Thursday, 3 November 2016

Jinsi ya Kutatua Tatizo la Barua Pepe Kutoingia Katika Inbox

Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio!

Barua pepe ni njia ambayo watumiaji wa kompyuta hutumia kutuma ujumbe kwa njia ya kidigitali. Kuna kampuni za aina mbalimbali ambazo zinatoa huduma hii. Baadhi ya kampuni ni Google, Yahoo na kadhalika. Ili uweze kupokea na kutuma ujumbe kwa njia ya barua pepe ni lazima uwe na akaunti katika kampuni hizi. Akaunti hizi huwa hazihitaji malipo.

Makala Inayohusiana: Faida Nne (04) Unazopata Ukiwa na Akaunti ya Gmail.

Kawaida ujumbe unapoingia katika akaunti yako ya barua pepe unapaswa kukaa katika sehemu inayoitwa inbox. Kwa maana nyingine ujumbe ukiingia sehemu nyingine isipokuwa inbox inakuwa si kawaida. Katika makala hii napenda kukushirikisha hatua unazopaswa kufuata ikiwa utakuta barua pepe imeingia katika sehemu nyingine yoyote badala ya inbox.

(a) Ingia katika akaunti yako ya barua pepe ya Yahoo.

(b) Nenda upande wa kulia juu kuna sehemu ina alama kama ya gia,kisha bofya sehemu iliyoandikwa settings.



(c) Bofya sehemu iliyoandikwa Filters.Katika kiboksi kitakachotokea kunatakiwa kusiwe na kitu chochote.Ikiwa utakuta maandishi yoyote , yachague kwa kubofya maandishi yaliyopo , kisha katika sehemu ya juu bofya sehemu iliyoandikwa Remove



(d) Baada ya hatua (c) bofya kitufe cha Save kilichopo upande wa kushoto chini ili kukamilisha.

Hatua hizi ni kwa ajili ya akaunti za barua pepe za Yahoo tu.

Rafiki unaweza kuwashirikisha wengine kuhusu blogu hii kwa ajili ya kupata maarifa mbalimbali na pia unaweza kubofya hapa ili kuweza kupata makala kila inapowekwa kupitia barua pepe yako

0 comments:

Post a Comment