Sunday, 13 November 2016

Namna ya Kutambua Dalili Za Kushindwa

Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio!
Rafiki gari linapopelekwa kwa fundi kwa ajili ya kutatua tatizo lililo nalo, litaweza kutatuliwa ikiwa tuu kisababishi cha tatizo husika kimefahamika . Ila pia ukienda kwa daktari wa binadamu ukiwa dhaifu , ataweza kukupatia matibabu sahihi baada ya kugundua dalili za tatizo husika. 



Kwa upande mwingine katika maisha yetu unaweza kuwa unashindwa katika kila kitu unachofanya na ukakosa mtu wa kukusaidia kuvuka hiyo hali kwa sababu tuu ya kutoa visingizio (excuse) au sababu zilizokusababishwa ushindwe.
Mambo haya yanaweza kuwa yanaumiza lakini ni bora na sahihi kufahamu ukweli ambao umekuwa hujui na namna ambavyo unaathiri fursa yako ya kufanikiwa.
Soma Makala Hii Inayohusiana : Jinsi Ya Kuishinda Hofu Uliyonayo
Kufanya jambo chini ya uwezo ulionao au kufanya tofauti na mpango uliokuwa umejiwekea ni moja ya dalili itakayokupelekea. kushindwa. Hali hii inachangiwa sawa na kujidanganya kwa kukubali maoni ya marafiki au mambo ambayo umeshafanikiwa kuyapata.
Ili kuweza kuepuka hali hii hakikisha unafanya jambo lolote kwa uwezo wako wote na kuzingatia mpango uliouweka katika kufanikisha jambo husika.
Kufanya jambo kana kwamba una muda wa miaka elfu ya kuishi ni dalili nyingine itakayokupelekea kushindwa. Na hapa utakuta kwa chochote unachofanya utakuta unafanya kama vile unayo masaa yakutosha au wakati mwingine unatumia muda wako muhimu katika mambo muhimu bila kujali kuwa muda upo na ukomo.
Ili kuweza kuepuka hali hii hakikisha unatumia muda wako vizuri kwa kuchagua kufanya yale mambo muhimu ambayo yatachangia katika kukusogeza hatua ya kutimiza malengo yako, na epuka kufanya mambo yasiyo ya msingi.
Kukubali kuchukua jambo ambalo unajua linazidi uwezo wako wa kulitenda ni dalili nyingine itakayokupelekea kushindwa. Sababu ujuzi na maarifa uliyonayo hayakidhi uwezo wa kulibeba jambo. Hivyo hata kama utalichukua ujue utafanya chini ya kiwango au utafanya bila mafanikio.
Ili kuweza kuepuka hali hii ikiwa umechukua jambo linalozidi uwezo wako hakikisha una mpango mkakati wa kukuwezesha kupandisha uwezo wako wa kimaarifa na kiujuzi utakaoweza kuhimili ukubwa wa jambo unapokwenda.
Rafiki unaweza kuwashirikisha wengine kuhusu blogu hii kwa ajili ya kupata maarifa mbalimbali na pia unaweza kubofya hapa ili kuweza kupata makala kila inapowekwa kupitia barua pepe yako.
Goodluck Moshi
Author
StadizaMafanikio

0 comments:

Post a Comment