Wednesday, 9 November 2016

Hatua Zitakazokusaidia Kukabili Changamoto Zinazokuzuia Kupata Mafanikio

Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio!

Rafiki unahitaji kufahamu haitatokea kuwepo kwa mtu ambaye ataishi au atapata mafanikio kwa ajili yako au kwa niaba yako. Mambo yote ambayo unayohitaji iwe ni mafanikio au vitu, unahitaji kuwajibika kuvitafuta kwa ajili yako binafsi.



Utakuwa unafanya makosa makubwa sana ikiwa utaamua kuridhika na hali uliyo nayo na kukubali kuwa dunia ndiyo itaweka jitihada kwa ajili ya kuboresha hali yako.Unahitaji kuweka jitihada binafsi ili kubadili hali uliyonayo au unayoipitia kwa sasa.


Soma Makala Hii Inayohusiana: Jambo Moja la Kuzingatia Ili Kuwa Tajiri


Tumaini kubwa ambalo unahitaji kulijua bila kujali umeathiriwa kwa kiwango gani na changamoto, bado unayo nafasi ya kuamua kujifunza jinsi ya kuinuka kutoka katika hizo changamoto, kusimama tena na kusonga mbele.

Kitendo cha kuinuka na kusonga mbele kinabeba kwanza ujumbe wa kujitegemea (self reliance au independence). Na hii ni moja ya kiungo muhimu sana ambacho kitakusaidia kutoka zaidi ya maeneo yako uliyoyazoea (comfort zone). Lakini pia  hii itachangia kujua ukomo wa uwezo wako na kupata watu wengine ambao wataungana na wewe kukusaidia (dependence) kutokea pale ulipoishia kulikosababishwa na uwezo wa juhudi zako.

Utapata hamasa ya kutafuta majibu ya maswali mengi sana ambayo utakutana nayo, lakini rafiki suala la kutafuta majibu ni sawa na kufanya hitimisho (conclusion), badala yake unashauriwa uulize maswali zaidi, kitendo cha kuuliza maswali kinasaidia kukusanya taarifa zaidi (facts) , ambazo pia zitakusaidia kupata sababu ya majibu au hitimisho kuwa vile lilivyo.

Rafiki ili kuweza kupangilia vizuri maisha yako ya baadae ni muhimu kutazama maisha yako miaka ya nyuma yathamini,yakubali , shukuru kwa ajili ya mafunzo yaliyokupatia na kusonga mbele.

Rafiki unaweza kuwashirikisha wengine kuhusu blogu hii kwa ajili ya kupata maarifa mbalimbali na pia unaweza kubofya hapa ili kuweza kupata makala kila inapowekwa kupitia barua pepe yako.

Goodluck Moshi
Author
StadizaMafanikio

0 comments:

Post a Comment