweza kukusaidia kufikia mafanikio yako
17. Ujasiri katika kufanikiwa hutokana na utayari wa kuweka mambo katika matendo na kuvumilia.
18. Bila kujali shida unayoipata ni ya namna gani jifunze kuiongelesha na kuiambia kuwa wewe ni mkubwa mno kuliko hiyo shida na haitaweza kukushinda
19. Kila Mafanikio makubwa ni mjumuisho wa mafanikio madogo madogo
20. Jifunze kutokana na makosa yako, fanya marekebisho yanayohitajika alafu jiweke katika nafasi sahihi ya kutumia fursa inayokuja mbele yako
21. Shauku yako ya kufanikiwa itakupa nguvu ya kukusaidia usiachie njiani unachokihitaji na pia itakupa njia za kuweza kufanya ili ufanikiwe
22. Fanya zaidi ya kile kinachotarajiwa
23. Ukiamini kuwa unachokitaka kuwa kinawezekana na ukatenda mambo ambayo yanasaidia kukfanikisha unachotaka, ulimwengu nao utakusaidia kufanya ndoto, mipango na matarajio yako katika uhalisia
24. Tumaini hutuonyesha vile visivyoonekana na kutupatia vile visivyowezekana
25. Usiruhusu hofu ikutawale, hofu inatawaliwa kwa kutenda yale unayoyahofia
26. Usijudge siku kwa mavuno uliyoyapata bali judge kwa mbegu uliyootesha/uliyopanda
27. Ulimwengu daima humpatia mtu fursa ya kufanikiwa ikiwa maneno na matendo yake yanaonesha anajua anapoelekea
28. Kila siku kitu cha kwanza andika malengo yako
29. Amua kuwa mwanafunzi wa kudumu wa mafanikio
30. Vitabu unavyosoma na watu unaokutana nao vinaamua wapi utakuwa miaka mitano ijayo
31. Furaha ni zao la mambo matatu:
a) ubora wa mahusiano na watu wako muhimu
b) kiwango cha kudhibiti hisia zako
c) kutumia vipawa vyako kufikia malengo yako
32. Haijalishi unaanguka mara ngapi katika safari ya Mafanikio simama endelea na safari
33. Watu waliofanikiwa wanawekeza muda wao kutafuta njia za kufanikiwa zaidi
34. Fall in love with the process of making you succeed
35. Tafuta watu ambao wana ujuzi na rasilimali ambazo unahitaji ili kuweza kufikia mafanikio unayoyahitaji
36. Tafuta mshauri au kocha ambaye ataharakisha mafanikio yako
37. Leaders make decision all time. Followers make suggestions.
38. Kama unapitia mapambano katika maisha , unaandaliwa kwa ajili ya malengo makubwa na muhimu
39. Viongozi wapo tayari kufanya lolote linatakiwa kufanywa na wao ili kuboresha matokeo
40. Hauwezi kufanikiwa kupata kitu kikubwa katika maisha mpaka utakapoanza kuamini kuwa kuna kitu kikubwa ndani yako kuliko hali au mazingira unayoikabili
Rafiki unaweza kuwashirikisha wengine kuhusu blogu hii kwa ajili ya kupata maarifa mbalimbali na pia unaweza kubofya hapa ili kuweza kupata makala kila inapowekwa kupitia barua pepe yako.

0 comments:

Post a Comment