Tuesday, 8 November 2016

Vigezo Vitatu (03) Vya Kuzingatia Kabla ya Kupublish Makala Katika Blogu

Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio!

Rafiki kwa kila msomaji ambaye amechagua kutembelea blogu yako hakika ni fursa ya kipekee mno kwako, kwa sababu kwanza kati ya masaa 24 aliyonayo katika siku ameamua kutenga sehemu ya muda  kupata maarifa kupitia blogu yako, lakini pili ni kuwa kati ya blogu nyingi ambazo angeweza kwenda kutembelea ameamua kuchagua blogu yako kwa ajili ya kupata maarifa.



Katika makala ya leo ninapenda kukushirikisha vigezo vitatu ambavyo unapaswa kuhakikisha unazingatia kabla ya kuiweka hewani (publish) makala yoyote unayoandika katika blogu yako.



(a) Utofauti au upekee (distinction)
Hii ni thamani au kigezo namba moja ambacho kila makala unayoandika hakikisha imebeba. Tengeneza mikakati na malengo maalum ya kuhakikisha kazi yako inakidhi kigezo hiki. Fanya homework ya kutosha kutembelea waandishi wengine na kujifunza mambo kama vile wanaandika nini, wanatumia staili gani ya uandishi na kadhalika.
Usishawishike na kukopi makala au aina ya uandishi wa mwandishi mwingine kwa kuwa tayari ana wasomaji wengi, bali angalia namna ambavyo unaleta kitu kipya ambacho wasomaji wamekuwa hawakipati (tafuta pengo au gap).
Upekee katika uandishi wako ndiyo silaha pekee ambayo itatofautisha makala zako na za waandishi wengine zinapowekwa pamoja.

(b) Ubora (Excellence)
Hii ni thamani au kigezo namba mbili ambacho kila makala unayoandika hakikisha imebeba. Hakikisha unaweka jitihada kubwa ya kutosheleza kutoa kilichobora mno ndani yako ,penda makala unazoandika na wasomaji wako kwa kuzifanya  kuwa bora kuliko makala zako zilizotangulia au makala za waandishi wengine.
Kiwango cha ubora kinatakiwa kupanda siku hadi siku, kamwe usiridhike kutokana na idadi ya mashabiki au wasomaji wako kupitia mrejesho wanaokupatia. Hii ni mbinu pekee itakayokusaidia kuendelea kubaki na wasomaji kutokana na kuwa na uboreshaji endelevu au usio na kikomo. Usibaki na kitu ndani yako (die empty).

(c) Huduma (World - Class Service)
Hii ni thamani au kigezo namba tatu ambacho kila makala unayoandika hakikisha imebeba pia. Makala unayoandika hakikisha inamuhudumia msomaji katika kiwango sawasawa na mahitaji yake au kupitiliza mahitaji yake lakini isiwe kiwango cha chini kuliko mahitaji yake. Kupitia maandishi unayoandika hakikisha yana mtiririko mzuri, hayana makosa ya uandishi (grammar), umetumia lugha rahisi inayoeleweka kwa msomaji ili kumwezesha kupata maarifa ambayo yatachangia kuboresha maisha yake. Akili na moyo ujikite (focus) katika kile unachoandika kama fursa ya kuhudumia wasomaji .Na hakikisha unatumia fursa vizuri kwa kufanya kilicho sahihi kwa msomaji.
Mambo haya matatu ni muhimu yaende kwa pamoja bila kuacha lolote.

Soma Makala Hii Inayohusiana: Kanuni Kumi (10) za Huduma Bora Kwa Mteja

Rafiki unaweza kuwashirikisha wengine kuhusu blogu hii kwa ajili ya kupata maarifa mbalimbali na pia unaweza kubofya hapa ili kuweza kupata makala kila inapowekwa kupitia barua pepe yako.

Goodluck Moshi
Author
StadizaMafanikio

Related Posts:

  • Msingi wa kutimiza maisha yenye ufanisiUwezo uliopo ndani yetu ni mkubwa sana kuliko kile ambacho tumeshakitendea haki kwa nafasi zetu tulizonazo kwa kutendea ulimwengu. Maswali haya yatakusaidia kutafakari kitu gani ambacho unacho ndani yako bado hujakileta ulimw… Read More
  • Maliza Robo ya Kwanza 2015 Hivi Hatua 3 muhimu unazohitaji kuzichukua ili kuweza kutumia muda wako kwa ufanisi na kupata matokeo ya ndoto yako kwa haraka: 1. Have a Plan Kuwa na mpango wa kina unaoanisha nini unachotaka kufanya na mpango huu ni lazima uw… Read More
  • Uwekaji Mipango UsioaminikaNi asili yetu kuwa na matumaini mema juu ya jambo fulani ambayo yamepitiliza uhalisia. Mfano tunadhani kuwa tutafanya mambo mengi kwa muda mchache kuliko inavyotakiwa kiuhalisia au kudhani jambo unalolifanya litachukua muda m… Read More
  • Fursa nyingi, Muda mchache na Rasilimali chache, Nifanyaje?Ukifanya uchambuzi kwa kulinganisha kundi la "shughuli na fursa" na kundi la "muda na rasimali" utapata hitimisho ya kuona katika kundi la "shughuli na fursa" zipo nyingi kuliko kundi la "muda na rasilimali" tulizonazo kwa aj… Read More
  • Usipobadilika, utamezwa na mabadilikoYanapotokea mabadiliko jifunze kukabiliana nayo (kuadapt) kwa haraka vinginevyo utakavochelewa zaidi kwa kutafakari nini cha kufanya na kulialia na hali halisi utatumia gharama kubwa kuyapokea na muda utakuwa umekwenda pia. … Read More

0 comments:

Post a Comment